Kamau: Rais Magufuli adhibitiwe na EAC, amevuka mipaka!

Kamau: Rais Magufuli adhibitiwe na EAC, amevuka mipaka!

Napatia kwa mama yako mdogo,muulize vzr atakwambia.
Engekuwa hivyo lisingeendea kutoka kila siku! Endelea kujidanganya kwanza wewe hata pesa ya kununua gazeti utapata wapi wakati ni kula kulala??

dodge
 
Na WANDERI KAMAU

MNAMO Novemba 5, 1984, kinara wa ODM Raila Odinga alifahamishwa kuhusu kifo cha mamake, Bi Mary Juma ikiwa imepita muda wa miezi miwili tangu afariki.

Mary alifariki mnamo Septemba 1984, lakini Bw Odinga hakuwa na ufahamu wowote kuhusu tukio hilo kwa kuwa alikuwa akitumikia kifungo katika Gereza la Shimo la Tewa, jijini Mombasa.

Alikuwa na mfungwa mwenzake, Bw George Anyona alipopata habari hizo za kuhuzunisha.

Kwa jumla, ilikuwa vigumu kwa wafungwa kuwasiliana na jamaa zao wakati huo kutokana na ulinzi mkali waliowekewa na serikali ya Rais Mstaafu Daniel Moi.

Kwa mujibu wa simulizi nyingi za watu waliojipata kama wafungwa wa kisiasa katika utawala wa Mzee Jomo Kenyatta na Bw Moi, walikuwa wakiwasiliana na jamaa zao kwa kuandika kwenye shashi ndipo wasijulikane na serikali.

Katika maisha, hilo ndilo mojawapo ya pigo kubwa zaidi mwanadamu yeyote anaweza kukumbana nalo; kutopata nafasi ya kumuaga mzazi, hasa mama.

Hali hiyo hiyo ndiyo imemkumba mwanahabari Eric Kabendera kutoka Tanzania, anayeendelea kuzuiliwa na serikali ya Rais John Magufuli, kwa tuhuma za kuandika habari za “uongo na kuwapotosha” wananchi.

Bw Kabendera amekuwa akizuiliwa kwa zaidi ya miezi mitatu sasa, huku juhudi zake zote kuomba msamaha Rais Magufuli zikigonga mwamba.

Serikali pia imepuuzilia mbali rai za mawakili wake kumwachilia kwa dhamana ili kuendelea na kesi yake akiwa huru.

Majuma mawili kabla ya kifo chake, Bi Verdiana Mjwahuzi alikuwa amemwomba Rais Magufuli kumsamehe mwanawe, hasa baada ya Bw Kabendera kumwandikia barua akimwomba msamaha.

Licha ya juhudi hizo zote, Bw Magufuli alifumbia macho kilio hicho cha mama kwa niaba ya mwanawe.

Taswira hii bila shaka inaondoa dhana ambayo imekuwepo kwa muda mrefu kwamba, Bw Magufuli ni “ufufuo na msisimko” wa aliyekuwa rais wa kwanza wa taifa hilo, Bw Julius Kabarage Nyerere.

Badala yake, ameibuka kuwa kiongozi wa kiimla anayeendesha taifa hilo kwa mfumo wa kidikteta.

Chini ya utawala wa Bw Magufuli, uhuru wa wanahabari umedidimia pakubwa, huku baadhi yao wakitoweka wasijulikane waliko.

Mfano dhahiri ni mwanahabari Azory Gwanda, aliyetoweka Novemba 2017 katika hali ya kutatanisha. Hadi sasa, haijulikani aliko mwanahabari huyo.

Kando na wanahabari, Tanzania pia imekuwa ikiwahangaisha viongozi wa upinzani, mmoja wao akiwa aliyekuwa mbunge wa Singinda Mashariki, Bw Tundu Lissu.

Mnamo Oktoba 2017 gari la Bw Lissu lilimiminiwa risasi zaidi ya 30 baada ya kuondoka kwenye kikao cha Bunge jijini Dodoma.

Bw Lissu, ambaye ni mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) amekuwa mkosoaji mkubwa wa utawala wa Rais Magufuli na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Alipoteza kiti chake akitafuta matibabu katika nchi mbalimbali barani Ulaya.

Bila shaka, viongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) wafaa kusimama kidete kupinga dhuluma anazoendeleza Bw Magufuli dhidi ya wapinzani wake. Kwa sasa anairejesha kanda hii katika enzi ya giza.

[email protected]

Mjumbe hauawi jamani ni kupashana habari za majirani zetu wanavyo tuona. Lakini mwandishi anasahau kuwa EAC almost 90% + ya tawala ni za kidictator. Nani amfunge Paka kengere?
Kuna wakati mtu anaamua kuwa mjinga akiamini yuko sahihi. Nchini Kenya ni kawaida kuteteana kwa ukabila. Kila mtu anatetea kabila lake kwa makosa yoyote yale. Tanzania tunapiga vita upuuzi huo na sasa linaibuka hili la kuteteana kwa kufuata umaarufu na uhusiano wa kitaaluma. CCM waliteteana miaka mingi, Magufuli kawakomesha.

Wanasheria wanatetea wanasheria wenzao na kuwaonesha kwamba hawana makosa. Waandishi habari na wanasiasa ni hivyo hivyo. Huu ni upuuzi! Nani atawatetea wakulima na wafugani na watu wa juakali? Ndo maana nasema ukiwa mjinga ukaamua kujinyonga, tafuta kamba ngumu. Kabendela siyo mtu pekee ndani ya mahabusu. Wangapi wamepewa dhamana ya kwenda kwenye mazishi ya mama zao hapa TZ au huko Kenya wana raha hiyo? Au ni imani kwamba woote walio mahabusu hakuna aliyefiwa na mama? Au Kabendela aachiwe kwa sababu ni mwandishi habari? That's nuisance of nonsense!
 
