PreGE2025 Kampeni ya No Reforms No Election (No-No Campaign) ni Mtego Usionasa? CHADEMA Matatani

PreGE2025 Kampeni ya No Reforms No Election (No-No Campaign) ni Mtego Usionasa? CHADEMA Matatani

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Tofauti ya sasa ni kwamba Watanzania hawako tu online ,, wako tayari offline pia.

Usidharau nguvu ya kizazi kinachosema hatupigi kura bila mabadiliko ,hiki si kizazi cha kungoja miujiza, ni kizazi cha kusababisha mabadiliko.
Wazee wanajisahau wamekuza nyoka
 
Kwa kutotaka kupoteza muda juu ya jambo hili kukufafanulia tofauti zilizopo kwa sasa...; NARC Kenya hawakufanikiwa kukomesha utawala wa KANU chini ya Moi?
Au wewe unatafuta mafanikio gani?
Sijazungumzia NARC nimezungumzia NASA
 
Hii campaign ilifaaa nchi kama Kenya ambapo watu wana akili,sio kwa matahira sisi ya kitanzania.
Labda kama ni long term plan.
Kwani Kenya ilifaulu?

Kwa uganda ilifaulu

Hadi sasa sijaona ujanja wa Kenya …. Apart from online drama and a few on the field drama kama ile ya mwangi
 
Sasa hapa tunalo la kujadili zaidi, mkuu, Mwanakijiji?
Ni kuwa NoNo kampeni ya Chadema iko kwenye matatizo...yaani wajitahidi kweli uchaguzi usifanyike au uvurugike. Kwa mfano siku ya uchaguzi wanachadema wazuie watu kwenda kupiga kura kiasi cha kupunguza sana idadi ya wapiga kura...lakini pamoja na kampeni yote wasipofanikiwa je?
 
Hiyo kampeni ilianza wakati vijana wa chuo wamepata Hela ya kujikimu ya boom...Sasa ni wiki ya pili Hela wana anza kuhesabia mfukoni...hawawezi kuweka bundle ya internet kila siku... Ndio maana imekuwa kimya Sasa nguvu imepungua.
 
Ni kuwa NoNo kampeni ya Chadema iko kwenye matatizo...yaani wajitahidi kweli uchaguzi usifanyike au uvurugike. Kwa mfano siku ya uchaguzi wanachadema wazuie watu kwenda kupiga kura kiasi cha kupunguza sana idadi ya wapiga kura...lakini pamoja na kampeni yote wasipofanikiwa je?
hayo ya kutofanikiwa yaache yalale hivyo hivyo, siyo hitaji la sasa.
Na wewe unapohitimisha ya kwamba "kampeni ya chadema ipo kwenye matatizo", hili umelifanyia kazi wapi ili utuonyeshe ushahidi wa matatizo hayo?

Kitakachotokea Oktoba, ndiyo kazi inayofanyika sasa hivi. Hakuna popote waliposema njia zipi zitatumika kuzuia uchaguzi huo. Inakulazimu pia uelewe kwamba siyo CHADEMA watakaozuia uchaguzi usifanyike.

Kiujumla sioni mahali popote penye hoja katika andiko lako hapo juu; mbali ya yale yale ya siku zote ya kuishangilia CCM; ambalo sasa hivi ni dubwasha linalotumiwa tu na Samia na Genge lake.
 
Kampeni ya No Reforms No Elections (No-No Campaign) imeanza kupamba moto. Maneno yake yanasikika vizuri masikioni mwa Watanzania na Watanzania wengi hasa mitandaoni wamekuwa wakirudia kauli hii kuonesha kuunga kwao mkono harakati za mabadiliko nchini.

Kauli hii si ngeni katika eneo letu la Afrika ya Mashariki. Imetumiwa na Kiiza Besigye kule Uganda miaka kumi hivi iliyopita na miaka kama nane nyuma ilitumiwa na Raila Odinga na ushirika wa NASA kule Kenya. Chadema wameicopy na kuipaste wakitumaini kuwa inaweza kuleta mafanikio katika kuilazimisha CCM ilete mabadiliko ambayo yatafanya iwe rahisi kwa vyama vya upinzani kuiondoa madarakani.

