Kamati Kuu ya CHADEMA yawavua nyadhifa na uanachama Halima Mdee na wenzake 18 walioapishwa kuwa Wabunge wa Viti Maalum

Kamati Kuu ya CHADEMA yawavua nyadhifa na uanachama Halima Mdee na wenzake 18 walioapishwa kuwa Wabunge wa Viti Maalum

Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe atazungumza na Umma wa Watanzania kupitia mkutano na waandishi wa habari, leo Novemba 27, 2020, kuanzia saa 3.00 (usiku huu), kuhusu maamuzi ya Kikao cha Kamati Kuu ya Chama

Vyombo vya habari vya Kitaifa na Kimataifa vimealikwa.

Stay Tuned for Updates

======================
Waandishi wanaanza kuwasili ukumbini wanaoingia wanatakiwa kuwa vitambulisho.
Muda wowote kuanzia Viongozi wa Chadema wataingia ukumbini kuongea na waandishi wa habari.
22:08
Bado Viongozi wa Chadema hawajafika ukumbini
Mkutano huo utakuwa live kupitia
Tayari Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Freeman Mbowe ameshafika ukumbini
Tunawashukuru Watanzania wengi ambao wanafuatilia kikao maalum cha ajenda moja ya kujadili, kushauriana na kutafakari juu ya wanachama wetu 19 waliokwenda kuapa kuwa wabunge wa viti maalum- Freeman Mbowe
"Sisi kama kamati kuu ya chama kikuu cha upinzani, tumeona na kuridhishwa kuna ukiukwaji mkubwa umekiukwa katika mchakato mzima wa uchaguzi na huu wa viti maalum. Tumejiridhisha ndani ya chama kuhusu mapungufu kadhaa yaliyofanyika-; Mbowe
“Chama chetu hakijateuwa Wabunge wa Viti Maalum lakini tunaona wapo Bungeni wanaapishwa”Mbowe
Tangu nchi hii ipate uhuru hatujawai kuona Mbunge/Wabunge wakiapishwa garage, mambo ya kihuni kabisa haya..." Mbowe
“Hiki chama kinaongozwa na principles bila kujali maumivu makubwa tuliyopitia chama chetu kitafuata utaratibu siku zote, kwahiyo kamati kuu imewavua nafasi zao za uongozi viongozi wote waliokua na nafasi katika mabaraza ya chama.”
@freemanmbowetz

“Kamati Kuu imewavua Uongozi wale wote ambao walikuwa Viongozi kwenye Mabaraza kati ya hao Dada zetu 19 sitaki kupoteza muda kuwataja majina, kwahiyo kuanzia sasa hawapaswi kushughulika na lolote kama Viongozi na tumeelekeza nafasi zao zizibwe haraka” -MBOWE

"Ili kanuni ambayo Spika ametumia iweze kufanya kazi kuapisha wabunge wetu. Kwanza wangestahili kubadilisha Katiba iruhusu wabunge kuapishwa nje ya utaratibu ambao ni ndani ya Bunge" -

Nusrate Hanje Katibu wa Bavicha amefungwa jela siku 133 kwa makosa yenye dhamana, hawa Watesi wetu wanakwenda kumtoa saa moja usiku akaape.”

”Chama chetu hakijateua Wabunge wa Viti Maalum tunaona tu Watu wetu wanaapishwa na hatuna taarifa, hatujapeleka majina, fomu za Tume zipo ofisini Mama zetu hawa Dada zetu hawajajaza fomu, ila tunaona tu wanaaapishwa”-

"Sisi kama chama cha siasa, hii 'process' yote hatuijui, tunaona tu wabunge wetu wanaapishwa. Chama chetu hakijateua wabunge wa viti maalum" -

"Wabunge hawa 19, mama zangu na dada zangu wameapishwa kiapo batili kwani Katiba inasema waapishwe mbele ya Bunge. Sasa kanuni zimebadilishwa ili kumruhusu Spika kumwapisha popote hata eneo la gereji-

