PreGE2025 Kampeni ya No Reforms No Election (No-No Campaign) ni Mtego Usionasa? CHADEMA Matatani

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Mzee hupo ? Hujui dunia pamoja kwamba nakueshimu,

NR nE ilisha kuwa balaa, wale wanakimbizana na mali za chama ,sijui vile vibanda ,n.k wachukue vyote ,wananchi watafanya makubwa kuliko pitia chama chao, Chadema sio Cuf, wanachama wao kwanza wapo na uwezo binafsi , wakiamua jengo kubwa kuliko la sasa la makao makuu chadema , hivyo vigari, sijui viwanja ni ndani ya miezi sita tu ,wenye chama ambao ni wananchi wanakua wamekamilisha.

Siamini kama hili lipo na mkono wa Mbowe, ila kama upo mkono wake bado wanachama wanao uwezo wa kumjengea nyumba ya ghorofa kumi kuliko ile alijenga na kumpa bure, tusibabaishane hapa.

Ni maskini wa kutupa ambae unafikili mali za bure tena za taasisi , ili upate mgao ,na kwa lipi ?

Kuna watu wanaenda kupata laana ya milele asema Bwana , tutafute hela ,

Nyie mlio enda ishitaki chadema ili hali mmekua chamani ,nendeni tena mshitaki vichwa vya wanachama wa chadema maana chadema sio majengo bali wenye chama ,na mtalaaniwa vizazi vyenu vyote ,asema Bwana.

Chadema is on a point of no return, mwakesha bure.

Chukueni kila kitu mmuonacho kinawafaa , waachieni chadema ilivyo kw a wenye chama ambao ni wananchi , alafu tuone , upumbavu ni mzigo sana
 
Nimekuwa CHADEMA kwa miaka 20 Sasa. Tangu wakati huo mpaka Sasa hatujawahi kuwa na harakati (Movement) iliyoanzia kwa wananchi kama hii ya NO REFORMS NO ELECTION.

Watu wengi wanajisahaulisha kuwa ni wananchi wenyewe bila ya kushawishiwa na CHADEMA ndiyo baada ya uhuni uliofanyika kwenye uchaguzi wa mwaka 2019 na 2020 walisema kuwa hawatapiga kura kama kanuni na Sheria mbali mbali za kiuchaguzi hazitarekebishwa.

Na ushahidi ni uchaguzi wa mwaka 2024 wa Serikali za mitaa ambao ushiriki wa wananchi ulikuwa wa chini kabisa kwenye historia ya uchaguzi huo.

Kwa ivo nguvu ya NO REFORMS NO ELECTION haitokani na CHADEMA bali inatoka kwa wananchi wengi wa Tanzania waliopoteza Imani na mifumo ya kiuchaguzi ya nchi hii.

Kwa mtazamo wangu kaulimbiu ya NO REFORMS NO ELECTION inaweza kufifia, lakini wananchi wengi hawatakwenda kupiga kura kama mifumo ya kiuchaguzi haitabadilishwa na kuaminika Kwa wengi.

Moto huanza na cheche na mwanzo wa Ngoma ni lele!
 
EEEeeennHEEEEeeee!

Hii nayo ni nguvu ya hoja Mzee Mwanakijiji!
Hii mvua ilianza kukutandikia wapi mkuu, hadi kufika kwenye ngazi hii!
Mkuu, Ninachosema ni kuwa ni makosa makubwa kwa NoNo campaigners kudhania kuwa sehemu kubwa ya Watanzania wapiga kura wnaichukia CCM. Watu wengi wanakula na kujaza mifuko na matumbo yao kwa Hispanic ya CCM
..hawa hawana ndoto ya kuona CCM nje ya utawala. Wataenda kutiki Oktoba...unafikiri CDM inanguvu kweli ya kuzuia uchaguzi usifanyike Oktoba?
 
Mkuu utafanya kosa kubwa sana kudhania Samia yuko juu ya CCM....
 
Walichokuwa wanataka Kenya na Uganda na wanachotaka Tanzania vina tofauti gani?
 
Hii nr ne haiwezi fifia mpaka pale walioianzisha wakirudi kwa wananchi, wala sio ubabe wa ccm na kwambinu hizi nyepesi watumiazo kwamba itafifia bali wanazidi ipakaa mafuta ya kiupako
 
Hizi discusion niliziona tangu 2009 kule jukwaa la intelectuals, Mkandala akisema source za ndani zinasema Mbowe lazima aondoke, mara alimchefua kikwete na mambo meengi.

Lakini kama Serikali isingeingilia kati hili game lilikuwa linaenda kuisha CCM wakiwa wana hali mbaya, ila kwasababu tunazozijua wote kwamba CCM ndiyo Serikali na kinyume chake, ndiyo maana mnakuja huku kutunyea, lakini bila hivyo hata msingekuwa mnaelewa chadema wamefikaje mlango wa Ikulu bila trace.

Hili linakubalika sana kwa wananchi nahata ndani ya CCM na Serikali, kwasababu nyingi lakini kwa uchache, Mgombea wa CCM hakubaliki hata huko kwake, na Pili Wananchi wanashindwa kuielewa Serikali inajitamba na miradi miingi ikiwa wananchi wako hoi kimaisha.

Watu hawataki sera za kwenye ILANI, wanataka kuona HAKI, ikitendeka kila mahala, jambo ambalo CCM na serikali waliishalipoteza na hawajui walirudishe vipi.

Anyway mawazo ni mawazo, unayako na mi nina yangu.
 
Kama kampeni ya HATUCHEZI ya Simba na Yanga ambayo kimsingi ni madai ya REFORMS imepatiwa ufumbuzi na REFORMS zinaanza kufanyika...
Inashindikanaje kampeni ya NO REFORMS NO ELECTIONS kufanikiwa?

CHADEMA ni vehicle tu... wananchi wanazitaka REFORMS!

Serikali na ccm isiendelee kujidanganya Kwamba REFORMS kwenye soka ni muhimu zaidi ya REFORMS kwenye uchaguzi ambao ni mustakabali wa maendeleo ya taifa na maisha ya raia!

Wananchi na hasa vijana wanazitaka REFORMS vinginevyo chaguzi zitasusiwa!
Wakipuuzwa ipo siku Rais, mbunge ama diwani atachaguliwa na wananchi less than 10%!
 
Katika siku ambayo umejinjia heshima hapa ni leo. Yaani No Reforms No Election ni kwa ajili ya upinzani kutaka ishinde kirahisi uchaguzi? Unazeeka vibaya.
 
Mkuu mbona imenasa, naona umeamua kutumia fasihi kutoa kutoa hoja ili usijulikane kuegemea upande fulani. Sio mbaya kumlinda maslahi yako mzee wangu.
 
Katika siku ambayo umejinjia heshima hapa ni leo. Yaani No Reforms No Election ni kwa ajili ya upinzani kutaka ishinde kirahisi uchaguzi? Unazeeka vibaya.
Mkuu hujamuelewa, read between the line utamuelwa! Maboya yametumika mahala pake!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…