#COVID19 Kamati ya Corona: Serikali itoe taarifa uwepo wa Ugonjwa wa COVID-19 na kuruhusu matumizi huru ya chanjo

MTU anaona mwenyewe nchi yake haina SHIDA ya Corona.
Watu hawavai barakoa wala kutumia sanitizer.
Na bado watu wanadunda wapo salama.
ILA anaona haitoshi
Hii nchi ilishatabiriwa Sana kuhusu Corona ILA tulivuka.
ilishajengwa propaganda kuwa kila dereva wa Tanzania akienda nchi jirani ana Corona.
Na bado tukavuka.
HOFU inaanza kutengenezwa kwa makusudi.

Lengo ni chanjo na lockdown.
 
Then ikumuua, yeye na katibu mkuu wake kiongozi, angeacha ujinga na ubishi kuhusu corona angekuwa hai hadi leo
 
Rais Samia Suluhu Hassan akipokea Ripoti ya Kamati Maalum aliyoiunda kwa ajili ya kufanya tathmini ya Ugonjwa wa Corona -COVID -19 nchini kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo Profesa Said Aboud Ikulu Jijini Dar es Salaam leo.



Hii corona ipo Ikulu tu maana tunaona mmevaa barakoa tu ila huku wananchi tulisha sahau kabisa.
 
ukiona nyungu itakusaidia kwenye UKIMWI.
unaruhusiwa kutumia.
ILA mbinu za magufuli zilizaa matunda Sana.
UKWELI USEMWE.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]Jesus..

Kwanini hatujaja na mbadala wa HIV,TB na Malaria tofauti na recommandation za WHO kama tuvilyopiga uturn na nyungu uchwara hizo kwenye corona?
 
Watu wakianza kutishwa hata maisha yatabadilika.

Kwa kweli tunaangamia. Tunatishwa kwa kitu kisichokuwepo.

Makuwadi wa mabeberu watatumaliza kwa hofu.
 
Poleni sana Watanzania, tume na mavitabu ndio kichaka cha kuhalalisha uchanjwaji wa chanjo ya korona.

Mliambiwa mtamkumbuka na bado wingu zito laja
 
Kwa nini kila aliye kinyume na hoja zenu mnamhusisha na JPM?
Siyo kila aliye kinyume namhusisha na JMP, atleast nikizungumzia mimi mwenyewe(wewe ume-address na watu wengine unaowajua). Kilichonifanya niseme hivyo ni kwa sababu Magufuli ndiye alianzisha huu ujinga wa kusema kuwa kutangaza Tanzania kuna corona ni kutia watu hofu wakati tangu tupate uhuru kumekuwepo na milipuko ya magonjwa mbalimbali na tumekuwa tunatangaziwa. Hili suala la kusema kutangaza kuna ugonjwa ni kutia watu hofu ni ujinga wa hali ya juu sana. Watu watajikingaje bila kujua kuna ugonjwa?
 
mnatafuta kichaka cha kujifichia.
Hapana mkuu..unajua shida hapa ni mahaba na tunavyojaribu kuchambua tu mambo..jpm alianza vizuri uraisi wake,,baada ya muda akapiga u-turn ya ajabu na ameacha mambo hovyo..NSSF na PSSSF ni mfano na Samia ameadmit hili waziwazi
 
Pigo jingine kwa sukuma gang!
 
Hapo sasa ndio naona hatuna Rais tuna picha ya Rais tu,eti Tanzania tuna corona wakati jana tu Makamu wa Rais alikuwa kwenye kampeni uko Kigoma na CCM wameishinda majimbo yote mawili na watu walikuwa wakikusanyika nyomi kama kwaida,leo mbio za mwenge zimeanza, mitaani ndio usiseme,leo eti Tanzania tuna corona; ngoja tuone huyu mama anapotupeleka.
 
Uko sahihi. Tunakosa hata umakini wa kuangalia kwa macho kilichoandikwa, sembuse kusoma na kuelewa? Tunapaswa kujadili kilichowasilishwa, na si tunachohisi au kufikiri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…