Hahahaha! Nilitaka tu uthibitisho ili adhalilike mwana Lumumba huyo

Hao wapo kibiashara humu, huna lolote unaloweza kumfanya adhalilike, huandika utumbo kwa makusudi wakijua wanazingua, lakini kwa vile inampa kipato cha buku kadhaa pale Lumumba, hajali hata ukimuumbua vipi, bado atakuja na lingine.
Wewe ndiye utachoka maana unahangaika kushughulisha ubongo ili kujenga hoja na mantiki, ila yeye anaandika ilmradi aonekane yupo busy anazingua na kupata cha kwake fasta.
 
"Uhuru wa wanahabari umedidimia pakubwa" Ni kweli kabisaa.
 
We kama malayamalaya,kuna wakati humu uliwahi kusema Mkenya,ilikuwa mjadala wa ujenzi wa miji,leo unasema umedfika huko,
Hakuna gazeti linalodharauliwa na Wakenya kama Taifa leo, nimefika huko mara nyingi, huwa nikinunua hilo Gazeti wananishangaa na kunicheka sana, hivyo hiyo siyo newsworthy kwa Mkenya.
 
Wangapi wamepewa dhamana ya kwenda kwenye mazishi ya mama zao hapa TZ au huko Kenya wana raha hiyo? Au ni imani kwamba woote walio mahabusu hakuna aliyefiwa na mama? Au Kabendela aachiwe kwa sababu ni mwandishi habari? That's nuisance of nonsense!
I guess you are not informed or you are a lunatic! hypocrite! It is as if you are unaware of the political environment currently Tanzania is undergoing!. Unaonekana kama vile msomi maana kiingereza chako kidogo kina mwanga. The concern of most contributors on this thread particularly the Issue of Kabendera is not PROSECUTION , but PERSECUTION! definitely under the prevailing political "turmoil" in Tanzania with respect to a compromised judiciary, toothless parliament, and an omnipotent president!
 
Hao wapo kibiashara humu, huna lolote unaloweza kumfanya adhalilike, huandika utumbo kwa makusudi wakijua wanazingua, lakini kwa vile inampa kipato cha buku kadhaa pale Lumumba, hajali hata ukimuumbua vipi, bado atakuja na lingine.
Wewe ndiye utachoka maana unahangaika kushughulisha ubongo ili kujenga hoja na mantiki, ila yeye anaandika ilmradi aonekane yupo busy anazingua na kupata cha kwake fasta.
I didn't knew this kwa kweli.
Ahsante kwa taarifa
 
Mh, it is true, acha urongo, we mwenyewe upo kazini mtandaoni huku kutetea kila jambo la jubilee.

Sent using Jamii Forums mobile app

Itahitaji kutumia akili kuelewa mada zangu, mimi sio mfuasi wa chama chochote, nipo kiuzalendo zaidi, chochote kizuri kwenye nchi yetu natetea, hutakuta nikifanya ujinga mnaofanya nyie MaCCM, kushabikia hata mabaya, kwa mfano bila aibu unakuta mnashabikia Tundu Lissue kupigwa marisasi, hebu nionyeshe mada au uzi wowote ambao mimi nimeshabikia udhalimu wa serikali.
Rais Kenyatta akizingua huwa namponda maana kwetu hapa uhuru huo tunao, lakini haina maana nianze kuponda miradi ya serikali, penye mazuri tunasifia na pia tunawatambia kwenye ligi za Ke/Tz
 
kwahiyo sisi tukisifia rais wetu basi ni maccm,ila wewe ukimsifia uhuru basi ni haki yako.

hapa ndio huwa nashindwa kumtofautisha binaadamu kama wewe na kuku.
 
  • Thanks
Reactions: Oii
Itahitaji kutumia akili kuelewa mada zangu, mimi sio mfuasi wa chama chochote, nipo kiuzalendo zaidi, chochote kizuri kwenye nchi yetu natetea, hutakuta nikifanya ujinga mnaofanya nyie MaCCM, kushabikia hata mabaya, kwa mfano bila aibu unakuta mnashabikia Tundu Lissue kupigwa marisasi, hebu nionyeshe mada au uzi wowote ambao mimi nimeshabikia udhalimu wa serikali.
Rais Kenyatta akizingua huwa namponda maana kwetu hapa uhuru huo tunao, lakini haina maana nianze kuponda miradi ya serikali, penye mazuri tunasifia na pia tunawatambia kwenye ligi za Ke/Tz

Yule jamaa aliyeimba waninga nyinyi tayari kashakoswakoswa na Risasi mara kadhaa[emoji2][emoji2]
 
Itahitaji kutumia akili kuelewa mada zangu, mimi sio mfuasi wa chama chochote, nipo kiuzalendo zaidi, chochote kizuri kwenye nchi yetu natetea, hutakuta nikifanya ujinga mnaofanya nyie MaCCM, kushabikia hata mabaya, kwa mfano bila aibu unakuta mnashabikia Tundu Lissue kupigwa marisasi, hebu nionyeshe mada au uzi wowote ambao mimi nimeshabikia udhalimu wa serikali.
Rais Kenyatta akizingua huwa namponda maana kwetu hapa uhuru huo tunao, lakini haina maana nianze kuponda miradi ya serikali, penye mazuri tunasifia na pia tunawatambia kwenye ligi za Ke/Tz
Nani kakwambia magu akikosea hakosolewi hata na wana ccm wenzake. Duh.
I'm ignoring your ignorance. Ndio maana king kaka akawaita "wajinga nyinyi".

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom