Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Usilie ndugu hao wanaenda kumalizika kisiasa kama profesa Lipumba , muda ni mwalimu mzuri sana , we subiri Jiwe akose tilioni mbili anazofukuzia uone atakavyowageuka .dah!! yan kiukweli mdee kaniliza sana jamaniiii dah!!! mdee mama ni wewe kweli?!! dah!! aisee!! anyway...poa poa mdee...fresh yan.
Unamuapisha mbunge kwenye garage ya bunge kama gari bovu,[emoji16][emoji16]nimeamini ccm mwenye akili timamu alikua julius nyerere tuKwanini kiongozi
Pia sura iyo utafikiri 'dikhed'Sura utafikiria kapatwa na tatizo la kupumua,huyu elimu yke haina tofauti na DK manyaunyauView attachment 1636348
Huna unachokielewa kakojoe mkalaleHapo ndio utajua hata kamati kuu wamekurupuka, nenda kasome katiba ya CHADEMA, utaratibu wa kumvua mtu uanachama
Inaumaa eeh mkuuHata useme nini kwisha kazi yenu. Mtajuana huko huko ufipa.
chini ya uangalizi wa Mambosasa , aliyesimamia kura za mabegi KaweSasa kazi ipo duh! Mdee atazungumza kwa niaba ya UWT au CCM?😂😂😂😂
Sawa, maoni yako yaheshimiwe. Mimi ya kwangu ni kwamba hizo hatua zote zinaonesha kwamba kweli CHADEMA kuna demokrasia na walijitahidi sana kutaka hao Dada na mama zetu watendewe haki.Baada ya kusikiliza kile kilichoitwa maamuzi ya kikao cha kamati kuu haya ndiyo nimejionea.
1.Wamevuliwa uanachama wa Chadema kwa sababu hawajatokea kuhojiwa na kamati kuu na siyo sababu ya ubunge wa viti maalum.!
2. Wameambiwa wanaweza kuandika barua ya kuomba radhi ili warejeshewe uanachama wao.!
3. Ndani ya siku 30 wanaweza kukata rufaa kwa kupinga hukumu ya kamati kuu kwenye baraza kuu la chadema.!
4. Chadema iliwaandikia barua mara mbili kuwabembeleza wafike kuhojiwa na kamati kuu pia kamati kuu ililazimika kubadili eneo la kuwahoji kutoka makao makuu ya chadema hadi kwenye hoteli ya kitalii ili kulinda usalama wao.!
Mtu ambaye ni msaliti unaweza kumbembeleza kwa kumwandikia barua mbili na hadi kuingia gharama za kukodi hoteli ili kumuhoji?
Ni vipi msaliti aruhusiwe kuandika barua ya kuomba radhi tu na atarudishiwa uanachama wake?
Kifupi upinzani hakuna wapo kuchumia matumbo sio kutetea wananchi!
sasa atarudishaje mil 600 alizowekewa benki ?Nasrat; ulikuwa ndani miezi kadhaa; umetolewa usiku kwa ulinzi mkali... hukujua.lolote zaidi ya kukutana na deal mezani..
Nadhani hukupata hata nafasi ya kutafakari zaidi ya kuambiwa kesho ni kuapa kwamba unakuwa mbunge. Hata mimi ninge panic.. toka gelezani hadi kuwa mbunge looh
Nimekuombea msamaha kwa kamati Kùu kwamba achana na huo ubunge wa kupewa think about ur future ..think about ur political status...
Jiongeze!! To me ur stil innocent and u still have political future with opposition.
naanza kuona kwa nini shangazi Fatma alifungua kesi dhidi ya jiwe kwa kumchagua mwanasheia mkuu ambaye hatoshi,hatoi ushauri wa haki kila siku mambo yanaenda kinyume na katiba na sheriaUmeandika nini?
Subiri waandike barua ya kuomba radhi na warejeshewe uanachama wao alafu wewe uendelee kupiga miayo hapo ufipa.Nyumbu wa Lumumba, Pole pole anakuchora tu jinsi unavyojipaka mavi!!
Tatizo lako huelewi hata hatua ambazo inatikiwa uzikamilishe mtu kumvua uanachama.View attachment 1636344
Taarifa rasmi ya chama hiyo
Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe atazungumza na Umma wa Watanzania kupitia mkutano na waandishi wa habari, leo Novemba 27, 2020, kuanzia saa 3.00 (usiku huu), kuhusu maamuzi ya Kikao cha Kamati Kuu ya Chama
Vyombo vya habari vya Kitaifa na Kimataifa vimealikwa.
Stay Tuned for Updates
======================
Waandishi wanaanza kuwasili ukumbini wanaoingia wanatakiwa kuwa vitambulisho.
Muda wowote kuanzia Viongozi wa Chadema wataingia ukumbini kuongea na waandishi wa habari.
22:08
Bado Viongozi wa Chadema hawajafika ukumbini
Mkutano huo utakuwa live kupitia
Tayari Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Freeman Mbowe ameshafika ukumbini
Tunawashukuru Watanzania wengi ambao wanafuatilia kikao maalum cha ajenda moja ya kujadili, kushauriana na kutafakari juu ya wanachama wetu 19 waliokwenda kuapa kuwa wabunge wa viti maalum- Freeman Mbowe
"Sisi kama kamati kuu ya chama kikuu cha upinzani, tumeona na kuridhishwa kuna ukiukwaji mkubwa umekiukwa katika mchakato mzima wa uchaguzi na huu wa viti maalum. Tumejiridhisha ndani ya chama kuhusu mapungufu kadhaa yaliyofanyika-; Mbowe
“Chama chetu hakijateuwa Wabunge wa Viti Maalum lakini tunaona wapo Bungeni wanaapishwa”Mbowe
Tangu nchi hii ipate uhuru hatujawai kuona Mbunge/Wabunge wakiapishwa garage, mambo ya kihuni kabisa haya..." Mbowe
“Hiki chama kinaongozwa na principles bila kujali maumivu makubwa tuliyopitia chama chetu kitafuata utaratibu siku zote, kwahiyo kamati kuu imewavua nafasi zao za uongozi viongozi wote waliokua na nafasi katika mabaraza ya chama.”
