Kamati ya Bunge yapigwa butwaa na Deni la ATCL kufika bilioni 472. Kuna hatari ya shirika kufa

Kamati ya Bunge yapigwa butwaa na Deni la ATCL kufika bilioni 472. Kuna hatari ya shirika kufa

AAIewx.jpg
 
Biashara ya usafiri wa anga, ni vigumu kupata faida ndani ya muda mfupi au muda wa kati (Short term or midium term plan),labda faida itapatikana kwenye milango ya muda mrefu (long-term plan).
-Mashitika mengi ya ndege yanaendeshwa kwa hasara na waumini wa kuwekeza kwenye biashara ya ndege,wanategemea multiplier effect kwenye sector zingine (kama utalii na mahoteli nk).Sina uhakika kama Manejimenti na Bodi yà ATCL wanaimbia ukweli serikali.
-Serikali kununua wa ndege nyingi kwa fedha taslimu ni miongoni mwa maamuzi mabovu sana kuwahi kutokea kwa Serikali yetu,uwekezaji huu,hautawanufaisha wananchi wa kawaida(common people) na wapiga kura wao,Bali unawanufaisha watu wachache sana (wanaotumia ndege).
-Ni ukweli usiopingika kuwa serikali itaendelea kutoa ruzuku ya uendeshaji wa shirika kila mwezi miaka mingi ijayo.
-Menejimenti inaendesha shirika kisiasa badala ya kufuata weledi.
-Mtaji/Ruzuku inatolewa ATCL kupitia wakala wa ndege za serikali zingewekezwa kwenye miradi ya maendeleo inayogusa wananchi wengi (wakulima).
-Serikali ingenunua matreka (ya kukodisha) kwa kila Kijiji na kujenga viwanda vya mbolea na viwatilifu kila Kanda,ili kuongeza uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara badala ya kuwekeza kwenye ndege nyingi bila kufanya upembuzi yakinifu.
 
Zote hizi ni matokeo ya utawala mbovu wa Magufuli. Awamu hii haihusiki.
Awamu hii? Wamejipambanua vipi na Magufuli? Sioni tofauti ya fikra na nyendo zao.

Nilitarajia katika hatua za awali kabisa waweke kamati ya wataalamu wenye credibility waandae mpango wa kuendesha ATCL au hata namna kutumia hizo ndege kwa ufanisi kwa muda mfupi na mrefu hapo baadaye. Badala yake wanaonekana wakizitumia tu kama ndege za serikali na mambo yakiendelea kama kawaida yao.
 
Hata sishangai, management bado ileile, wanasiasa walewale, tabia zao zilezile, chama kilichoshindwa kilekile, kupata hasara iko kwenye DNA yao.

And some people expect to see different results!
 
Kama kila siku mtu mmoja anazulula na dreamliner ,hatulii nyumbani ,unazani Deni litakuwaje,ovious huge loss lzm izalishwe!! Sasa akianza kuzulula ughaibuni na m dreamliner ndo kabisaaa!ninachokiona Kuna kitu kinatengenezwa,nahisi ni mikakati ya kuja na agenda ya ATCL ibinafsishwe,kwa kuwa inaingiza hasara!!
 
Ndege tayari zishanunuliwa ni wajibu wa serikali sasa kuja na strategic sahihi za namna ya kuendesha biashara hiyo,kulia Lia haisaidii chochote.Hasara inayotangazwa leo si ni pamoja na ile hela iliyoporwa Morocco kwenye ofsi za ATCL
 
Yule mzee alituona mazwazwa sana...

Kamati inasemaje kuhusu ule uwanja wa kimataifa wa Chato? Njiwa zinatua pale au tufanye uwanja wa ng'ombe kuotea jua wapate vitamin D kwa wingi?
[emoji1787][emoji23][emoji1787] Welcome Tanzania.
 
