Texas Tiger
JF-Expert Member
- Nov 5, 2022
- 483
- 1,100
Mmmmmm hawatajibu hayo nina hakika jeuri watasema wewe ni nani ? Mamlaka au?Ni jambo la uzuri kuweka hapa mchanganuo wote na proposal ilopelekea huyo mzabuni kushinda zabuni.
Pia hata tukifahamu gharama ya kamera moja.
Nani atasimamia hizo CCTV masaa 24?
Ujuzi wao kusimamia CCTV na kadhalika.
Subiri tender itoke utaona specs......Hiyo ni government grade surveillance system, sivyo?
Kama ndiyo hii Tzs514m ni high end estimate.
Hatutakuwa tumepigwa iwapo…
Deal inahusisha installation and integration lakini pia zinatumika high end cameras Type: 4K, PTZ (Pan-Tilt-Zoom), Night Vision.
Pia kutakuwa na software inayorun AI analytics mfano facial recognition, License Plate recognition, Behavior detection etc.
Kama cameras zitakuwa ni basic models hazina advanced storage au integration basi hakika tumepigwa.
Wewe una akili ya aina gani? Dah 🙌🏾Ili huu mjadala uwe na maana, hebu tufanye uchambuzi mdogo hapa kwa bei na gharama za soko zilizopo kwa sasa. Hii itasaidia kupima kwa uhakika.
Nitafanya uchambuzi wa shughuli hii kwa ununuzi kamera za kiwango cha juu, tukichukua gharamani za vifaa, installation na huduma za ziada baada ya ufungaji.
Hii itatufanya tuweze kuona kama bei ya Tsh milioni 514 ni halali au ni ya juu kuliko inavyostahili.
1. UFUNGA KAMERA ZA CCTV ZA KIWANGO CHA JUU
Kamera 40 zitafungwa katika soko la Kariakoo kwa madhumuni ya kuimarisha usalama.
Kamera hizi zitahakikisha maeneo yote muhimu ya soko yanachunguzwa na kurekodiwa kwa video, hivyo kusaidia kupambana na wizi, ghasia, na uhalifu mwingine.
Kamera zitahakikisha usalama wa wateja na wafanyabiashara katika soko kubwa na lenye shughuli nyingi.
Aina ya Kamera Zitatumika
Kamera ni lazima ziwe za ubora wa picha wa juu, kuhakikisha kuwa picha zinakuwa wazi hata kwenye giza, zina uwezo wa kupiga picha kwa umbali mrefu, na zina teknolojia ya kutambua harakati.
Nitachambua baadhi ya kamera za kiwango cha juu ambazo zinaweza kutumika kwenye mradi huu.
2. AINA ZA KAMERA ZA KIWANGO CHA JUU NA BEI ZAKE
(A) Axis Communications Q-Series
- 4K resolution (Picha za ubora wa juu)
- Bei: Tsh 10,000,000 - 20,000,000 kwa kila kamera
- Sifa:
- Infrared night vision
- AI Motion Detection
- Face Recognition Technology
- IP67-rated (Inafaa kutumika kwenye hali mbaya ya hewa)
- Cloud storage kwa usalama wa data
- Kiasi cha Kamera: 40 kamera
- Jumla ya Gharama kwa Kamera 40: 40 × Tsh 15,000,000 = Tsh 600,000,000 (Bei ya wastani kwa kila kamera).
(B) Bosch MIC IP Fusion 9000i
- 40x optical zoom
- Bei: Tsh 8,000,000 - 15,000,000 kwa kila kamera
- Sifa:
- Thermal imaging (Mwangaza wa joto kwa ulinzi wa hali ya juu)
- Weather-resistant
- Real-time video streaming
(C) Hikvision DarkfighterX Series
- Kiasi cha Kamera: 40 kamera
- Jumla ya Gharama kwa Kamera 40: 40 × Tsh 12,000,000 = Tsh 480,000,000.
- Super low-light performance
- Bei: Tsh 7,000,000 - 12,000,000 kwa kila kamera
- Sifa:
- True color night vision
- Smart IR technology
- IP67 rating
3. GHARAMA ZA USAKINISHAJI, VIFAA VYA ZIADA, NA HUDUMA ZA BAADA YA USAKINISHAJI
- Kiasi cha Kamera: 40 kamera
- Jumla ya Gharama kwa Kamera 40: 40 × Tsh 10,000,000 = Tsh 400,000,000.