“Tangu Nchi yetu imeanza hatujawahi kuona Wabunge wanaapishwa Gereji, lakini Dada zetu na Mama zetu hawa wameapishwa nje ya Bunge, wakati Katiba inataka waapishwe ndani ya Bunge, kwahiyo wamekula kiapo batili”
Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe amesema Kamati Kuu ya Chama hicho iliyoketi leo Nov 27,2020 imeazimia kuwavua uanachama Halima Mdee na wenzake 18 waliopishwa juzi kuwa Wabunge Viti Maalum “wamekinajisi Chama na wamekataa kuja kwenye Kamati Kuu”

”Chama chetu hakijateua Wabunge wa Viti Maalum tunaona tu Watu wetu wanaapishwa na hatuna taarifa, hatujapeleka majina, fomu za Tume zipo ofisini Mama zetu hawa Dada zetu hawajajaza fomu, ila tunaona tu wanaapishwa”

“Kamati Kuu imewavua Uongozi wale wote ambao walikuwa Viongozi kwenye Mabaraza kati ya hao Dada zetu 19 sitaki kupoteza muda kuwataja majina, kwahiyo kuanzia sasa hawapaswi kushughulika na lolote kama Viongozi na tumeelekeza nafasi zao zizibwe haraka”
"Kamati Kuu imeazimia kuwavua uanachama wake wote 19 wakiongozwa na Halima Mdee , walioapa kule Dodoma.-Mbowe

Hii ndo chadema,thanks kamati kuu
 
Vyama vya upinzani nchini vinaboreshwa na ubovu wa serikali.Huu ndo msingi mkuu wa ukuaji wa vyama vya upinzani.Kama serikali ikiamua kusimama barabara katika HAKI nakuhakikishia vyama vya upinzani vitabaki majina tu.

Hapana na hapa ndio tatizo linapoanzia mtaji si madhaifu ya mwengine bali ni jinsi gani ulivyo mzuri zaidi yake .
Ubovu wa Serikali hutoa nafasi ya kukua kwa upinzani wenye mipango.
 
Hapana na hapa ndio tatizo linapoanzia mtaji si madhaifu ya mwengine bali ni jinsi gani ulivyo mzuri zaidi yake .
Ubovu wa Serikali hutoa nafasi ya kukua kwa upinzani wenye mipango.
Kiujumla Upo sahihi ila Mimi nazungumzia kwa hapa nchini kwetu.
 
Unataka wasaliti wapewe masaa mangapi mkuu?.Binafsi hata kuwaita tu naona bado ni uungwana sana.

Hivi unajua Yesu alimjua Yuda kuwa ni msaliti hata wakati anamchagua! Logically tu unadhani uchambuzi wa facts na matukio umefanyika kwa maslahi mapana ya CDM .
Lengo la adhabu ni nini?Kitu gani kilipelekea mpaka BAWACHA au uongozi wake kufanya maamuzi haya?
 
Hamna kitu hapo
Sukule is always a sukule.
2020_11_25_15.00.17.jpg
 
Hivi unajua Yesu alimjua Yuda kuwa ni msaliti hata wakati anamchagua! Logically tu unadhani uchambuzi wa facts na matukio umefanyika kwa maslahi mapana ya CDM .
Lengo la adhabu ni nini?Kitu gani kilipelekea mpaka BAWACHA au uongozi wake kufanya maamuzi haya?
Ni usaliti tu hakuna kingine.Kuendekeza tumbo kubaya sana.
 
Kiujumla Upo sahihi ila Mimi nazungumzia kwa hapa nchini kwetu.

Sasa kwa mtindo huu wamekuwa wakiendelea kupata matokeo yale yale na kujeruhiwa kwenye kila uchaguzi.
CDM ni lazima iwekeze katika watu na kujifunza kuishi nao kwani mtaji mkubwa wa chama chochote cha siasa ni watu .
Leo hii hata mawakala wa kueleweka kwenye baadhi ya majimbo walikuwa hawana!
 
