Tetesi: Kampeni ya kumpongeza Rais Samia imetumia billion 80. Je, huu sio upigaji?

Wadau katika kuongea na mdau serikalini ngazi za juu kanitonya kuwa gharama iliyotumia katika kampeni ya kumpongeza Samia inakadiliww kufikia sh Billion 80Tz. Hizi ni Gharama za posho za vikao vya kamati mbalimbali kuanzia ngazi ya serikali na chama Kwenye kata, wilaya, mkoa na Taifa.

Gharama za vyombo vya habari, machapisho, mabango etc. Huyu mtu Yuko ofisi ya TAKUKURU. Kanitonya hivyo ni kwa mjibu wa riport walizozikusanya na bado wanaendele kuzifanyia KAZI.

Kwa kifupi kila sherehe unayoona ni upigaji ndo agenda iliyo nyuma yake. Je, ni fair kutumia billion 80 Kwenye sherehe ya kumpongeza wakati shule za msingi hazina hata vyoo vya maana?
Pesa za ndani zinapigwa sana Kisha tunaomba misaada na kuwapigia magoti wazungu .
Juzi Makamu wa Rais wa Marekani alipokuja Tumepewa Dola mil. 8 sawa na bil 20 za kitanzania na Marekani kama Msaada Kwa masharti ya Kuruhusu Demokrasia na ndoa za jinsia Moja.

Kupanga ni kuchagua.
Tatizo wa Tanzania tunawaonea huruma matajiri kuliko maskini.
Yaani viongozi wanapiga mabilion ya pesa lakini uchaguzi ukifika tunasema tumwache amalize muda wake astaafu kama wenzake . Yaani ujinga mtupu.

Badala ya kusema hapa alipofikia basi apumzike hata kama ni mwaka mmoja. Sasa pamekua na desturi Rais akiingia ni lazima amalize miaka Kumi. Mpaka tunampa Mungu kazi ya kututeulia viongozi wakati alitupa nafasi ya Kuchagua .

CCM ilitakiwa iwe imeondoka madarakani Tangu 1995 . Leo Tungekua tumeshaibadili Tanzania na kuweka mifumo ya kuwawajibisha wezi na wapigaji. Kwa Sasa CCM wanaoneana aibu mana kila mmoja anawaza Kupiga au kuteuliwa akapige . Na kila mmoja anawaza siku Moja atapata nafasi ya Kupiga.
Kuna mama mmoja ni mwanafunzi wa Chuo Fulani katokea kazini yaani wanaambizana kuwa watafute Kadi ya CCM ili wapate uteuzi wakimaliza Chuo au wapandiswe vyeo wakati wanafanya kazi za umma zisizohusika kwenye siasa.
Wanasema hawapendi CCM ila wanataka maslahi yanayopatikana ndani ya CCM.

Wananchi wangekua na akili CCM haipaswi kupata kura zaidi ya 25% kwani haiwezekani vyakula vimepanda Bei halafu watu wanaandaa sherehe nchi nzima kushangalia mafanikio ya Rais.
Tulitegemea Rais apige marufuku hizo sherehe na pesa hizo ziwekwe kwenye mfuko wa njaa na kuagiza mahindi na Mengine Kununua mahindi ya ndani na mchele, mafuta n.k na Kisha kusambaza kwenye maghala nchi nzima ili mahindi yabakie kuuza sh. 800 / Kwa kilo mpaka hapo Hali ya mavuno itakapotengemaa na mvua kuonyesha na mavuno yaliyokusudiwa kupatikana Toka Kwa WAKULIMA wa ndani.

Rais katika Hali ya dharura ukionyesha kuguswa na maisha ya watu hasa wakati wa njaa na dhiki hakika huna haja ya kufanya tathimini mana jamii nzima inahitaji chakula . Kura nyingi zinatokana na maskini ambao wanaumizwa na mfumuko wa Bei ya chakula na sio hao wakuu wa Wilaya na mikoa wanatengeneza michongo ya Kupiga pesa ili watoto wao wale na kuvimbiwa na kusaza.

Sh. Bil 80 zikiingizwa kwenye ununuzi wa nafaka kunauwezekano wa Kununua Elfu 80 za mahindi na kuingizwa kwenye maghala ya serikali na kuuzwa Kwa Bei nusu ili serikali irudishe nusu ya gharama. Ambapo serikali ingerudisha bil. 40.
Hii inafanywa makusudi ili kupunguza makali ya maisha Kwa wananchi ambao vipato vyao ni vidogo huku wakiwa wanaishi na Vijana wao ambao wamekosa ajira.
 
