Kamau: Rais Magufuli adhibitiwe na EAC, amevuka mipaka!

Nani kakwambia magu akikosea hakosolewi hata na wana ccm wenzake. Duh.
I'm ignoring your ignorance. Ndio maana king kaka akawaita "wajinga nyinyi".

Sent using Jamii Forums mobile app

Ndio maana pale mwanzo nilisema itakubidi utumie akili kunielewa, huko kwenu kuna tofauti kati ya MaCCM na Watanzania wazalendo, nyie MaCCM mnasifia kila kitu hata kibaya, mpo kimapambio zaidi, hamna tofauti yenu na yule jamaa anaitwa Polepole, lakini wazalendo huwa wanasheherekea mazuri na kukosoa penye mabaya.
Hebu tembelea nyuzi zinazomjadili Miguna uone ninavyoiponda serikali ya Kenyatta, lakini akitenda mazuri huwa sichelewi kusifia. Pitia huu uzi hapa Miguna Miguna, 'Le General', atangaza kurejea Kenya, Rais Uhuru amhakikishia kuwa yupo huru kurudi nchini

Ni jambo njema sana kumsifia rais wenu, maana mnampa hamasa ya kufanya mazuri hata zaidi, ila inakuwa uzezeta fulani pale mnapitiliza na kuanza kumuabudu na kutukana kila anayemkosoa.
Ona hii picha mlivyo

2257396_IMG_20191230_125043.jpeg
 
Rubbish of Mr Kamau
MNAMO Novemba 5, 1984, kinara wa ODM Raila Odinga alifahamishwa kuhusu kifo cha mamake, Bi Mary Juma ikiwa imepita muda wa miezi miwili tangu afariki.
View attachment 1314663
Mary alifariki mnamo Septemba 1984, lakini Bw Odinga hakuwa na ufahamu wowote kuhusu tukio hilo kwa kuwa alikuwa akitumikia kifungo katika Gereza la Shimo la Tewa, jijini Mombasa.

Alikuwa na mfungwa mwenzake, Bw George Anyona alipopata habari hizo za kuhuzunisha.

Kwa jumla, ilikuwa vigumu kwa wafungwa kuwasiliana na jamaa zao wakati huo kutokana na ulinzi mkali waliowekewa na serikali ya Rais Mstaafu Daniel Moi.

Kwa mujibu wa simulizi nyingi za watu waliojipata kama wafungwa wa kisiasa katika utawala wa Mzee Jomo Kenyatta na Bw Moi, walikuwa wakiwasiliana na jamaa zao kwa kuandika kwenye shashi ndipo wasijulikane na serikali.

Katika maisha, hilo ndilo mojawapo ya pigo kubwa zaidi mwanadamu yeyote anaweza kukumbana nalo; kutopata nafasi ya kumuaga mzazi, hasa mama.

Hali hiyo hiyo ndiyo imemkumba mwanahabari Eric Kabendera kutoka Tanzania, anayeendelea kuzuiliwa na serikali ya Rais John Magufuli, kwa tuhuma za kuandika habari za “uongo na kuwapotosha” wananchi.

Bw Kabendera amekuwa akizuiliwa kwa zaidi ya miezi mitatu sasa, huku juhudi zake zote kuomba msamaha Rais Magufuli zikigonga mwamba.

Serikali pia imepuuzilia mbali rai za mawakili wake kumwachilia kwa dhamana ili kuendelea na kesi yake akiwa huru.

Majuma mawili kabla ya kifo chake, Bi Verdiana Mjwahuzi alikuwa amemwomba Rais Magufuli kumsamehe mwanawe, hasa baada ya Bw Kabendera kumwandikia barua akimwomba msamaha.

Licha ya juhudi hizo zote, Bw Magufuli alifumbia macho kilio hicho cha mama kwa niaba ya mwanawe.

Taswira hii bila shaka inaondoa dhana ambayo imekuwepo kwa muda mrefu kwamba, Bw Magufuli ni “ufufuo na msisimko” wa aliyekuwa rais wa kwanza wa taifa hilo, Bw Julius Kabarage Nyerere.

Badala yake, ameibuka kuwa kiongozi wa kiimla anayeendesha taifa hilo kwa mfumo wa kidikteta.

Chini ya utawala wa Bw Magufuli, uhuru wa wanahabari umedidimia pakubwa, huku baadhi yao wakitoweka wasijulikane waliko.