Swali nimeshauliza sana; ndege ya rais wetu ni Gulfstream iliyonunuliwa kwa mbwembwe kuwa hata kama watanzania tutakula nyasi lazima rais awe na gulfstream. Cha ajabu siku hizi rais hasafiri kwa gulfstream tena ingawa ina masafa marefu kuliko hiyo airbus, bado rais wetu anapenda airbus tu ambyo ni ndege ya abiria kibiashara. Gulfstream ilimpeleka mama Kikwete Brazil non-stop kutoka Dar hadi Rio; hii airbus haiwezi kufanya trip ya aina hiyo, lakini mama kaing'anagania kweli kweli!
Unajua raha ya kupanda ndege mpya tena yenye nafwasi. Hiyo GS viti vimeshakaliwa na kina prof “mia kenda” na mabox ya juisi.
 
Mali za urithi haziumagi. Tunatapanya tu. Tozo zitaongezeka

R.I.P JPM
 
Mwendazake alifufua shirika hili kishabiki sana kuonyesha kwamba yeye anaweza kununua midege mikubwa kwa cash huku watanguzi wake wote walishindwa - mbaya zaidi alifanya haya bila upembuzi yakinifu. haya sasa kazi hiyo.
Mimi : Bwana mwenye duka" nataka ile basikeli ya laki tano,,
Mwenye duka: ,,Hii hapa mzee"
 
Mimi : Bwana mwenye duka" nataka ile basikeli ya laki tano,,
Mwenye duka: ,,Hii hapa mzee"
Huu ndio ukweli wenyewe 😂😕.

Halafu wanajua Watanzania hawana kero na gharama za serikali wala hawaoni zinavyohusiana na “tozo”! Au zinavyoathiri maendeleo yao.
 
Kamati ya bunge yang'aka na kushangaa deni la shirika la ndege la ATCL kufika shilingi bilioni 472 na kuna hatari ya kufirisika na kufa kama seikali haitaingilia kati.

HT gazeti Mwananchi
Acha tu lijifie kwa sababu wenye mamlaka hapa kwetu hawataki kufikirisha akili zao.
Nchi bado haijajikomboa katika suala la huduma za msingi za jamii kama elimu, maji na afya anaenda kununua ndege cash.
Unanunua ndege cash huku deni la taifa likipaa kwa spidi ya 5G.
 
Mimi nilimshangaa sana mwendakuzimu alipokua anasema analipa kesh kununua ndege na kujenga SGR. Wakati kuendesha kamradi kadogo tu ka UDART kamewashinda.
Madereva wa daladala na mokondakta wao walevi wa Gongo wanawezaje kupata faida na mijifoleni yote hii halafu watu wenye degree wanashindwaje kuendesha UDART?
KILE KITUO KUJENGWA PALE JANGWANI NI KIPIMO TOSHA CHA AKILI YA CCM.
SGR hapo Moro tu pamewashinda wanaanza Isaka Mza. Hawajui kwamba siku hizi kila msukuma ana IST.
 
Hili shirika litakufa tu hata waliache ICU kwa muda gani na haitakuwa mara yake ya kwanza kufanya hivyo.

Kwa zama hizi serikali hizi kuendesha shirika la ndege na lipate faida ni kitu hakiwezekani, kama zamani tu wakati ushindani ulikuwa ni mdogo na ndio zilishindwa sasa leo chini ya ushindani mkali hivi ndio wataweza. Never.

Mashirika ya ndege kama ya Quatar, Etihad, Emirates, Kuwait yanapata mafuta kwa bei ndogo sasa utawezaje kushindana nazo na kwa huu ufisadi tuliozoea.
 
Yule mzee alituona mazwazwa sana...

Kamati inasemaje kuhusu ule uwanja wa kimataifa wa Chato? Njiwa zinatua pale au tufanye uwanja wa ng'ombe kuotea jua wapate vitamin D kwa wingi?
Mbona wakati yule mzee yupo hai hawakung'aka hivi?!
 
Back
Top Bottom