Katika onesho hili la leo podcast nazungumzia mantiki na uwezekano wa kampeni hii kufanikiwa na kama katika hali iliyopo sasa CHADEMA Kampeni ya No-No inaweza kufanikiwa au kunahitajika mkakati mwingine bora zaidi isije ikawa ni kampeni ambayo mwisho wake ni kwenye keyboard za komputa na za simu.


View: https://youtu.be/cyGnk6oC0Pg


Tanzania kutokukubali pesa maana yake ni chaguzi huru?
 
Tofauti ya sasa ni kwamba Watanzania hawako tu online ,, wako tayari offline pia.

Usidharau nguvu ya kizazi kinachosema hatupigi kura bila mabadiliko ,hiki si kizazi cha kungoja miujiza, ni kizazi cha kusababisha mabadiliko.

GOOD JOKE
 
Bado unaamini CCM inao uhai wa miaka madarakani hadi CHADEMA wapoteze muda wa kwenda kutafuta dawa huko kwingine?
Oktoba kama Samia na Genge watalazimisha kubaki madarakani huo utakuwa ndio mwisho wao. Samia hawezi tena kupata miaka mitano ya kuivuruga nchi. Atakuwa amebaki madarakani kwa nguvu, na ni halali kuondolewa madarakani kwa nguvu.
I also sai this again and again lakini watu hawaelewi..

Kwanza movement ya NO REFORMS NO ELECTION iko fire 🔥 🔥 and is working very properly and effectively..

Mzee Mwanakijiji asichojua (labda), kama ni watu kutopiga kura, hawataanza mwaka huu (2025)...

Watu walishaacha kwenda kupiga kura miaka mingi, and actually, sana sana ni tangu mwaka 2020 baada ya upuuzi wa Magufuli wa mwaka 2019 kufuta wagombea wa vyama vingine vyote na kuacha wa CCM pekee yao halafu baadaye CCM kama mazuzu vile yanashangilia kuwa yameshinda kwa 99.99%...

From there, watu wakaona kabisa, kuwa, kumbe Kuna maana gani kuacha shughuli zako kwenda kupanga foleni na kupigwa jua au baridi eti Ili kupiga kura wakati utakayemchagua wala hatapewa kura yako, atatangazwa ambaye hajashinda...?

Watu walishaona tangu wakati huo kuwa, kura zao hazina maana tena, hazina thamani tena, kwa kuwa hazihesabiwi wala kuhesabika kwa kiongozi aliyepata kura nyingi...

Mwaka Jana 2024 katika uchaguzi wa vijiji na Mitaa, ndugu yangu mmoja (mwalimu) alikuwa msimamizi wa kituo kimoja cha kupigia kura ktk manispaa ya Shinyanga. Alisema, mpaka saa 12jioni wanafunga kituo, ni wapiga kura 20 tu ndio walifika na kupiga kura kwenye kituo chao kati ya orodha ya wapiga kura 230+ wa kituo kile. Anasema, hata wao walishangaa sana...!

Msimamizi wa eneo lile (Mtendaji wa Mtaa), baada kufika na kukuta hali ile, akawasiliana na walio juu yake, yakaja maelekezo kuwa wasimamizi wapige kura zilizosalia zote kwa idadi ya wapiga kura ktk kituo kile wao kwa mgombea wa CCM. Na ikawa hivyo, mchezo ukaishia hapo...


Sasa huo👆👆 ndio uhuni unaofanywa na serikali na CCM everywhere na karibu kila uchaguzi. Na ndio maana ya figisifigusu za mawakala (polling agents) wa vyama vya upinzani kuwekewa unnecessary vikwazo ili mradi tu wasitokee kwenye vituo vya kupigia kura na kuwa kikwazo kwa CCM ku - execute plan zao za wizi wa kura....

Watu walishasusaga kwenda kupiga kura kitambo hata kabla ya NO REFORMS NO ELECTION kuanza...!!