Mfano dhahiri ni mwanahabari Azory Gwanda, aliyetoweka Novemba 2017 katika hali ya kutatanisha. Hadi sasa, haijulikani aliko mwanahabari huyo.

Kando na wanahabari, Tanzania pia imekuwa ikiwahangaisha viongozi wa upinzani, mmoja wao akiwa aliyekuwa mbunge wa Singinda Mashariki, Bw Tundu Lissu.

Mnamo Oktoba 2017 gari la Bw Lissu lilimiminiwa risasi zaidi ya 30 baada ya kuondoka kwenye kikao cha Bunge jijini Dodoma.

Bw Lissu, ambaye ni mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) amekuwa mkosoaji mkubwa wa utawala wa Rais Magufuli na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Alipoteza kiti chake akitafuta matibabu katika nchi mbalimbali barani Ulaya.

Bila shaka, viongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) wafaa kusimama kidete kupinga dhuluma anazoendeleza Bw Magufuli dhidi ya wapinzani wake. Kwa sasa anairejesha kanda hii katika enzi ya giza.

[email protected]

Mjumbe hauawi jamani ni kupashana habari za majirani zetu wanavyo tuona. Lakini mwandishi anasahau kuwa EAC almost 90% + ya tawala ni za kidictator. Nani amfunge Paka kengere?

Na WANDERI KAMAU

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwambie
Sijui kuhusu Msiba lkn Tanzania hakuna ,,classes” baina ya Wasomaji Magazeti kila mtu anaweza kununua Gazeti lolote na kusoma bila ya kujificha, Kenya ni tofauti, ukisoma Taifa leo unaonekana wewe ni mtu wa chini kabisa kwenye jamii ambaye haujui English language na hivyo wa kudharauliwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lkn tofauti ni kwamba Kenya wanadharau Taifa leo shauri ni la Kiswahili na siyo kilichoandikwa na hilo Gazeti kwa maaa wanasoma nation, hivyo hakuna ulinganifu.
Watanzania kama hawasomi Gazeti xyz hakuna uhusiano wowote na lugha bali ni labda maudhui ya Gazeti hilo au muelekeo wake.
Tuachane na gazeti na tujadili kilichoandikwa;Je kina ukweli au uongo?
 
Wakenya sio kama sisi wabongo, wanatuzidi ujasiri mpaka maendeleo

Kibera is a division of Nairobi Area, Kenya, and neighbourhood of the city of Nairobi, 6.6 kilometres from the city centre. Kibera is the largest slum in Nairobi, and the largest urban slum in Africa.
 
Which impact does this Kenyan moron called Wanderi Kamau have over our country so that we pay attention to what he has written?

It's very interesting that, a Kenyan moron called Wanderi Kamau can see the Magulification policies impact on our country, but you as a Tanzanian nincompoop can't see this naked impact(see Gado cartoons below for clarity).

1578393926465.png
1578393948945.png
 
Kibera is a division of Nairobi Area, Kenya, and neighbourhood of the city of Nairobi, 6.6 kilometres from the city centre. Kibera is the largest slum in Nairobi, and the largest urban slum in Africa.

Turnkey,
There're many areas of the same in Dar-es-salaam city as compared to Kibera! What about Manzese squatters or slums?
What about Jangwani Valley, Mkunguni,Mbagala and Kinondoni areas? No difference at all!
1578395099766.png
 
Kibera is a division of Nairobi Area, Kenya, and neighbourhood of the city of Nairobi, 6.6 kilometres from the city centre. Kibera is the largest slum in Nairobi, and the largest urban slum in Africa.
Ndicho wanachotuzidi?
.
Hivi masikini wa Tanzania unawajua bro walivyo wengi?
 
Ukipondwa na Gates unakuwa ni wivu? au kwa vile siyo jirani? kati ya kenya na TZ nani mwenye index kubwa ya "development"
Ni wivu tu hakuna lolote! Uchumi wa kenya umewezeshwa sana na Tz! Ngoja uone baada ya miaka kumi kukamirika kama utaleza hivyo viji'index' vyako!
 
Huu uzi wa huyu mwandishi sijui somebody kamau ni mfumo ule ule wa kina the economist.
Hakuna jipya hapa bali ni muendelezo wa makala kuandaliwa Tanzania na kina Zitto & the company.

Nakuomba kamau kama ulivyojiita usishugurike na matatizo ya huko kwenyu!

Mfano !