Wadau katika kuongea na mdau serikalini ngazi za juu kanitonya kuwa gharama iliyotumia katika kampeni ya kumpongeza Samia inakadiliww kufikia sh Billion 80Tz. Hizi ni Gharama za posho za vikao vya kamati mbalimbali kuanzia ngazi ya serikali na chama Kwenye kata, wilaya, mkoa na Taifa.

Gharama za vyombo vya habari, machapisho, mabango etc. Huyu mtu Yuko ofisi ya TAKUKURU. Kanitonya hivyo ni kwa mjibu wa riport walizozikusanya na bado wanaendele kuzifanyia KAZI.

Kwa kifupi kila sherehe unayoona ni upigaji ndo agenda iliyo nyuma yake. Je, ni fair kutumia billion 80 Kwenye sherehe ya kumpongeza wakati shule za msingi hazina hata vyoo vya maana?
Bango moja ni shs. milioni 12! Waongeze tozo kufidia hizo, ila watanzania tujue wanaccm ndio wanaoihujumu nchi na ndio kwa hivi sasa matajiri wakubwa ambao hawajawahi kufanya biashara na ndio wanaoporomosha maghorofa vichochoroni na ni wamiliki wa malori na mabasi.
 
Haya mambo ya kupongeza pongeza hua ni ya ajabu sana. Kwanini asipongezwe na wanachama ndani ya chama chake kwa ghalama za chama!! Mana wako ndo wa kutakiwa kumpongeza kwa kuwakilisha chama chao vizuri sio serikali kwa sababu serikalini anawajibika na sio kwamba anatoa msaada. Mama namkubali ila kuna mambo kama haya namwona nae anafeli
 
Wewe Ni muongo tu na mbabaishaji tu ndio maana hata uandishi wako Ni wa kibabaishaji tu haueleweki Wala kusomeka vizuri.

Rais Samia hahitaji kuundiwa kamati za kulipwa Hadi posho kwa ajili ya kumpongeza,kwa kuwa kazi zake zinaonekana machoni mwa kila mtanzania mwenye uwezo wa kuona na asiye na matatizo ya macho.

Rais Samia na serikali yake kajenga miradi mbalimbali kila Kona ya nchi hii inayoonekana na kuwanufaisha watanzania,Nani asiyeona vituo mbalimbali vya Afya hapa nchini ,Nani asiyeona vyumba vya madarasa vikipendeza,Nani asiyeona hayo? Kwani hayo yanamhitaji kamati? Kwani watanzania Ni vipofu Hadi wasione?

Nani asiyefahamu juhudi za mh Rais kuwasaidia na kuwainua kiuchumi wakulima? Nani hafahamu juu ya utolewaji wa Ruzuku ya billion Mia moja hamsini katika mbolea iliyopelekea kushuka kwa Bei ya mbolea sokoni mfano mbolea ya DAP msimu uliopita ilikuwa inauzwa shillingi laki moja na 40 lakini msimu huu inapatikana kwa Elfu 70 tu?

Nani hafahamu namna mh Rais alivyowabebea mzigo wa gharama za maisha kwa kutoa Ruzuku ya billion Mia moja kila mwezi katika mafuta na hivyo kupelekea kushuka kwa Bei kwa bidhàa mbalimbali? Au hujuwi mafuta Ni injini ya uchumi?

Mtanzania yupi hatambui kazi kubwa na ya kutukuka iliyofanywa na mh Rais katika kuvutia wawekezaji,watalii pamoja na wafanyabiashara hasa baada ya wazo lake la kuitangaza nchi yetu na vivutio vyake kupitia Royal Tour?

Rais Samia Ni chaguo la watanzania Kuendelea kututumikia na kuwaongoza katika muhula wa pili,ndio kiu Yao Watanzania na kwa sauti za pamoja watanzania wameamua kwenda na Rais Samia na kuiomba kwa magoti na unyenyekevu CCM iwaletee mama Samia Uchaguzi Ujao.

