Kampuni inayojenga Uwanja wa ndege Chato, Mayanga Construction inamilikiwa na nani na ilipataje tenda hiyo?

Kampuni inayojenga Uwanja wa ndege Chato, Mayanga Construction inamilikiwa na nani na ilipataje tenda hiyo?

Ni ndoto kwamba eti kuna mtu mmoja ataweza kupamabana au kuthibiti rushwa na ufisadi Tanzania. Ufisadi wote nchini kwetu unafanywa ki-mfumo na ki-taasisi hivyo haiwezekani mtu mmoja afanye yanayotakiwa. Magufuli hawezi (natumai analijua hilo) na haitawezekana kwa mtu mmoja kufanya.

Lazima kama nchi tujenge taasisi na mifumo imara kwanza = Katiba Mpya. Lazima tuanze kwenye shina, kwenye msingi, na Katiba ndio mahali pekee sahihi pa kuanzia. Kisha tuje kwenye Sera, Sheria, Kanuni na elimu na mafunzo na mengineyo.

Kuna watu wanabeza umuhimu wa Katiba Mpya, wanasema hawaoni au hawajui umuhimu wake.Sasa ukweli ni kwamba ingawa Katiba Mpya si 100% solution to all problems in the land but it is the single major factor to bring about the desired solutions.
 
Kumbe ni kampuni ya MWANZA hapo sawa
Shilawadu wanasema huyo mayanga ni"bhageshi" wake baba jesca.
Wasukuma wanajua maana ya bhageshi.
Lakini Mimi naona hata kama ni jamaa take sio ishu ilimradi kama amepata tenda kwa njia ya haki maana kuwa ndugu au jamaa wa baba jesca sio kwamba hustahili kupata tenda za serikali
 
Ataa tender ilikuwa inaelekeza maalumu mjenzi atoke kanda ya ziwa .Yote hii ilikuwa makusudi
Umeona enh? Watu hawafahamu kwamba moja ya mambo ambayo ni abuse kwenye tenda ni kuweka conditions ambazo zina kila dalili ya kutaka ku-favor
 
Kama nitakuwa sahihi nadhani ilisajiliwa April 2016 kama class 1 contractor.

Kama ni hivyo, uzoefu wa project za ukubwa huo ilipata lini?!
No, ina muda kidogo, may be toka 2010 ipo.
 
Haijawahi kuwa dormant,,,itakua imepewa class 1 mwaka Jana or structure ya kampuni na wamiliki ilibadilishwa to the extent wakaona waisajili upya
Sasa unakataa nn kuwa haikusajiliwa mwaka jana? Sioni unachojaribu kujengea hoja hapa
 
Nyie bavicha acheni kupiga kelele. Mwambieni Mbowe amtumie huyo Manyanga sijui Mayanga kukarabati jengo la ufipa. Jamaa inaonekana ni mkandarasi mzuri tu.
 
Wadau, mimi hayo ndio maswali yangu na anaeweza kutoa majibu atusaidie na ikiwezekana atoe na nyaraka kusapoti majibu yake.

Kama ana document za kutangaza tender kama vile gazeti,n.k atuweke hapa na nyaraka zingine zote muhumu katika utangazaji na utoaji wa tender.

Nasikia hii kampuni ni ya wazawa(sijui ukweli wa hili jambo) ila kama ni kweli basi si vibaya tukawajua maana watakuwa wamesaidia fedha nyingi isiende nje ya nchi lakini ni lazima tujue kama sheria na taratibu zimezingatiwa katika kuwapatia tender hiyo.

Hata kama itakuwa ni kampuni ya kigeni nayo tungependa kujua namna ilivyopewa tender/kandarasi husika.

Ni hayo tu.
Sio lazima kila kitu kipitishwe na bunge acha unoko kwanza unalipa kodi shilingi ngapi
 
Nenda kaulize BRELA.
Kuuliza kwako kutachangia nchi kupata mapato.
Watanzania tu watu wa ajabu sana akijenga mzawa ooh kampuni ni ya nani...... Akijenga mzungu ooh sisi wazawa hatupewi tenda.
Kila siku mnaambiwa mjiunge mpate tenda ooh.... Kampuni hii ni yangu na familia yangu, mara fulani bhana si mtu mzuri kuungana naye utadhani kinachoungani kampuni ni tabia ya mtu kumbe ni matumizi ya nyaraka.

Na wakati mwingine mnadiliki kutokuungana eti kwa sababu tu fulani bhana ni kada wa chama fulani... hivyo kuungana naye kutatukosesha tenda.

Tuache kuchanganya siasa na kazi /utendaji hii haitatusaidia mfano mbona hatukuhoji/hatuhoji aliyejenga/anayejenga miundombinu ya barabara na maji mikoa ya kaskazini?
 
Wadau, mimi hayo ndio maswali yangu na anaeweza kutoa majibu atusaidie na ikiwezekana atoe na nyaraka kusapoti majibu yake.

Kama ana document za kutangaza tender kama vile gazeti,n.k atuweke hapa na nyaraka zingine zote muhumu katika utangazaji na utoaji wa tender.