(A) Gharama za Usakinishaji na Wiring
Usakinishaji wa kamera za CCTV unahitaji nyaya za umeme, switches, na vifaa vya kuunganishia ili kuhakikisha kila kamera inafanya kazi ipasavyo.
Hii itajumuisha wiring kutoka kwenye NVR (Network Video Recorder) hadi kwa kamera. Hii inaweza kugharimu Tsh 70,000,000 kwa mradi mkubwa kama huu.
(B) Mfumo wa Kuhifadhi Video (NVR / Server)
Kamera 40 za CCTV zitahitaji server au NVR (Network Video Recorder) ili kuhifadhi video inayoendelea kurekodiwa kutoka kwenye kamera. Mfumo huu utakuwa na uwezo wa kuhifadhi video kwa siku kadhaa ili kurahisisha upatikanaji wa video endapo kutahitajika kwa uchunguzi wa uhalifu.
- Gharama ya NVR/Server: Tsh 50,000,000 (kwa uwezo wa kuhifadhi video kwa muda mrefu, na salama).
(C) Gharama za Monita na Vifaa vya Kuonyesha Video
Kwa ufanisi, itahitaji monita (screens) kwa ajili ya kuangalia video za kamera, ambapo vituo vya kudhibiti usalama vitahitaji kuunganishwa na monita za ubora wa juu.
- Gharama za Monita: Tsh 10,000,000.
(D) Huduma za Matengenezo ya Baada ya Usakinishaji
Baada ya kuanzishwa kwa kamera, itahitajika huduma ya matengenezo na usimamizi wa vifaa, ili kuhakikisha kwamba vifaa vinaendelea kufanya kazi ipasavyo na kuwa na matengenezo ya mara kwa mara.
- Gharama za Huduma ya Matengenezo (kwa mwaka): Tsh 20,000,000.
4. UWEZEKANO WA GHARAMA YA TSH MILIONI 514
Gharama za Vifaa (Kamera)
Tuchukulie tunatumia Hikvision DarkfighterX Series kwa bei ya wastani ya Tsh 10,000,000 kwa kamera.
- Jumla ya Kamera 40: 40 × Tsh 10,000,000 = Tsh 400,000,000
Gharama za Usakinishaji na Vifaa Vya Ziada
Jumla ya Gharama:
- Usakinishaji & Wiring: Tsh 70,000,000
- NVR/Server: Tsh 50,000,000
- Monita: Tsh 10,000,000
- Huduma ya Matengenezo: Tsh 20,000,000
Tsh 400,000,000 (kamera) + Tsh 70,000,000 (usakinishaji) + Tsh 50,000,000 (NVR/Server) + Tsh 10,000,000 (monita) + Tsh 20,000,000 (huduma) = Tsh 550,000,000.
5. MAJUMUISHO
Kwa kutumia kamera za kiwango cha juu kama Hikvision DarkfighterX Series, gharama halisi ya mradi huu ni karibu Tsh 550,000,000, ambayo ni zaidi ya Tsh milioni 514 zinazozungumziwa.
Hivyo, kazi yetu kwenye hili ni kujua ni aina gani ya kamera na vifaa vingine vitakavyotumika kwa shughuli hii ili kuona gharama iliyotajwa itaendana na bei husika.
Ova
Sidhani, hiyo ya AI analytics na hizo zingine kama Facial recognition, License plate recognition, na Behaviour Detection zahitaji framework, regulation, guidance na code of conduct.Hiyo ni government grade surveillance system, sivyo?
Kama ndiyo hii Tzs514m ni high end estimate.
Hatutakuwa tumepigwa iwapo…
Deal inahusisha installation and integration lakini pia zinatumika high end cameras Type: 4K, PTZ (Pan-Tilt-Zoom), Night Vision.
Pia kutakuwa na software inayorun AI analytics mfano facial recognition, License Plate recognition, Behavior detection etc.
Kama cameras zitakuwa ni basic models hazina advanced storage au integration basi hakika tumepigwa.
Mkuu ni kamera 4,000 au 400 au 40??Umoja, amani na utulivu wa waTanzania wote Taifa katika kila kona na pembe ya nchi yetu, vitalindwa kwa nguvu na gharama yoyote bila kujali kelele au mdomo wa kibaka au tapeli yoyote wa kisiasa nchini.
Kamera za specifications gani?Kulinda umoja na amani kwa kuliibia Taifa? Kweli mpo vizuri. Kamera 40 tu kwa Milioni 514?
