Kamati ya Bunge yapigwa butwaa na Deni la ATCL kufika bilioni 472. Kuna hatari ya shirika kufa

Kamati ya Bunge yapigwa butwaa na Deni la ATCL kufika bilioni 472. Kuna hatari ya shirika kufa

Pythagoras,
Hawa Wabunge wa CCM wanatufanya Watz hatuna akili!! Wapinzani wakipiga kelele sana Bungeni kuhusu ununuzi wa hii midege ya MABILIONI ambayo HAINA FAIDA YOYOTE KWA ATCL, SERIKALI NA WATZ!!!
Wabunge hawahawa walikuwa wakishangilia na kupiga meza kukubaliana na ujinga huu......Pambaf kabisa!!!
sio wabunge tu hata watanzania nao wengi ni tatizo. Elimu ilitolewa sana juu ya ununuzi wa hizi ndege kuwa haukuwa na nia njema wala tija. Hata hivyo waliendelea kushangilia.
 
Deleted but not because I am scared, some people have to get out of our politics I will say that anytime.

Ila vijana walamba miguu mnatuangusha our politics have to evolve.

👋👋👋 last goodbye
wamelamba miguu sana wakaona haitoshi wamehamia kwenye ugaidi
 
Bado Samia anasema wameagiza ndege nyingine tano. Kwanini Ofisi ya rais watumie ndege ya ATCL wakati wakijua ndege hizo ni za biashara na wakiruka tu juu mamlaka ya anga ya kimataifa inataka walipe? Kwanini wasitumie ndege ya rais?
Najua wengi mtakataa. Lakini naamini hao wakubwa wakizitumia, wanalipia tena in advance
 
Kamati ya Bunge la nchi gani! Kamati za Bunge hutokana na wabunge na ni wabunge haohao wanaosifu kwa asilimia mia wakati wa bajeti, leo kutuambia wameshituka ni kutufanya sisi mataahira.
Umenena vema ndg. Walituona mazwazwa sana wakati tunapinga manunuzi ya ngede bila kuwa na credible business plan. Mzee kashikilia bango
 
Kamati ya bunge yang'aka na kushangaa deni la shirika la ndege la ATCL kufika shilingi bilioni 472 na kuna hatari ya kufirisika na kufa kama seikali haitaingilia kati.

HT gazeti Mwananchi
ATCL hii au ni tofauti na ile ya JIWE aliyokuwa anasema inapata faida?
Tena kwa kuiua fast jet na precision air ili atawale soko mwenyewe?
 
Sawa tuseme Jiwe alikuwa mbaya Sasa hawa malaika watuonyeshe uwezo wao kubadilika shirika.
Kwenye tozo, safari za nde kila kukicha wameweza.
Zote hizi ni matokeo ya utawala mbovu wa Magufuli. Awamu hii haihusiki.
 
Akili zitarudi tu. Hivi kuna shirika kama hilo hapa nchini? Kwa kuanzia halina ndege zake lenyewe kwani karibia zote ni za kukodi. Hivyo basi wanapaswa kwanza kuwalipa hao waliowakodisha hizo ndege, watoe na fedha za uendedhaji wa hizo shughuli zao ndiposa wabaki na faida! Mkodishaji anafaidika zaidi. Enzi zetu tukiuita uhusiano huu kuwa wa kinyonyaji. Unakaa tu nyumbani, Una majumba 10 mjini uliyoyapangisha na unavuta pesa kiulaini!
Ndege za kukodi tena? Fafanua mkuu
 
Serikali ikitumia ndege za ATCL gharama zinakuaje za ATCL? Kama ndege ya Rais ni mbovu sio kesi.
 
Tuliaminishwa kuwa hili shirika linaingiza faida mpaka wakaanda tukio live kabisa la kutoa gawio kwa serikali
Hili shirika limeanza kula hasara toka lianze kuruka enzi za Mwendazake na deni linazidi kukua,hili deni hasa linasababishwa na nini? Wanakodi nini?
 
Me sishangai kabisaaah!

Prof.Assad aliwashauri waue shirika, walipe madeni, then waanze upya, aliambulia matusi kutoka UVCCM!

#ukipanda magugu tegemea kuvuna magugu!
Kumbe walieithi madeni ya awali? Sasa wanavyochelewa deni linakua plus hasara wanazopata kwa vile hawapati faida yoyote.
 
This is TZ, ukweli humweka mtu huru. Ukweli ni biashara ya Ndege ni ngumu na kubreak-even ni ngumu kidogo. Ila uongo sio mzuri hasa kwenye vitu nyeti kama hivi. Na anedanganywa ni mwenye mali hatari sana.
 
Swali nimeshauliza sana; ndege ya rais wetu ni Gulfstream iliyonunuliwa kwa mbwebewe kuwa hata kama watanzania tutakula nyasi lazima rais awe na gu;fstream. Cha ajabu siku hisi rais hasafiri kwa gulfstream tena ingawa ina masafa marefu kuliko hiyo airbus, bado rais wetu anapenda airbus tu ambyo ni ndege ya abiria kibiashara. Gulfstream ilimpeleka mama Kikwete Brazil non-stop kutoka Dar hadi Rio; hii airbus haiwezi kufanya trip ya aina hiyo, lakini mama kaing'anagania kweli kweli!
Kitakuwa kibovu
 
Bado Samia anasema wameagiza ndege nyingine tano. Kwanini Ofisi ya rais watumie ndege ya ATCL wakati wakijua ndege hizo ni za biashara na wakiruka tu juu mamlaka ya anga ya kimataifa inataka walipe? Kwanini wasitumie ndege ya rais?
Ndege zote ni za serikali. ATCL ni wakodishaji. ATCL wanailipa serikali wanapozitumia. Muwage mnaelewa basi.
 
This is TZ, ukweli humweka mtu huru. Ukweli ni biashara ya Ndege ni ngumu na kubreak-even ni ngumu kidogo. Ila uongo sio mzuri hasa kwenye vitu nyeti kama hivi. Na anedanganywa ni mwenye mali hatari sana.
Naomba kuuliza hivi kila nchi hapa Duniani ina shirika lake la ndege?
 
Kwanini ATCL isipate hasara wakati zinatumika na Top three kama boda boda! Utasikia Rais yupo Rwanda na lile dege kubwa Dreamliner, Makamu yupo Burundi na Airbus, huku PM yupo kwao kusalimia kwa Bombardier. Nchi imepoteza dira kabisa.
Duh...
 
Back
Top Bottom