Uchaguzi 2020 Kamati ya Maadili NEC yamfungia Halima Mdee kuendesha kampeni kwa siku 7

Uchaguzi 2020 Kamati ya Maadili NEC yamfungia Halima Mdee kuendesha kampeni kwa siku 7

Quinine

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2010
Posts
22,227
Reaction score
49,628
Nimepata Taarifa NIMEFUNGIWA kufanya KAMPENI siku saba kuanzia tarehe 12-18/10/2020. Hukumu ilikuwa imesha andikwa kabla ya KIKAO cha Maadili. TUTAWEKA WAZI USHAHIDI tulio uwasilisha. NJIA moja ikifungwa....tunafungua nyingine.- H Mdee.



-----

Kamati ya Maadili NEC imemfungia kuendesha shughuli za kampeni Mgombea Ubunge wa jimbo la Kawe kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Halima Mdee.

Kwa mujibu wa taarifa aliyotoa kupitia ukurasa wake wa Twitter, adhabu hiyo inaanza kutekelezwa kuanzia tarehe 12 hadi 18 ya mwezi huu wa Oktoba, 2020.

photo_2020-10-12_00-00-45.jpg
 
Hii haita msaidia kushinda KAWE ya Gwajima bibi wewe kitulize tu huu sio muda wako tena ufungiwe usifungiwe haikusaidii

Sent from my SM-J110H using JamiiForums mobile app
 
Kama amekutwa na hatia ataadhibiwa tu, kujiwahisha kusema hakutishi athourity kumpa adhabu ova!
 
Hii nchi raha sana. CCM wanatukana mpaka wanaita watu malaya. Wagombea wao wanatishia wananchi kuwa hawataleta maendeleo. Mgombea wao anachanganya siasa na serikali. Wapinzani wakipeleka malalamiko hata hoja hazisikilizwi ila Wa Upinzani hasa CHADEMA akituhumiwa tu kikao kinakaa hata saa sita usiku. Ila tutafika tu. "One day Yes"
 
Hukumu inatolewa vipi kabla ya kikao? Au mtu anaitoa mwenyewe kisha kuwafahamisha wajumbe maamuzi yake?
 
Usijali wewe tayari ni kiongozi mbunge wa watu, wanakupunguzia bajeti kiasi, tumia muda huu kupanga timu makini na mbinu makini.
 
Bapa ndipo nnapomchukia Magu, yupo nyuma ya michezo yoote michafu dhidi ya upinzani wa kweli!.
 
Gwajima ataaibika sana, atashindwa na "mfungwa" huu ujinga wa NEC unazidi kuwapa promo wapinzani, watanzania wa leo sio wa jana.
 
Kosa lilianzia kwa lissu kukubaliana na zile siku 7.
 
Kamati ya maadili siyo tume inawajumbe 18 wa vyama vya siasa vinavyoshiriki uchaguzi kikiwemo CHADEMA aache kulia lia mitandaoni
Hivyo vyama washirika wa CCM upuuzi mtupu, walishamuunga mkono Magufuli halafu unawapelekea kesi ya mgombea wa Chadema watoe maamuzi.. bulls.it!.
 
Halima Kawe hatukutaki. Wewe subiri uingie bungeni kwa tiketi ya viti maalum.

Rais nitampigia Lissu,ubunge nitampa kura yangu Gwajiboy. Halafu nani akufungie kampein jamani ?Acha kuleta mizengwe.
 
Pelekeni mapingamizi dhidi ya Maguful kampeni yake Ina makosa mengi ya kikanuni/kisheria.
 
Back
Top Bottom