Kamati ya Amani yapiga marufuku Magufuli kuitwa "Mwendazake", Wametumia sheria gani?

Waache upumbavu, kwani Magufuli si bado anaishi mioyoni mwa baadhi ya watanzania? Kwani neno hilo likitumiwa linawadhuru nini wao? Si neno la kiswahili? Hawa ndiyo maana wakati mwingine wanatafsiriwa ni waganga njaa, wamekosa mambo ya msingi ya kujadili wanashikashika vitu very minute, tulitegemea wazungumzie katiba mpya na siyo vineno vidogo kama Mwendazake
 
Ukiisikiliza hii kamati mara nyingine unaweza kupata hasira kiasi ambacho ukatoa maneno ukajikuta umeingia matatizoni kwa kumkufuru mwenyezi Mungu muumba wa mbingu na nchi pamoja na vyote vilivyomo. Hii kamati si ndio ile ile yupo yule shehe aliyemfananisha mwendazake na Yesu akaona haitoshi akamfananisha na Mtume Muhamad SAW bado hakuridhika akamfananisha na Mungu kabisa. Ngoja niishie hapa hapa nibaki nasoma tu maoni maana naona nikiendelea hii kamati itanichonganisha na muumba.
 
Nayo ni majizi tu kama majizi wengine
 
Hii kamati si ndio ile ile yupo yule shehe aliyemfananisha mwendazake na Yesu akaona haitoshi akamfananisha na Mtume Muhamad SAW bado hakuridhika akamfananisha na Mungu kabisa
Ni kweli Mkuu wakati mwingine bora kuwasamehe maana hatujui hata huo uongozi waliupataje
 
😆😆😆
 
Kwanza watueleze na watuthibitshie pasipo shaka kuwa wamejuaje kuwa huyo mheshimiwa waliyemtaja ndio watu wanamwita mwendazake. Pili hawaoni kufanya kwao mkutano na kutangaza kupiga marufuku ndio watakuwa wanatangaza kabisa na kuwajuza hata wale ambao walikuwa hawajui kuwa mwendazake ni nani sasa watamjua.

Mimi nafikiri viongozi wetu wa dini wana wajibu mkubwa sana katika maisha ya mwanadamu ya kila siku. Lakini kujiingiza huku kwenye hayo mambo ya kutoa matamko sijui watu wasimwite fulani mwendazake kunawashushi hadhi waliyo nayo kwenye jamii kwani haya majina/maneno mengine huzuka ghafla kutokana na msimu na mazingira yalipotokea tukio fulani kwa hiyo hata mwisho wa hayo majina/maneno nao huwa ni ghafla tu bila hata matamko.
 
Yeye aliyebaki ndio tutamwita mwendazake maana analitaka hilo jina “ mwendazake askofu konki “
 
Kwa kufanya hivo ni kutuonyesha jinsi wanapingana na kamusi ya TUKI
 
Hatuachi kama wanaona vipi wanywe sumu wamfuate. Viongozi wa dini sampuli hii ni wa kuwasusia kabisa kwenye nyumba za ibada wanakohudumu
 
Akumbushwe Amani haiji kwa marufuku.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…