Wewe Ni muongo tu na mbabaishaji tu ndio maana hata uandishi wako Ni wa kibabaishaji tu haueleweki Wala kusomeka vizuri.
Rais Samia hahitaji kuundiwa kamati za kulipwa Hadi posho kwa ajili ya kumpongeza,kwa kuwa kazi zake zinaonekana machoni mwa kila mtanzania mwenye uwezo wa kuona na asiye na matatizo ya macho.
Rais Samia na serikali yake kajenga miradi mbalimbali kila Kona ya nchi hii inayoonekana na kuwanufaisha watanzania,Nani asiyeona vituo mbalimbali vya Afya hapa nchini ,Nani asiyeona vyumba vya madarasa vikipendeza,Nani asiyeona hayo? Kwani hayo yanamhitaji kamati? Kwani watanzania Ni vipofu Hadi wasione?
Nani asiyefahamu juhudi za mh Rais kuwasaidia na kuwainua kiuchumi wakulima? Nani hafahamu juu ya utolewaji wa Ruzuku ya billion Mia moja hamsini katika mbolea iliyopelekea kushuka kwa Bei ya mbolea sokoni mfano mbolea ya DAP msimu uliopita ilikuwa inauzwa shillingi laki moja na 40 lakini msimu huu inapatikana kwa Elfu 70 tu?
Nani hafahamu namna mh Rais alivyowabebea mzigo wa gharama za maisha kwa kutoa Ruzuku ya billion Mia moja kila mwezi katika mafuta na hivyo kupelekea kushuka kwa Bei kwa bidhàa mbalimbali? Au hujuwi mafuta Ni injini ya uchumi?
Mtanzania yupi hatambui kazi kubwa na ya kutukuka iliyofanywa na mh Rais katika kuvutia wawekezaji,watalii pamoja na wafanyabiashara hasa baada ya wazo lake la kuitangaza nchi yetu na vivutio vyake kupitia Royal Tour?
Rais Samia Ni chaguo la watanzania Kuendelea kututumikia na kuwaongoza katika muhula wa pili,ndio kiu Yao Watanzania na kwa sauti za pamoja watanzania wameamua kwenda na Rais Samia na kuiomba kwa magoti na unyenyekevu CCM iwaletee mama Samia Uchaguzi Ujao.
Katika Uongozi Wa Rais Samia huwezi ukabaki salama wala kusalimika ukibainika Kuchezea pesa za umma,huwezi ukapona Wala kupata njia ya kuukwep mkono wa Sheria ,Ni lazima ukione Cha Moto,Ni lazima upitishwe njia ya majonzi,maumivu, uchungu na majuto kisheria. Rais Samia Hana Subira katika Hilo la mtu yeyote yule juu ya pesa za umma