@freemanmbowetz
“Kamati Kuu imewavua Uongozi wale wote ambao walikuwa Viongozi kwenye Mabaraza kati ya hao Dada zetu 19 sitaki kupoteza muda kuwataja majina, kwahiyo kuanzia sasa hawapaswi kushughulika na lolote kama Viongozi na tumeelekeza nafasi zao zizibwe haraka” -MBOWE
"Ili kanuni ambayo Spika ametumia iweze kufanya kazi kuapisha wabunge wetu. Kwanza wangestahili kubadilisha Katiba iruhusu wabunge kuapishwa nje ya utaratibu ambao ni ndani ya Bunge" -
Nusrate Hanje Katibu wa Bavicha amefungwa jela siku 133 kwa makosa yenye dhamana, hawa Watesi wetu wanakwenda kumtoa saa moja usiku akaape.”
”Chama chetu hakijateua Wabunge wa Viti Maalum tunaona tu Watu wetu wanaapishwa na hatuna taarifa, hatujapeleka majina, fomu za Tume zipo ofisini Mama zetu hawa Dada zetu hawajajaza fomu, ila tunaona tu wanaaapishwa”-
"Sisi kama chama cha siasa, hii 'process' yote hatuijui, tunaona tu wabunge wetu wanaapishwa. Chama chetu hakijateua wabunge wa viti maalum" -
"Wabunge hawa 19, mama zangu na dada zangu wameapishwa kiapo batili kwani Katiba inasema waapishwe mbele ya Bunge. Sasa kanuni zimebadilishwa ili kumruhusu Spika kumwapisha popote hata eneo la gereji-
“Tangu Nchi yetu imeanza hatujawahi kuona Wabunge wanaapishwa Gereji, lakini Dada zetu na Mama zetu hawa wameapishwa nje ya Bunge, wakati Katiba inataka waapishwe ndani ya Bunge, kwahiyo wamekula kiapo batili”
Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe amesema Kamati Kuu ya Chama hicho iliyoketi leo Nov 27,2020 imeazimia kuwavua uanachama Halima Mdee na wenzake 18 waliopishwa juzi kuwa Wabunge Viti Maalum “wamekinajisi Chama na wamekataa kuja kwenye Kamati Kuu”
”Chama chetu hakijateua Wabunge wa Viti Maalum tunaona tu Watu wetu wanaapishwa na hatuna taarifa, hatujapeleka majina, fomu za Tume zipo ofisini Mama zetu hawa Dada zetu hawajajaza fomu, ila tunaona tu wanaapishwa”
“Kamati Kuu imewavua Uongozi wale wote ambao walikuwa Viongozi kwenye Mabaraza kati ya hao Dada zetu 19 sitaki kupoteza muda kuwataja majina, kwahiyo kuanzia sasa hawapaswi kushughulika na lolote kama Viongozi na tumeelekeza nafasi zao zizibwe haraka”
"Kamati Kuu imeazimia kuwavua uanachama wake wote 19 wakiongozwa na Halima Mdee , walioapa kule Dodoma.-Mbowe
Sawa waliapishwa Bungeni, ila wameshavuliwa uanachama.Mkuu mleta mada
1. Nusrat hakuapishwa saa moja usiku kama ulivyomnukuu Mbowe kila mmoja aliona tukio hilo ilukwa ni mchana kweupe;
2. Mh Freeman Mbowe kudai taratibu na kanuni za kudumu za bunge zimekiukwa na kwamba mbunge anaapishwa ndani ya bunge pekee wakati akijua anasema uongo wa wazi kabisa maana yeye pamoja na wabunge wengine walishiriki kubadilisha kanuni Agosti 2020 (Rejea TANGAZO LA SERIKALI NA. 626 la tarehe 7/8/2020) na mabadiliko ni haya:
(2) Bila ya kujali masharti ya fasili ya
(1), endapo Mbunge atachaguliwa au kuteuliwa baada ya Uchaguzi Mkuu, Spika atamwapisha katika: (a) kikao chochote cha Bunge iwapo kuna Mkutano wa Bunge; au (b) eneo litakalopangwa na Spika iwapo hakuna Mkutano wa Bunge unaoendelea na baadaye Spika atatoa taarifa Bungeni kwenye Kikao cha Kwanza cha Mkutano wa Bunge unaofuata.
(3) Wakati wa kuapa, Mbunge anayeamini kuwa kuna Mungu, atalazimika kushika Biblia au Kuran au kitabu kingine kitakatifu kinachotambuliwa na imani ya dini yake.
(4) Iwapo Mbunge haamini kuwa kuna Mungu, hatashika Biblia au Kuran au kitabu chochote kitakatifu au kutamka maneno, “Ewe Mwenyezi Mungu nisaidie,” bali atalazimika kuinua mkono wake wa kuume juu.
(5) Kiapo cha uaminifu cha Mbunge kitakuwa na maneno yafuatayo: “Mimi, ………..., naapa kwamba, nitakuwa mwaminifu kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuitumikia kwa moyo wangu wote na kwamba nitaihifadhi, nitailinda na kuitetea Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mujibu wa Sheria iliyowekwa. Ewe Mwenyezi Mungu, nisaidie.”