Kampuni inayojenga Uwanja wa ndege Chato, Mayanga Construction inamilikiwa na nani na ilipataje tenda hiyo?

Kampuni inayojenga Uwanja wa ndege Chato, Mayanga Construction inamilikiwa na nani na ilipataje tenda hiyo?

sijaelewa kwamba imesajiliwa mwaka jana reg no au????
 
Wadau, mimi hayo ndio maswali yangu na anaeweza kutoa majibu atusaidie na ikiwezekana atoe na nyaraka kusapoti majibu yake.

Kama ana document za kutangaza tender kama vile gazeti,n.k atuweke hapa na nyaraka zingine zote muhumu katika utangazaji na utoaji wa tender.

Nasikia hii kampuni ni ya wazawa(sijui ukweli wa hili jambo) ila kama ni kweli basi si vibaya tukawajua maana watakuwa wamesaidia fedha nyingi isiende nje ya nchi lakini ni lazima tujue kama sheria na taratibu zimezingatiwa katika kuwapatia tender hiyo.

Hata kama itakuwa ni kampuni ya kigeni nayo tungependa kujua namna ilivyopewa tender/kandarasi husika.

Ni hayo tu.
Mkuu wewe unawashwa na nini?
Akijenga mzawa maneno hadi povu.
Wivu unawasumbua, jenga na wewe ingalau nyumba ysko ujijengee uwezo.
 
Ni kampuni ya mzawa na anauwezo wa kufanya hiyo kazi
 
Wadau, mimi hayo ndio maswali yangu na anaeweza kutoa majibu atusaidie na ikiwezekana atoe na nyaraka kusapoti majibu yake.

Kama ana document za kutangaza tender kama vile gazeti,n.k atuweke hapa na nyaraka zingine zote muhumu katika utangazaji na utoaji wa tender.

Nasikia hii kampuni ni ya wazawa(sijui ukweli wa hili jambo) ila kama ni kweli basi si vibaya tukawajua maana watakuwa wamesaidia fedha nyingi isiende nje ya nchi lakini ni lazima tujue kama sheria na taratibu zimezingatiwa katika kuwapatia tender hiyo.

Hata kama itakuwa ni kampuni ya kigeni nayo tungependa kujua namna ilivyopewa tender/kandarasi husika.

Ni hayo tu.
This is a good question and I support accountability.
 
Kabisa SE, jamaa anaziweka kama mapambo Ikulu zipigwe vumbi maana anajua ni madudu matupu kuhusu awamu hii.

Hizo ripoff za CAG zinakuja na hazifanyiwi chochote
 
Mkuu unajua amewahi kufanya kazi zipi nchini za ukandarasi? Hapa nataka kujua kama ana uzoefu au ndiyo mpigaji madili wa Ikulu kafanya yake.

Sina uhakika!

Hata hivyo, nilicho na uhakika nacho ni kwamba, Managing Director ni Stephen Makigo! Huyu Stephen Makigo aliwahi kuteuliwa na JPM kuwa Mjumbe wa TEMESA mwaka 2012! Kwa maana nyingine, kuna kila dalili kwamba JPM anafahamiana na Managing Director wa hii kampuni.

UPDATE:
CV ya Stephen Makigo:
View attachment 625369

Ni mshikaji flan hivi; kitambo sana... ndo maana wakati nipo ujenzi nikamtupa kwenye ujumbe TAMESA na hivi sasa kala shavu la kandarasi nene!!!
 
Kama ni hao jamaa wanajuana. Huyo jamaa amebebwa sana na Mzee. Tuache ukabila...JPM aache kuipendelea Chato sio kitu kizuri. Nakumbuka aliwahi kuhamisha barabara ya Sengerema Busisi Geita akaipeleka Geita Chato. That is wrong.
 
Mkuu unajua amewahi kufanya kazi zipi nchini za ukandarasi? Hapa nataka kujua kama ana uzoefu au ndiyo mpigaji madili wa Ikulu kafanya yake.

Mayanga yupo sababu ya JPM. Toka akiwa waziri huyo ni mtu wake. JPM aache kupendelea Chato maana watanzania wote wanamtazama.
Very pathetic
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Jamaa ni janga la Taifa huyu na ndani ya CCM wastaafu wengi wameanza kumsemea hovyo baada ya kutoridhishwa na muelekeo anakotaka kuipeleka nchi. Msekwa naye katoa kauli ya kumpa uenyekiti wa CCM Rais utaratibu huo utazamwe upya. Wanaona hakuna namna ya kumdhibiti huyu uchwara. Na kama kweli watashindwa kumdhibiti 2020 ili wamuweke pembeni basi ataiacha nchi yetu ikiwa katika hali mbaya sana.

Mayanga yupo sababu ya JPM. Toka akiwa waziri huyo ni mtu wake. JPM aache kupendelea Chato maana watanzania wote wanamtazama.
Very pathetic
 
Maswali kama haya wapeni wabunge wenu wakaulize bungeni.

Tunahangaika kuulizana JF, toka 2016 uwanja unajengwa, wabunge wenu hawasemi kitu hali kuwa pesa wanaidhinishwa tu. Wanaidhinisha pasipokujua mchakato na sababu za ujenzi?

Thubutu,
labda kama unataka kutolewa nje ya Bunge na kifungo juu!
kule kinachotakiwa ni mapambio tu!
 
Kwa upande wa uwezo Mkandarasi anakidhi vigezo vya kimataifa kwani ni class 1 contractor in Building and civil works and also ana uzoefu wa kazi za ujenzi wa muda mrefu hivyo kwenye uzoefu wa job with similar work mkandrasi yuko vzuri pia ni Mkandarasi mzawa anafanya mradi mkubwa wa lami Makutano - Mugumu alishakamilisha Daraja la Mbutu wilayani Igunga
Swali la msingi ni je sheria za manunuzi yaani PPRA zilifuatwa? lakini kiuwezo mkandarasi yuko vzuri sana.
Labda nami niongeze swali lingine hapa, kwa sasa ni viwanja vingapi vya kimikoa vinajengwa nchini? La mwisho,hivi ni kweli bilioni chini ya 50 inaweza ikajenga uwanja na ukawa na vigezo vyote vya kuitwa wa kimataifa? Kama ndivyo tungeujenga Kibaha, nadhani utakuwa ni wa kisasa zaidi ya wa Julius.
 
Madictator wengi huwa wanaanzaga kujenga viwanja vya ndege vijijini kwao....then hotel ya nyota5
Stay tune na kichwa namba8
 
Hivi managing director na executive director ni nani mmiliki wa kampuni? Sorry, kuuliza si ujinga waungwana, haya mambo mimi ni mgeni.
Inategemea, Umiliki wa kampuni ni kuwa na hisa nyingi, lakn hao wote ni watendaji wakuu wa kampuni, ikiwamo CEO wa kampuni. Kama kampuni ni ya mke na mme wamiki ninwao, kama ni ya partners, ni hao wamiliki.
 
Mkuu unajua amewahi kufanya kazi zipi nchini za ukandarasi? Hapa nataka kujua kama ana uzoefu au ndiyo mpigaji madili wa Ikulu kafanya yake.
Mradi mkubwa ninaokumbuka vizuri ni ule wa ujenzi wa barabara pamoja na daraja la Mbutu! Huu mradi naukumbuka kwa sababu ulitumiwa na CCM kwenye kampeni za uchaguzi mdogo Igunga baada ya Rostam kuachia ngazi!!!

Hata hivyo, sina uhakika huu mradi kama ulienda vizuri manake mwaka jana Mbunge wa Serengeti alimripua bungeni huyu Stephen Matiko kwamba yeye pamoja na wakandarasi wenzake wamelamba 14 Billion lakini hakuna cha maana kilichofanyika!!
 
I wish mnge fahamu hio MANYANGA ina maana gani wala msinge jisumbua
 
ili upewe Tenda ya kujenga au project yeyote ambayo ni sensitive kama airport pamoja na kukidhi vigezo vya usajili pia kigezo kikuu ni CV inayoonyesha umewahi kufanya kazi sawa na uliyoomba sehemu fulani...

Mawazo ya kujenga airport yanaweza yasiwe mabaya kama mtoa mawazo na mtoa hela kuna future business plan wameshaiweka kiasi cha kuwepo faida wakati wa matumizi, Mtoa mawazo ya kujenga labda ameshaona umuhimu wa uwanja kibiashara kutokana na mazingira atakayoyatengeneza baada ya ujenzi kukamilika, tumpe nafasi na muda..

Kiwango cha ujenzi kulingana na data za bwana Barafu ambaye tunamuamini kwa uwezo wake katika masuala ya aviation humu JF bila shaka ni kiwango sawa na KIA na JKNIA hivyo basi ukweli ni kwamba tumedhamiria kujenga uwanja wa Kimataifa ambao ili zitue ndege kubwa lazima ubora na usalama uwe first priority, JE HUYU MKANDARASI TULIYEMPA HII KAZI AMESHAWAHI KUFANYA KAZI KAMA HII MAHALI GANI TENA DUNIANI.. NA KAMA JIBU NI NDIYO JE UWANJA HUO NI WA UKUBWA GANI NA UKO WAPI?
 
Back
Top Bottom