Ndio maana, movement hii ya NO REFORMS NO ELECTION ilivyoanza tu, imepokelewa kwa shauku na kwa hamasa kubwa na wananchi kwa sbb wamechoka na hawapendi haki yao kudhulumuwa. Wanataka waongozwe na viongozi waliomchagua wao kwa utashi wao, sio hawa waliowekwa tu kinguvu au kwa kuiba kura....

Na hii imeitisha CCM na serikali yao yote kupita kawaida. Ndio maana ya mambo haya ya hovyo yanayoendelea sasa hapa nchini ya kuteka, kupiga, kupoteza na kuua watu hovyo; kugombana na watumishi wa Mungu na makanisa kwa kisingizio cha "kuhubiri siasa". Hii yote ni ktk kujaribu kuzima moto wa gesi kwa mchanga...

Inawezekana kabisa uchaguzi wa mwaka huu 2025 ukafamyika kibabe hivyo hivyo. Lakini, hautakuwa uchaguzi bali maigizo ya uchaguzi yaliyo wazi sana. Na kwa maana hakuna watu wenye akili duniani watautambua...!

Lakini ukiacha ushabiki na ukada au uchawa, hekima inasema wazi kuwa kuna possibility kubwa zaidi ya KUTOFANYIKA UCHAGUZI MWAKA HUU 2025. TUTAU - PUSH MBELE kwa utaratibu wa kikatiba unaruhusu....

Na hili mimi niko very optimistic kwa 95%. Na maana yake ni kuruhusu twende kwanza kwenye dialogue itakayotupeleka kwenye minimal all major reforms of our electoral system...

Iko wazi kuwa CCM na serikali yao wanataka hili kwa sababu wanajua wataendelea kuwa madarakani for 1 or 2 more years. You just wait and see this to happen. It's just a matter of time watatoka na ku - admit hili...

We all understand that, they're in a very big fear to accept these proposed changes kwa sbb yanawaondolea advantage ya kutumia mfumo dhaifu wa uchaguzi uliokuwa unawapendelea kubaki madarakani. Wanaogopa mabadiliko. Wengine wanaogopa jela pia kwa sbb ya dhambi zao nyekundu mno walizozitenda kwa nchi na taifa hili....

The fear of changes embroiding them puts CCM in a big dilemma of making right decisions. But they don't have any option, they have to take this whether they like it or not...

Ndio maana kwa sasa wanakomaa hivyo hivyo huko wakijua wanaenda shimoni kutumbukia...!!
 
Inawezekana kabisa uchaguzi wa mwaka huu 2025 ukafamyika kibabe hivyo hivyo. Lakini, hautakuwa uchaguzi bali maigizo ya uchaguzi yaliyo wazi sana. Na kwa maana hakuna watu wenye akili duniani watautambua...!
Panahitajika pawepo na 'pushback' safari hii. Wasiachiwe tu CCM kujitangaza washindi bila ya wananchi kushiriki kwenye uchaguzi.
Hii 'pushback' ndiyo inayotakiwa itafutwe kwa umakini mkubwa, ili wakati utakapowadia ifanyiwe kazi.

Tunajuwa njia wanazotumia CCM; ni kuwatumia wenyeviti wa mitaa, vijiji na wengineo. Njia za kuwazuia hawa kushiriki kwenye uhalifu huo ndizo njia zinazoweza kubana mianya ya CCM kujitangazia ushindi ambao haukuwepo.

Ni wakati mwafaka kuzitafuta hizo njia sasa hivi.
 
Panahitajika pawepo na 'pushback' safari hii. Wasiachiwe tu CCM kujitangaza washindi bila ya wananchi kushiriki kwenye uchaguzi.
Hii 'pushback' ndiyo inayotakiwa itafutwe kwa umakini mkubwa, ili wakati utakapowadia ifanyiwe kazi.

Tunajuwa njia wanazotumia CCM; ni kuwatumia wenyeviti wa mitaa, vijiji na wengineo. Njia za kuwazuia hawa kushiriki kwenye uhalifu huo ndizo njia zinazoweza kubana mianya ya CCM kujitangazia ushindi ambao haukuwepo.