Nasikia hii kampuni ni ya wazawa(sijui ukweli wa hili jambo) ila kama ni kweli basi si vibaya tukawajua maana watakuwa wamesaidia fedha nyingi isiende nje ya nchi lakini ni lazima tujue kama sheria na taratibu zimezingatiwa katika kuwapatia tender hiyo.

Hata kama itakuwa ni kampuni ya kigeni nayo tungependa kujua namna ilivyopewa tender/kandarasi husika.

Ni hayo tu.
Wakileta majibu na mimi nijulishe mkuu .

Hata hivyo nawaomba wadau wa JF ondoeni uoga tutajieni hii kampuni tuijue ili Tuisaidie serikali yetu isiyopenda Rushwa .

" HAPA KAZI TU "
 
Chini ya miaka kumi hiyo kampuni ilikuwa Class Seven kama sikosei, nahisi kupanda kwake hadi kufikia Class One leo ulikuwa ni mkakati maalum uliyoandaliwa kwa muda mrefu kwa msaada wa wizara ya ujenzi.

Hivyo kufikia leo wamepewa contract ya kujenja uwanja wa ndege sio ajabu sana kwani kila utawala huangaika kutafuta resources kwa ajili ya uchaguzi uliyo mbele yake.
 
Hii post ni ya kizalendo sana lakini unaweza kukuta mtu kama huyu anaanza kusakwa kwa uchochezi.
Pia kiasi cha billion zaidi ya 30 si kinapaswa kupitisha bungeni, ilikuwa hivyo!? Maendeleo ni yetu sote.
 
MAYANGA CONTRACTORS CO. LTD
Registration Number:
B1/154/04/2016
Managing Director:
STEPHEN MAKIGO
Types of Contractor:
BUILDING
Class:
1
Category:
Local
Town:
MWANZA
HideContacts
Postal Address:
P.O. BOX 10795
Physical Address:
PLOT NO.424, BLOCK A,MUSOMA ROAD,NYAMHONGOLO, MWANZA
E-mail:
stevenmakigo@yahoo.com
Phone:
+255 28 2561041/ 2560474/0754 301785
Source: http://www.crb.go.tz/mayanga-contractors
Aisee! Ngoja na mimi nisikate tamaa kumbe maisha yanaweza yakabadilika maana hakuna aijuaye kesho!
 
Sio lazima kila kitu kipitishwe na bunge acha unoko kwanza unalipa kodi shilingi ngapi
i
Rudi kwenye senses zako tafadhali. Matumizi yoyote ya fedha za serikali sharti yaidhinishwe na bunge kabla hazijaanza kutumika.

Pili, lazima uelewe kuwa kila moja analipa kodi, either directly or indirectly, hivyo ktk nchi yoyote ya kidemokrasia wana uhalali wa kuhoji namna zinavyotumiwa.

Mwisho, usiwadhihaki wenzako wanapohoji mambo waliyo na maslahi nayo kwani ni haki yao kisheria.
 
Wadau, mimi hayo ndio maswali yangu na anaeweza kutoa majibu atusaidie na ikiwezekana atoe na nyaraka kusapoti majibu yake.

Kama ana document za kutangaza tender kama vile gazeti,n.k atuweke hapa na nyaraka zingine zote muhumu katika utangazaji na utoaji wa tender.

Nasikia hii kampuni ni ya wazawa(sijui ukweli wa hili jambo) ila kama ni kweli basi si vibaya tukawajua maana watakuwa wamesaidia fedha nyingi isiende nje ya nchi lakini ni lazima tujue kama sheria na taratibu zimezingatiwa katika kuwapatia tender hiyo.

Hata kama itakuwa ni kampuni ya kigeni nayo tungependa kujua namna ilivyopewa tender/kandarasi husika.

Ni hayo tu.
Mkuu salary Slip Dk. Mashinji alipata kusema kuwa wananchi waamke maana kuna nyani/ngedere wanakula mashamba yao!!! na hayo ndiyo yanayoendelea kwa sasa! ufisadi, vita ya uchumi ni maneno ya kuwazuga wananchi ila ni hapohapo nyani/ngedere wanakula mpaka wake za watu!!!!!
 
Huu mradi wa airport nilisikia mwanzoni kuwa gharama yake ni bilioni 200. Sasa nashangaa komenti nyingine zinasema mradi huu gharama ni 41 bilion na wengine 39.15...

Ebu vijana wa chadema nipeni takwimu sahihi...
 
Wadau, mimi hayo ndio maswali yangu na anaeweza kutoa majibu atusaidie na ikiwezekana atoe na nyaraka kusapoti majibu yake.

Kama ana document za kutangaza tender kama vile gazeti,n.k atuweke hapa na nyaraka zingine zote muhumu katika utangazaji na utoaji wa tender.

Nasikia hii kampuni ni ya wazawa(sijui ukweli wa hili jambo) ila kama ni kweli basi si vibaya tukawajua maana watakuwa wamesaidia fedha nyingi isiende nje ya nchi lakini ni lazima tujue kama sheria na taratibu zimezingatiwa katika kuwapatia tender hiyo.

Hata kama itakuwa ni kampuni ya kigeni nayo tungependa kujua namna ilivyopewa tender/kandarasi husika.

Ni hayo tu.
Ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Chato: Serikali yatangaza tenda
Chato.jpg
 
Back
Top Bottom