Kamau: Rais Magufuli adhibitiwe na EAC, amevuka mipaka!

Kamau: Rais Magufuli adhibitiwe na EAC, amevuka mipaka!

Kama kiswahili kinadharaulika namna hiyo mbona mnafurahia mkisikia ni moja ya lugha inayotumika katika Bunge la Afrika Mashariki? Au hata AU na SADC? Una gubu sana wewe.


Umeelewa nilichoandika? Wakenya wanadharau Kiswahili na siyo mimi, mimi ni lugha yangu na kamwe siwezi kujidharau.
 
Labda tuanze na hili. Si kweli kwamba Kabendera yuko rumande kwa tuhuma za kuandika uongo. Anatuhumiwa makosa ya utakatishaji pesa na ukwepaji kodi.
Na Kabendera akiwa kama mtuhumiwa anapewa haki zote zilizoainishwa kisheria pasipo uingiliaji wowote wa mamlaka za juu?
 
"Katika maisha, hilo ndilo mojawapo ya pigo kubwa zaidi mwanadamu yeyote anaweza kukumbana nalo; kutopata nafasi ya kumuaga mzazi, hasa mama."

Eti mzazi, hasa Mama.

Mwandishi bado mchanga sana kwa upeo.
 
Ndio maana pale mwanzo nilisema itakubidi utumie akili kunielewa, huko kwenu kuna tofauti kati ya MaCCM na Watanzania wazalendo, nyie MaCCM mnasifia kila kitu hata kibaya, mpo kimapambio zaidi, hamna tofauti yenu na yule jamaa anaitwa Polepole, lakini wazalendo huwa wanasheherekea mazuri na kukosoa penye mabaya.
Hebu tembelea nyuzi zinazomjadili Miguna uone ninavyoiponda serikali ya Kenyatta, lakini akitenda mazuri huwa sichelewi kusifia. Pitia huu uzi hapa Miguna Miguna, 'Le General', atangaza kurejea Kenya, Rais Uhuru amhakikishia kuwa yupo huru kurudi nchini


Ni jambo njema sana kumsifia rais wenu, maana mnampa hamasa ya kufanya mazuri hata zaidi, ila inakuwa uzezeta fulani pale mnapitiliza na kuanza kumuabudu na kutukana kila anayemkosoa.
Ona hii picha mlivyo


2257396_IMG_20191230_125043.jpeg
Mwanaume nae kupenda kusifiwa uleta shaka ya utimamu wa saikolojia yake.
 
"Katika maisha, hilo ndilo mojawapo ya pigo kubwa zaidi mwanadamu yeyote anaweza kukumbana nalo; kutopata nafasi ya kumuaga mzazi, hasa mama."

Eti mzazi, hasa Mama.

Mwandishi bado mchanga sana kwa upeo.
Mchanga kiupeo uandikia uhuru na tanzanite unajua the economist usomwa na watu gani?
 
Jumuia za kimataifa zingeanza na kuziwekea vikwazo vya kusafiri wao na familia zao yaani lifeburn ya kukanyaga ulaya na USA.
Hawa jamaa ni very shortminded kwanza tayari washaharibu future za watoto zao bad image kwenye wataelewa wakiwa nje ya mfumo.Leo ukisikia mtoto wa mugabe,mobutu,amini,bokasa,Osama hawana respect kwenye jamii walisharaibiwa na wazazi wao sababu ya maovu waliyoitendea jamii.
 
Retired

BUSARA HUTUMIKA PANAPOKUA HAKUNA SHERIA.

Ulishawaza kwamba wapo wangapi ambao wamekutwa na kadhia hiyo? Kama argument yako ita-base kwamba kaonewa ndio kisa cha kelele zako hizi, iwapi haja ya kuwa na mahakama kama hukumu tunazijua.

Kamanda Abdallah Zimbe alishahukumiwa na magazeti yote ya Tanzania lakini mahakama ilikuja kuamua tofauti.

Kama mnazo agenda zenu za siri msitulazimishie sympathy

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kamau


MNAMO Novemba 5, 1984, kinara wa ODM Raila Odinga alifahamishwa kuhusu kifo cha mamake, Bi Mary Juma ikiwa imepita muda wa miezi miwili tangu afariki.
View attachment 1314663
Mary alifariki mnamo Septemba 1984, lakini Bw Odinga hakuwa na ufahamu wowote kuhusu tukio hilo kwa kuwa alikuwa akitumikia kifungo katika Gereza la Shimo la Tewa, jijini Mombasa.

Alikuwa na mfungwa mwenzake, Bw George Anyona alipopata habari hizo za kuhuzunisha.