Ni wakati mwafaka kuzitafuta hizo njia sasa hivi.
Sisi ndio wananchi wenyewe, ndio wapiga kura. CHADEMA ni viongozi tu wa harakati za mabadiliko na wamefanikiwa kwa zaidi ya 95% kupata uungwaji mkono wa wananchi...

Tupendekeze njia za kutumia kuhakikisha kuwa hata kama watafanya uchaguzi kinguvu, lakini tuhakikishe kuwa uchaguzi huo na viongozi watakaopatikana na uchaguzi wasiwe na uhalali na wanuke kinyesi popote watakapokuwa...

#Ukiachilia njia hizi;

1. Kutokwenda kupiga kura (hili liko obvious, kwa kuwa 90% ya wapiga kura hawatakwenda kupiga kura kwenye uchaguzi ambao CCM tayari wameshjitangaza washindi). Experience ya chaguzi zilizopita zinathibitisha hili kuwa watu tangu 2020 hawapigi kura tena kwa sbb ya upuuzi huu

2. Kupaza sauti ktk Jumuiya za kimataifa kuwa, hakuna uchaguzi TZ bali ni maigizo tu. Hii itasaidia wahisani kutoleta pesa zao kwa serikali yenye viongozi wasio na ridhaa ya wananchi kwa sbb watazitumia kwa manufaa yao na sio ya wananchi..

#Njia gani zingine zitumike hususani kuwazuia wasitoe matokeo ya udanganyifu..?
 
#Njia gani zingine zitumike hususani kuwazuia wasitoe matokeo ya udanganyifu..?
Ni muhimu/NI LAZIMA, njia sahihi zipatikane kabla ya shughuli hiyo ya Oktoba. Na wasipewe fursa ya kujiandaa kupambana na mikakati hiyo.

Sasa hivi wanamshikilia Tundu Lissu kwa kutamka tu wananchi kuasi kushiriki upuuzi!

Mpango wa Kimataifa tayari umeanza kuwanyemelea : Tanzania tayari imeingizwa kwenye orodha ya nchi ambazo raia wake watapigwa marufuku kuingia Marekani, iwapo haitajirekebisha katika muda wa siku 60.

Sasa ngoja tuone watakavyo lichukulia hili.
 
Bado unaamini CCM inao uhai wa miaka madarakani hadi CHADEMA wapoteze muda wa kwenda kutafuta dawa huko kwingine?
Oktoba kama Samia na Genge watalazimisha kubaki madarakani huo utakuwa ndio mwisho wao. Samia hawezi tena kupata miaka mitano ya kuivuruga nchi. Atakuwa amebaki madarakani kwa nguvu, na ni halali kuondolewa madarakani kwa nguvu.
Kuna ujumbe mzito sana katikati ya hii mistari ndugu.
Naunga mkono na ndivyo itakavyokuwa.
 
Mkuu, Ninachosema ni kuwa ni makosa makubwa kwa NoNo campaigners kudhania kuwa sehemu kubwa ya Watanzania wapiga kura wnaichukia CCM. Watu wengi wanakula na kujaza mifuko na matumbo yao kwa Hispanic ya CCM
..hawa hawana ndoto ya kuona CCM nje ya utawala. Wataenda kutiki Oktoba...unafikiri CDM inanguvu kweli ya kuzuia uchaguzi usifanyike Oktoba?
Huu ni uongo wa wazi.
Ukiandika kuwa watu wengi wanakula na kujaza mifuko na matumbo yao kwa hisani (Hispanic) ya CCM, unaandika uongo wa mchana jua kali.

Wanaonufaika na CCM ni kakikundi ka watu wachache sana.

Katibu wa CCM (W) watoto wake wawili ni wahitimu wa shahada mwaka wa 4 huu hawana ajira, kawafungulia "kiwanda" cha uchapaji kwenye nguo na kutengeneza mabango, lakini hata tenda ya kuchapisha t shirts na mabango ya mbunge wa wilayani kwake yamechapishwa na Wachina.
 
Back
Top Bottom