PreGE2025 Kampeni ya No Reforms No Election (No-No Campaign) ni Mtego Usionasa? CHADEMA Matatani

PreGE2025 Kampeni ya No Reforms No Election (No-No Campaign) ni Mtego Usionasa? CHADEMA Matatani

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
I also sai this again and again lakini watu hawaelewi..

Kwanza movement ya NO REFORMS NO ELECTION iko fire 🔥 🔥 and is working very properly and effectively..

Mzee Mwanakijiji asichojua (labda), kama ni watu kutopiga kura, hawataanza mwaka huu (2025)...

Watu walishaacha kwenda kupiga kura miaka mingi, and actually, sana sana ni tangu mwaka 2020 baada ya upuuzi wa Magufuli wa mwaka 2019 kufuta wagombea wa vyama vingine vyote na kuacha wa CCM pekee yao halafu baadaye CCM kama mazuzu vile yanashangilia kuwa yameshinda kwa 99.99%...

From there, watu wakaona kabisa, kuwa, kumbe Kuna maana gani kuacha shughuli zako kwenda kupanga foleni na kupigwa jua au baridi eti Ili kupiga kura wakati utakayemchagua wala hatapewa kura yako, atatangazwa ambaye hajashinda...?

Watu walishaona tangu wakati huo kuwa, kura zao hazina maana tena, hazina thamani tena, kwa kuwa hazihesabiwi wala kuhesabika kwa kiongozi aliyepata kura nyingi...

Mwaka Jana 2024 katika uchaguzi wa vijiji na Mitaa, ndugu yangu mmoja (mwalimu) alikuwa msimamizi wa kituo kimoja cha kupigia kura ktk manispaa ya Shinyanga. Alisema, mpaka saa 12jioni wanafunga kituo, ni wapiga kura 20 tu ndio walifika na kupiga kura kwenye kituo chao kati ya orodha ya wapiga kura 230+ wa kituo kile. Anasema, hata wao walishangaa sana...!

Msimamizi wa eneo lile (Mtendaji wa Mtaa), baada kufika na kukuta hali ile, akawasiliana na walio juu yake, yakaja maelekezo kuwa wasimamizi wapige kura zilizosalia zote kwa idadi ya wapiga kura ktk kituo kile wao kwa mgombea wa CCM. Na ikawa hivyo, mchezo ukaishia hapo...


Sasa huo👆👆 ndio uhuni unaofanywa na serikali na CCM everywhere na karibu kila uchaguzi. Na ndio maana ya figisifigusu za mawakala (polling agents) wa vyama vya upinzani kuwekewa unnecessary vikwazo ili mradi tu wasitokee kwenye vituo vya kupigia kura na kuwa kikwazo kwa CCM ku - execute plan zao za wizi wa kura....

Watu walishasusaga kwenda kupiga kura kitambo hata kabla ya NO REFORMS NO ELECTION kuanza...!!


Ndio maana, movement hii ya NO REFORMS NO ELECTION ilivyoanza tu, imepokelewa kwa shauku na kwa hamasa kubwa na wananchi kwa sbb wamechoka na hawapendi haki yao kudhulumuwa. Wanataka waongozwe na viongozi waliomchagua wao kwa utashi wao, sio hawa waliowekwa tu kinguvu au kwa kuiba kura....

Na hii imeitisha CCM na serikali yao yote kupita kawaida. Ndio maana ya mambo haya ya hovyo yanayoendelea sasa hapa nchini ya kuteka, kupiga, kupoteza na kuua watu hovyo; kugombana na watumishi wa Mungu na makanisa kwa kisingizio cha "kuhubiri siasa". Hii yote ni ktk kujaribu kuzima moto wa gesi kwa mchanga...

Inawezekana kabisa uchaguzi wa mwaka huu 2025 ukafamyika kibabe hivyo hivyo. Lakini, hautakuwa uchaguzi bali maigizo ya uchaguzi yaliyo wazi sana. Na kwa maana hakuna watu wenye akili duniani watautambua...!

Lakini ukiacha ushabiki na ukada au uchawa, hekima inasema wazi kuwa kuna possibility kubwa zaidi ya KUTOFANYIKA UCHAGUZI MWAKA HUU 2025. TUTAU - PUSH MBELE kwa utaratibu wa kikatiba unaruhusu....

Na hili mimi niko very optimistic kwa 95%. Na maana yake ni kuruhusu twende kwanza kwenye dialogue itakayotupeleka kwenye minimal all major reforms of our electoral system...

Iko wazi kuwa CCM na serikali yao wanataka hili kwa sababu wanajua wataendelea kuwa madarakani for 1 or 2 more years. You just wait and see this to happen. It's just a matter of time watatoka na ku - admit hili...

