Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 34,256
- 44,597
Kampeni ya No Reforms No Elections (No-No Campaign) imeanza kupamba moto. Maneno yake yanasikika vizuri masikioni mwa Watanzania na Watanzania wengi hasa mitandaoni wamekuwa wakirudia kauli hii kuonesha kuunga kwao mkono harakati za mabadiliko nchini.
Kauli hii si ngeni katika eneo letu la Afrika ya Mashariki. Imetumiwa na Kiiza Besigye kule Uganda miaka kumi hivi iliyopita na miaka kama nane nyuma ilitumiwa na Raila Odinga na ushirika wa NASA kule Kenya. Chadema wameicopy na kuipaste wakitumaini kuwa inaweza kuleta mafanikio katika kuilazimisha CCM ilete mabadiliko ambayo yatafanya iwe rahisi kwa vyama vya upinzani kuiondoa madarakani.
Katika onesho hili la leo podcast nazungumzia mantiki na uwezekano wa kampeni hii kufanikiwa na kama katika hali iliyopo sasa CHADEMA Kampeni ya No-No inaweza kufanikiwa au kunahitajika mkakati mwingine bora zaidi isije ikawa ni kampeni ambayo mwisho wake ni kwenye keyboard za komputa na za simu.
View: https://youtu.be/cyGnk6oC0Pg