Kwa jumla, ilikuwa vigumu kwa wafungwa kuwasiliana na jamaa zao wakati huo kutokana na ulinzi mkali waliowekewa na serikali ya Rais Mstaafu Daniel Moi.

Kwa mujibu wa simulizi nyingi za watu waliojipata kama wafungwa wa kisiasa katika utawala wa Mzee Jomo Kenyatta na Bw Moi, walikuwa wakiwasiliana na jamaa zao kwa kuandika kwenye shashi ndipo wasijulikane na serikali.

Katika maisha, hilo ndilo mojawapo ya pigo kubwa zaidi mwanadamu yeyote anaweza kukumbana nalo; kutopata nafasi ya kumuaga mzazi, hasa mama.

Hali hiyo hiyo ndiyo imemkumba mwanahabari Eric Kabendera kutoka Tanzania, anayeendelea kuzuiliwa na serikali ya Rais John Magufuli, kwa tuhuma za kuandika habari za “uongo na kuwapotosha” wananchi.

Bw Kabendera amekuwa akizuiliwa kwa zaidi ya miezi mitatu sasa, huku juhudi zake zote kuomba msamaha Rais Magufuli zikigonga mwamba.

Serikali pia imepuuzilia mbali rai za mawakili wake kumwachilia kwa dhamana ili kuendelea na kesi yake akiwa huru.

Majuma mawili kabla ya kifo chake, Bi Verdiana Mjwahuzi alikuwa amemwomba Rais Magufuli kumsamehe mwanawe, hasa baada ya Bw Kabendera kumwandikia barua akimwomba msamaha.

Licha ya juhudi hizo zote, Bw Magufuli alifumbia macho kilio hicho cha mama kwa niaba ya mwanawe.

Taswira hii bila shaka inaondoa dhana ambayo imekuwepo kwa muda mrefu kwamba, Bw Magufuli ni “ufufuo na msisimko” wa aliyekuwa rais wa kwanza wa taifa hilo, Bw Julius Kabarage Nyerere.

Badala yake, ameibuka kuwa kiongozi wa kiimla anayeendesha taifa hilo kwa mfumo wa kidikteta.

Chini ya utawala wa Bw Magufuli, uhuru wa wanahabari umedidimia pakubwa, huku baadhi yao wakitoweka wasijulikane waliko.

Mfano dhahiri ni mwanahabari Azory Gwanda, aliyetoweka Novemba 2017 katika hali ya kutatanisha. Hadi sasa, haijulikani aliko mwanahabari huyo.

Kando na wanahabari, Tanzania pia imekuwa ikiwahangaisha viongozi wa upinzani, mmoja wao akiwa aliyekuwa mbunge wa Singinda Mashariki, Bw Tundu Lissu.

Mnamo Oktoba 2017 gari la Bw Lissu lilimiminiwa risasi zaidi ya 30 baada ya kuondoka kwenye kikao cha Bunge jijini Dodoma.

Bw Lissu, ambaye ni mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) amekuwa mkosoaji mkubwa wa utawala wa Rais Magufuli na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Alipoteza kiti chake akitafuta matibabu katika nchi mbalimbali barani Ulaya.

Bila shaka, viongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) wafaa kusimama kidete kupinga dhuluma anazoendeleza Bw Magufuli dhidi ya wapinzani wake. Kwa sasa anairejesha kanda hii katika enzi ya giza.

[email protected]

Mjumbe hauawi jamani ni kupashana habari za majirani zetu wanavyo tuona. Lakini mwandishi anasahau kuwa EAC almost 90% + ya tawala ni za kidictator. Nani amfunge Paka kengere?

Na WANDERI KAMAU
Kamau kwanini asimshauri Rais wake kumrejeshea uraia na passport Bwana Miguna?. Huyo Kabendera ametukosea sana Watanzania kama Taifa kwa kujipendekeza kwa Mabeberu, ni adui wa Taifa.
 
Lkn anajadiliwa kwa english Kenya kwenye media zote ila Tundu Lisu ndo anayedharauliwa hajawahi kujadiliwa ( Kenya) kwa english hata siku moja pamoja na kujipendekeza kwake kote kwa Wakenya, kwanza hata hawamjui!
Hivi umeandika kitu gani???

Na ulikuwa unataka kueleza nini kuhusu uzi huu?

Kama utalipwa hizo buku saba, leo leo navaa jezi za inzi wa kijani.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Waanze kwanza kumdhibiti Kenyatta, Kenyatta kamzuia tena Miguna Miguna kuingia nchini Kenya , kakwama uwanja wa ndege ujerumani, mseveni juzi kamrudisha demu mmoja wa SA kwa kupiga picha na mpinzani wake Uganda,yanayofanyika Tanzania yanafanyika kote EAC.
 
Back
Top Bottom