We all understand that, they're in a very big fear to accept these proposed changes kwa sbb yanawaondolea advantage ya kutumia mfumo dhaifu wa uchaguzi uliokuwa unawapendelea kubaki madarakani. Wanaogopa mabadiliko. Wengine wanaogopa jela pia kwa sbb ya dhambi zao nyekundu mno walizozitenda kwa nchi na taifa hili....

The fear of changes embroiding them puts CCM in a big dilemma of making right decisions. But they don't have any option, they have to take this whether they like it or not...

Ndio maana kwa sasa wanakomaa hivyo hivyo huko wakijua wanaenda shimoni kutumbukia...!!
Kongole sana ndugu.
Umeandika yote na ya ziada.
Asiye elewa mchango huu, huyo hata waje malaika hataweza kuelewa tena.
Huu ndio ukweli.
 
Huu ni uongo wa wazi.
Ukiandika kuwa watu wengi wanakula na kujaza mifuko na matumbo yao kwa hisani (Hispanic) ya CCM, unaandika uongo wa mchana jua kali.

Wanaonufaika na CCM ni kakikundi ka watu wachache sana.

Katibu wa CCM (W) watoto wake wawili ni wahitimu wa shahada mwaka wa 4 huu hawana ajira, kawafungulia "kiwanda" cha uchapaji kwenye nguo na kutengeneza mabango, lakini hata tenda ya kuchapisha t shirts na mabango ya mbunge wa wilayani kwake yamechapishwa na Wachina.
Ahsante sana kwa mfano halisi kama huu ulioutoa hapa.. CCM ni dubwasha kubwa ; ukilitazama kwa akili ya kizamani linatisha sana; lakini ukweli ni kwamba dubwasha hilo sasa hivi limejaa matobo mengi sana.

Kukitokea nguvu ya kulikandamiza kwa nje linaporomoka na kusambaratika lote.
 
Ahsante sana kwa mfano halisi kama huu ulioutoa hapa.. CCM ni dubwasha kubwa ; ukilitazama kwa akili ya kizamani linatisha sana; lakini ukweli ni kwamba dubwasha hilo sasa hivi limejaa matobo mengi sana.

Kukitokea nguvu ya kulikandamiza kwa nje linaporomoka na kusambaratika lote.
Nilimuonyesha video ya Wachina waki print tshirts za CCM, alisikitika sana.
Eti ananiomba niwaunganishie vijana wake kazi za kuprint kwa wale wanaogombea kwa kuwa ninajuana na watia nia wengi, nikamwambia kila mtu ale kwa urefu wa kamba yake kama alivyosema mwenyekiti wao.
 
Tofauti ya sasa ni kwamba Watanzania hawako tu online ,, wako tayari offline pia.

Usidharau nguvu ya kizazi kinachosema hatupigi kura bila mabadiliko ,hiki si kizazi cha kungoja miujiza, ni kizazi cha kusababisha mabadiliko.
Hakika .

Nilieleza pia humu hawa vijana sio zama za 1970 zidumu fikra za mwenyekiti wao waitikie zidumu!

Kwa yanayoendelea basi hawa vijana wataawacha watu uchi na hawatoamini wanachokiona.

Ni kizazi "ungovernable" uthubutu nilijua wanao ila wamefanya zaidi ya uthubutu.
 
Kampeni ya No Reforms No Elections (No-No Campaign) imeanza kupamba moto. Maneno yake yanasikika vizuri masikioni mwa Watanzania na Watanzania wengi hasa mitandaoni wamekuwa wakirudia kauli hii kuonesha kuunga kwao mkono harakati za mabadiliko nchini.

Kauli hii si ngeni katika eneo letu la Afrika ya Mashariki. Imetumiwa na Kiiza Besigye kule Uganda miaka kumi hivi iliyopita na miaka kama nane nyuma ilitumiwa na Raila Odinga na ushirika wa NASA kule Kenya. Chadema wameicopy na kuipaste wakitumaini kuwa inaweza kuleta mafanikio katika kuilazimisha CCM ilete mabadiliko ambayo yatafanya iwe rahisi kwa vyama vya upinzani kuiondoa madarakani.

Katika onesho hili la leo podcast nazungumzia mantiki na uwezekano wa kampeni hii kufanikiwa na kama katika hali iliyopo sasa CHADEMA Kampeni ya No-No inaweza kufanikiwa au kunahitajika mkakati mwingine bora zaidi isije ikawa ni kampeni ambayo mwisho wake ni kwenye keyboard za komputa na za simu.


View: https://youtu.be/cyGnk6oC0Pg

sasa mtego wao wa NRNE umenasa... yule mwamba huwa akisimamia jambo lake, lazima ashinde.. siku zote ushindi wake huwa ni figusu figusu tangu akiwa TLS, akaja CDM na sasa nchi imelipuka kwa msimamo wake usio yumba.
 
Back
Top Bottom