Katika Uongozi Wa Rais Samia huwezi ukabaki salama wala kusalimika ukibainika Kuchezea pesa za umma,huwezi ukapona Wala kupata njia ya kuukwep mkono wa Sheria ,Ni lazima ukione Cha Moto,Ni lazima upitishwe njia ya majonzi,maumivu, uchungu na majuto kisheria. Rais Samia Hana Subira katika Hilo la mtu yeyote yule juu ya pesa za umma
We ni mpumbavu plus
 
Wadau katika kuongea na mdau serikalini ngazi za juu kanitonya kuwa gharama iliyotumia katika kampeni ya kumpongeza Samia inakadiliww kufikia sh Billion 80Tz. Hizi ni Gharama za posho za vikao vya kamati mbalimbali kuanzia ngazi ya serikali na chama Kwenye kata, wilaya, mkoa na Taifa.

Gharama za vyombo vya habari, machapisho, mabango etc. Huyu mtu Yuko ofisi ya TAKUKURU. Kanitonya hivyo ni kwa mjibu wa riport walizozikusanya na bado wanaendele kuzifanyia KAZI.

Kwa kifupi kila sherehe unayoona ni upigaji ndo agenda iliyo nyuma yake. Je, ni fair kutumia billion 80 Kwenye sherehe ya kumpongeza wakati shule za msingi hazina hata vyoo vya maana?
Uongo sana huo

USSR
 
Wanampongeza kwa kazi gani aliyofanya; ya kushangilia uhujumu wa mashirika ya umma?
 
Ndio jinsi pesa inavyoingia kwenye mzunguko hivyo 😃 wataalam wa uchumi wanasema inaleta kitu inaitwa multiplier effect
Ana roho ya kujinyima inamtesa. Kifo cha Yesu ni kwamba Yuda alipokea pesa za watu ndio akaweza kukamatwa na kuuawa.

Huwezi kukwepa kutumia pesa kama unaitaka pesa.
 
Kwanza jifunze kuandika vizuri kiswahili, pili huyo "mtu wa juu serikalini aliye takukuru" alikuwa anakueleza ili iweje ? Je angekwambia ilitumika bil 300 ? Tatu, azimio la kumpongeza Samia ni la bunge, tangu lini bunge likatumia bil 80 kwa siku ?
Kaleta umbeya kama alivyoupokea huko mtaani.
 
Ukipata na wewe piga tu.Watumishi wa umma hawafungwi wakiisababishia hasara serikali,kinachofanyika ni kuhamishwa kituo Cha kazi au kupelekwa makao makuu kusoma magazeti.
 
Wadau katika kuongea na mdau serikalini ngazi za juu kanitonya kuwa gharama iliyotumia katika kampeni ya kumpongeza Samia inakadiliww kufikia sh Billion 80Tz. Hizi ni Gharama za posho za vikao vya kamati mbalimbali kuanzia ngazi ya serikali na chama Kwenye kata, wilaya, mkoa na Taifa.

Gharama za vyombo vya habari, machapisho, mabango etc. Huyu mtu Yuko ofisi ya TAKUKURU. Kanitonya hivyo ni kwa mjibu wa riport walizozikusanya na bado wanaendele kuzifanyia KAZI.

Kwa kifupi kila sherehe unayoona ni upigaji ndo agenda iliyo nyuma yake. Je, ni fair kutumia billion 80 Kwenye sherehe ya kumpongeza wakati shule za msingi hazina hata vyoo vya maana?
Hizi hesabu za billioni 80 umezotoa wapi..unaijua billion 80 mkuu?
 
Umekalia majungu tu, unahisi kila mahali ni vijiwe vya kahawa. Ukiambiwa utoe ushahidi wa hiyo bilioni 80 utaweza?

Eti mtu mkubwa takukuru, unahisi kila mtu pimbi umdanganye kindezi

Fanya kazi acha ujinga
Well said!
 
Wadau katika kuongea na mdau serikalini ngazi za juu kanitonya kuwa gharama iliyotumia katika kampeni ya kumpongeza Samia inakadiliww kufikia sh Billion 80Tz. Hizi ni Gharama za posho za vikao vya kamati mbalimbali kuanzia ngazi ya serikali na chama Kwenye kata, wilaya, mkoa na Taifa.

Gharama za vyombo vya habari, machapisho, mabango etc. Huyu mtu Yuko ofisi ya TAKUKURU. Kanitonya hivyo ni kwa mjibu wa riport walizozikusanya na bado wanaendele kuzifanyia KAZI.

Kwa kifupi kila sherehe unayoona ni upigaji ndo agenda iliyo nyuma yake. Je, ni fair kutumia billion 80 Kwenye sherehe ya kumpongeza wakati shule za msingi hazina hata vyoo vya maana?
Takukuru wanasemaje?
 
Back
Top Bottom