Kuna ids waliokuwa CDM lia lia hapa JF sijaona zikichangia thread,mfano Sky Eclat Erythrocyte (samahani sijapitia pages zote). Taja id nyingine kama umeigundua
 
Kama presha haiwapandi mbona mnahonga hao hao wapinzani na kufanya hujuma kila Kona , mmehujumu shughuli zabkisiasa Kwa miaka mitano mfululizo Kwa upinzani mkashindwa mkaona haitoshi , mmebambikizia watu kesi , mmeteka na kuua watu , mmehujumu na kunajisi uchaguzi WA serikali za kitaa, mmehonga wanasiasa Kwa kuwarubuni kwa pesa ( biashara ya utumwa ) , mmefunga watu , mmenajis uchaguzi mkuu mkaona bado haitoshi na bado mmeshindwa , chupi zimewatepeta bado mnanunua wapinzani na kutaka kuhujumu Chama cha Chadema .

Mpuuzi wewe
Politics is a game of intelligency.
Na watu wenye akili kwenye siasa wanatamani sana kuwapata wapinzani wa kariba yako kwenye siasa. Mbowe ana akili na uwezo mkubwa sana kwenye siasa kuliko hata Lissu.
Siasa ukiifanya kwa misingi ya lugha hii unayotumia hapa unapoteza kila kitu.
 
Ni usaliti tu hakuna kingine.Kuendekeza tumbo kubaya sana.

Hapana haya ni majumuisho au kwa lugha nyingine CDM watakuwa wamefanyia kazi matokeo na si mzizi wa tatizo.
Niliwahi kuuliza humu jamvini kwa kusema dhana ya kuwa viongozi wa CDM wananunuliwa haitoshi kuwaaminisha wananchi kuwa wakiwachagua tena hawata nunuliwa.
CDM ilitakiwa ije na majibu zaidi.Funny enough hata mwezi haujaisha sababu ile ile inatumika ina maana kila kiongozi CDM ana price tag?
 
Unajenga hoja vizuri ila kiswahili hujui. Sijaona muunganiko wa hiyo hoja yako "Kama unakubali la CCM kwanini ukubali Chadema kuwa na Mwenyekiti mpya"?

Nadhani ulipaswa kuandika "hukubali" na si "ukubali". Na usijaribu kusema ni typing error, hicho kichaka mmejificha sana tunakijua. Sana sana ishia kimya kimya, shule za kata tunazijua zilichofanya.
Mkuu,kila siku mimi husema hadharani kuwa CCM wamefanikiwa jambo moja tu huko Tanzania,nalo ni kuwafanya Watanzania wengi kuwa wajinga,wapumbavu na misukule kwa kuwapa elimu ya kipumbavu.
 
Mnafikiri nyie mnavyomsujudia Mh mungu na CHADEMA kuna huo upuuzi ?
Angalia mwehu huyu..kwamba hujajuaga tu kua chadema ni kundi dogo la kihuni?watu wengine sijui hata kwa nini mlikua watu na si viumbe vingine tu au mawe
 
Hapana haya ni majumuisho au kwa lugha nyingine CDM watakuwa wamefanyia kazi matokeo na si mzizi wa tatizo.
Niliwahi kuuliza humu jamvini kwa kusema dhana ya kuwa viongozi wa CDM wananunuliwa haitoshi kuwaaminisha wananchi kuwa wakiwachagua tena hawata nunuliwa.
CDM ilitakiwa ije na majibu zaidi.Funny enough hata mwezi haujaisha sababu ile ile inatumika ina maana kila kiongozi CDM ana price tag?
Unadhani dhana ya CCM kuua upinzani wanatekeleza vipi?.
 
Sasa kwa mtindo huu wamekuwa wakiendelea kupata matokeo yale yale na kujeruhiwa kwenye kila uchaguzi.
CDM ni lazima iwekeze katika watu na kujifunza kuishi nao kwani mtaji mkubwa wa chama chochote cha siasa ni watu .
Leo hii hata mawakala wa kueleweka kwenye baadhi ya majimbo walikuwa hawana!
Hata hao mawakala wangekuwepo kwa yaliyofanyika nini kingebadilika?.Ndio maana watu wameona wapande ndege ili kubadili uwanja wa mapambano.
 
Back
Top Bottom