Money Penny
JF-Expert Member
- Jun 20, 2016
- 17,694
- 17,131
- Thread starter
- #61
NANI MDOGOWAKO SASA?Unajua ngoja nikuambie kitu mdogo wangu Money Penny. Hapa duniani usipokua makini kuna watu wanaweza wakakuvurugia maisha bila sababu yoyote.
Mimi najua kila mtu ana madhambi yake ambayo asingependa jamii iyajue. Mfano kama mke wangu anachepuka, na anafanya kwa siri ili mimi nisijue, kwangu mimi huyo mke ananipenda na kuniheshimu sana ndio maana anafanya kwa kificho!
Sasa wewe unapomuona sehemu kajificha halafu unakuja kuniambia, we unataka nini kama sio kutufarakanisha?
Ujinga ni kujiaminisha kwamba wewe umeoa/lewa na malaika ambae hafanyi hayo mambo.