Kweli CCM mpo vizuri kuliibia Taifa.
Mkuu ujue kwa fedha ya Bilioni 1, hapa una maanisha Kamera 1 shilingi milioni 25,700,000/=. Duh!!nadhani ilifaa kua 1 billion kabisa,
kwasababu usalama wa Taifa na wananchi wake ni muhimu sana na gharama yake haipimwi kwa fedha
ni muhimu ikafahamika kwamba kwa nguvu na gharama yoyote ile usalama wa waTanzania utazingatiwa na serikali sikivu ya CCM gentleman bila mbambamba yoyote
Mkuu hakuna anayepinga wazo, uamuzi na umuhimu wa kufunga Kamera Kariokoo.Zitasaidia kukamata mizigo isiyolipiwa ushuru au kukamata vibaka wanaochomoa simu za watu!? 😊😊 nauliza tu lakini.
Wakati wa JPM pale bandari nasikia zilifungwa takribani 400 zikaunganishwa na Magogoni ili kumsaidia mhe.kujua kinachoendelea! Naona ni kama zilisaidia.
Mkuu kulikuwepo na Kamera wakati Tundu Lissu anacharazwa risasi, ilisadia nini hadi wa leo???sidhani kama kupoteza uhai na maisha hata ya mtu moja tukwasababu za kiusalama kudorora, inaweza kulinganishwa na milioni 514 au hata billion gentleman.
I think ilisha tangazwa na viongozi wetu kitaifa kwamba,
there will be no discussions katika suala la usalama wa watu, makazi na biashara zao.
umoja, amani na utulivu wa waTanzania popote walipo utalindwa kwa nguvu na gharama zote bila mbambamba za kibaka au tapeli yoyote wa kisiasa
Mkuu si utupe mchanganuo, ni rahisi tu. Bila mchanganuo wewe ndiye unayeleta utani hapa!!Hizo pesa ni ndogo sana. Kwa Camera arobaini?
Hivi mnataka waweke camera za aina gani hapo Kariakoo? CutePanda? Ring doorbell camera?
=============
Hivi bakresa ametumia kiasi gani cha pesa kufunga cctv camera azam tv? Acheni utani.
Mkuu kwani Kariakoo ndio Tanzania nzima, na Kamera 40 zitaona mitaa na vichochoro vyote vya Kariakoo???na zitafungwa tu bila mbambamba za mtu yeyote yule, kwa maslahi mapana ya taifa
🤣 🤣 🤣Hiyo Camera ya Mil 12 itakuwa inaona mpaka maungo ya watu waliovaa nguo.
🤔 🤔 🤔kikao walichokaa kuidhinisha hiyo tenda kimegharimu kiasi gani?
Hahahahaha umempiga za chembeHadi wewe kibaraka wa CCM umeona wizi wa watu wenu.
Ndo mjue CCM hamfai na mnaliibia hili Taifa vibaya sana!
Tuambie wewe ni gharama kiasi gani inahitajikaKatika kuhakikisha biashara zinafanyika saa
24, Jiji la Dar es Salaam limeingia mkataba na Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA) unaogharimu jumla ya shilingi milioni 514 wa usimikaji wa mifumo ya kamera za ulinzi katika barabara na maeneo ya Kariakoo ambapo jumla ya kamera 40 zitakazofanya kazi kwa saa 24 zitafungwa katika awamu ya kwanza ya mpango huo kwa ajili ya ufuatiliaji wa hali ya usalama na udhibiti wa matukio ya kihalifu.
Akizungumza baada ya kusaini makubaliano hayo Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo amesema lengo la mpango huo ni kuimarisha usalama wa wanachi na wafanyabiashara na kuongeza ufanisi wa shughuli za kibiashara.
Amesema, kamera hizo hizo zitasaidia kurahisisha utambuzi wa matukio, kuimarisha ufuatiliaji wa wahalifu na kutoa ushahidi wa haraka inapohitajika.
My take:
Hawa watu wanaliibia sana hili Taifa na ifike wakati wenye akili kwenye vyombo vya dola waungane na Wananchi Wazalendo wachukuliwe hatua.
Baada ya Wizi mkubwa uliofanywa kwa kuongeza gharama za ujenzi wa viwanja vya michezo, leo umesainiwa mkataba kufunga Kamera 40 tu Kariakoo kwa gharama ya milioni 514.
Acha niendelee kuwaamini CHADEMA kuwa No Reform No Election. Nchi hii inaibiwa sana
View attachment 3240972