4 7mbatizaji
JF-Expert Member
- Dec 8, 2019
- 11,613
- 13,543
Kampeni ya No Reforms No Elections (No-No Campaign) imeanza kupamba moto. Maneno yake yanasikika vizuri masikioni mwa Watanzania na Watanzania wengi hasa mitandaoni wamekuwa wakirudia kauli hii kuonesha kuunga kwao mkono harakati za mabadiliko nchini.
Kauli hii si ngeni katika eneo letu la Afrika ya Mashariki. Imetumiwa na Kiiza Besigye kule Uganda miaka kumi hivi iliyopita na miaka kama nane nyuma ilitumiwa na Raila Odinga na ushirika wa NASA kule Kenya. Chadema wameicopy na kuipaste wakitumaini kuwa inaweza kuleta mafanikio katika kuilazimisha CCM ilete mabadiliko ambayo yatafanya iwe rahisi kwa vyama vya upinzani kuiondoa madarakani.
Katika onesho hili la leo podcast nazungumzia mantiki na uwezekano wa kampeni hii kufanikiwa na kama katika hali iliyopo sasa CHADEMA Kampeni ya No-No inaweza kufanikiwa au kunahitajika mkakati mwingine bora zaidi isije ikawa ni kampeni ambayo mwisho wake ni kwenye keyboard za komputa na za simu.
View: https://youtu.be/cyGnk6oC0Pg
Mzee hupo ? Hujui dunia pamoja kwamba nakueshimu,
NR nE ilisha kuwa balaa, wale wanakimbizana na mali za chama ,sijui vile vibanda ,n.k wachukue vyote ,wananchi watafanya makubwa kuliko pitia chama chao, Chadema sio Cuf, wanachama wao kwanza wapo na uwezo binafsi , wakiamua jengo kubwa kuliko la sasa la makao makuu chadema , hivyo vigari, sijui viwanja ni ndani ya miezi sita tu ,wenye chama ambao ni wananchi wanakua wamekamilisha.
Siamini kama hili lipo na mkono wa Mbowe, ila kama upo mkono wake bado wanachama wanao uwezo wa kumjengea nyumba ya ghorofa kumi kuliko ile alijenga na kumpa bure, tusibabaishane hapa.
Ni maskini wa kutupa ambae unafikili mali za bure tena za taasisi , ili upate mgao ,na kwa lipi ?
Kuna watu wanaenda kupata laana ya milele asema Bwana , tutafute hela ,
Nyie mlio enda ishitaki chadema ili hali mmekua chamani ,nendeni tena mshitaki vichwa vya wanachama wa chadema maana chadema sio majengo bali wenye chama ,na mtalaaniwa vizazi vyenu vyote ,asema Bwana.
Chadema is on a point of no return, mwakesha bure.
Chukueni kila kitu mmuonacho kinawafaa , waachieni chadema ilivyo kw a wenye chama ambao ni wananchi , alafu tuone , upumbavu ni mzigo sana