Handshake kati ya Uhuru na kenyatta.(inavyotaka kuligawa taifa lenu kisa mgombea urais ruto)

The arrival or comeback ya General miguna wa miguna.

Vita ya mgombea urais wa ahadi kati ya wawili hawa uhuru na mkalenjin Ruto.

Manyanyaso na udhalilishaji dhidi ya governor wa Nairobi Bw Sonko.(kisa anatetea ardhi na wanyonge wa Nairobi)

Pia mfanye uchunguzi muiambie dunia na familia ya marehemu msando,nani alimuua mtu huyo muhimu kutoka IEBC,siku chache kabla ya uchaguzi mkuu wa kenya!

Pia ni wakati wa kuandika na kuishauri serikali yenu jinsi ya kuwalipa wachina mkopo wa SGR ya mombasa to naivasha.(magufuli kwa asilimia kubwa amejenga kwa fedha ya ndani)

Pia poleni na kubanwa na al shabab kule lamu,hivyo geuza uandishi na muisaidie serikali yenu jinsi ya kuepukana na hilo janga la usalama wa ndani ya kenya.

Ukishatuambia hayo ndio uje upewe hela yako toka kwa hii team kambole na zitto.

Tanzania ni nchi huru na inapaswa kuheshimiwa maamuzi yake ya ndani.yanayokuwepo kikatiba.

Na tunaposema EAC,hatuna lengo kama unalolenga wewe unayejiita kamau.

Viva magufuli [emoji1241] 2020 - 2025 [emoji818][emoji818][emoji818][emoji818][emoji818][emoji818][emoji818]

Sent using Jamii Forums mobile app

Baba wa Taifa Mwl. Nyerere(rip) alisema; Waafrika wote ni ndugu zangu na Africa ni moja.
Idealogy hii ya Nyerere ilisaidia nchi nyingi za Kiafrika kupata Uhuru wake. Nyerere hakuwa na mawazo finyu kama yako ya kumwambia Mkenya ahangaike na mambo ya nchi kwake na asijadili mambo ya Tanzania.

Ulichoongea hapa ni kukosa akili pana na kufikiri nje ya box! Kenya ni jirani zetu na tunashirikiana nao mpaka kwenye Jumuia yetu(EAC). Hivo wana haki ya kusemea Tanzania wakiona mambo yana kwenda kombo kama vile na sisi tunaweza kuwasema tuna poona wanafanya mafyongo kwenye siasa zao za nyumbani....!!
 
Sijui kuhusu Msiba lkn Tanzania hakuna ,,classes” baina ya Wasomaji Magazeti kila mtu anaweza kununua Gazeti lolote na kusoma bila ya kujificha, Kenya ni tofauti, ukisoma Taifa leo unaonekana wewe ni mtu wa chini kabisa kwenye jamii ambaye haujui English language na hivyo wa kudharauliwa.
Nani anunue la UHURU?
 
Lkn tofauti ni kwamba Kenya wanadharau Taifa leo shauri ni la Kiswahili na siyo kilichoandikwa na hilo Gazeti kwa maaa wanasoma nation, hivyo hakuna ulinganifu.
Watanzania kama hawasomi Gazeti xyz hakuna uhusiano wowote na lugha bali ni labda maudhui ya Gazeti hilo au muelekeo wake.
Kama kiswahili kinadharaulika namna hiyo mbona mnafurahia mkisikia ni moja ya lugha inayotumika katika Bunge la Afrika Mashariki? Au hata AU na SADC? Una gubu sana wewe.
 
Kwa hiyo huko kwao mtuhumiwa akiomba msamaha kwa Kenyatta tayari anakuwa huru?
 
Tuachane na gazeti na tujadili kilichoandikwa;Je kina ukweli au uongo?
Labda tuanze na hili. Si kweli kwamba Kabendera yuko rumande kwa tuhuma za kuandika uongo. Anatuhumiwa makosa ya utakatishaji pesa na ukwepaji kodi.
 
MNAMO Novemba 5, 1984, kinara wa ODM Raila Odinga alifahamishwa kuhusu kifo cha mamake, Bi Mary Juma ikiwa imepita muda wa miezi miwili tangu afariki.
View attachment 1314663
Mary alifariki mnamo Septemba 1984, lakini Bw Odinga hakuwa na ufahamu wowote kuhusu tukio hilo kwa kuwa alikuwa akitumikia kifungo katika Gereza la Shimo la Tewa, jijini Mombasa.

Alikuwa na mfungwa mwenzake, Bw George Anyona alipopata habari hizo za kuhuzunisha.

Kwa jumla, ilikuwa vigumu kwa wafungwa kuwasiliana na jamaa zao wakati huo kutokana na ulinzi mkali waliowekewa na serikali ya Rais Mstaafu Daniel Moi.

Kwa mujibu wa simulizi nyingi za watu waliojipata kama wafungwa wa kisiasa katika utawala wa Mzee Jomo Kenyatta na Bw Moi, walikuwa wakiwasiliana na jamaa zao kwa kuandika kwenye shashi ndipo wasijulikane na serikali.

Katika maisha, hilo ndilo mojawapo ya pigo kubwa zaidi mwanadamu yeyote anaweza kukumbana nalo; kutopata nafasi ya kumuaga mzazi, hasa mama.

Hali hiyo hiyo ndiyo imemkumba mwanahabari Eric Kabendera kutoka Tanzania, anayeendelea kuzuiliwa na serikali ya Rais John Magufuli, kwa tuhuma za kuandika habari za “uongo na kuwapotosha” wananchi.

Bw Kabendera amekuwa akizuiliwa kwa zaidi ya miezi mitatu sasa, huku juhudi zake zote kuomba msamaha Rais Magufuli zikigonga mwamba.

Serikali pia imepuuzilia mbali rai za mawakili wake kumwachilia kwa dhamana ili kuendelea na kesi yake akiwa huru.

Majuma mawili kabla ya kifo chake, Bi Verdiana Mjwahuzi alikuwa amemwomba Rais Magufuli kumsamehe mwanawe, hasa baada ya Bw Kabendera kumwandikia barua akimwomba msamaha.

Licha ya juhudi hizo zote, Bw Magufuli alifumbia macho kilio hicho cha mama kwa niaba ya mwanawe.

Taswira hii bila shaka inaondoa dhana ambayo imekuwepo kwa muda mrefu kwamba, Bw Magufuli ni “ufufuo na msisimko” wa aliyekuwa rais wa kwanza wa taifa hilo, Bw Julius Kabarage Nyerere.

Badala yake, ameibuka kuwa kiongozi wa kiimla anayeendesha taifa hilo kwa mfumo wa kidikteta.

Chini ya utawala wa Bw Magufuli, uhuru wa wanahabari umedidimia pakubwa, huku baadhi yao wakitoweka wasijulikane waliko.

Mfano dhahiri ni mwanahabari Azory Gwanda, aliyetoweka Novemba 2017 katika hali ya kutatanisha. Hadi sasa, haijulikani aliko mwanahabari huyo.

Kando na wanahabari, Tanzania pia imekuwa ikiwahangaisha viongozi wa upinzani, mmoja wao akiwa aliyekuwa mbunge wa Singinda Mashariki, Bw Tundu Lissu.

Mnamo Oktoba 2017 gari la Bw Lissu lilimiminiwa risasi zaidi ya 30 baada ya kuondoka kwenye kikao cha Bunge jijini Dodoma.

Bw Lissu, ambaye ni mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) amekuwa mkosoaji mkubwa wa utawala wa Rais Magufuli na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Alipoteza kiti chake akitafuta matibabu katika nchi mbalimbali barani Ulaya.

Bila shaka, viongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) wafaa kusimama kidete kupinga dhuluma anazoendeleza Bw Magufuli dhidi ya wapinzani wake. Kwa sasa anairejesha kanda hii katika enzi ya giza.

[email protected]

Mjumbe hauawi jamani ni kupashana habari za majirani zetu wanavyo tuona. Lakini mwandishi anasahau kuwa EAC almost 90% + ya tawala ni za kidictator. Nani amfunge Paka kengere?

Na WANDERI KAMAU
Rais angeiliaje madaraka ya mhimili mwingine? Na ukweli angejaribu kufanya hivyo tu baada ya muda sisi wote tungekuwa tunamsema rais kuwa ni dikteta aliyenyakuwa madaraka ya mhimili wa Judicial. Acheni propaganda za kipuuzi kwani kuna wengi waliwahi kukutwa na hali hii na wengine wanaendelea kukutwa na hali hii wakikwa magerezani. Kama hoja yenu ina mantiki basi ipelekwe bungeni ili irasimishwe.
Magufuli is 'damned if he does and damned if he doesnt' and this has been going on for the last 4 years.
 
Back
Top Bottom