Kampuni inayojenga Uwanja wa ndege Chato, Mayanga Construction inamilikiwa na nani na ilipataje tenda hiyo?

sijaelewa kwamba imesajiliwa mwaka jana reg no au????
 
Mkuu wewe unawashwa na nini?
Akijenga mzawa maneno hadi povu.
Wivu unawasumbua, jenga na wewe ingalau nyumba ysko ujijengee uwezo.
 
Ni kampuni ya mzawa na anauwezo wa kufanya hiyo kazi
 
This is a good question and I support accountability.
 
Kabisa SE, jamaa anaziweka kama mapambo Ikulu zipigwe vumbi maana anajua ni madudu matupu kuhusu awamu hii.

Hizo ripoff za CAG zinakuja na hazifanyiwi chochote
 
Mkuu unajua amewahi kufanya kazi zipi nchini za ukandarasi? Hapa nataka kujua kama ana uzoefu au ndiyo mpigaji madili wa Ikulu kafanya yake.

 

Kama ni hao jamaa wanajuana. Huyo jamaa amebebwa sana na Mzee. Tuache ukabila...JPM aache kuipendelea Chato sio kitu kizuri. Nakumbuka aliwahi kuhamisha barabara ya Sengerema Busisi Geita akaipeleka Geita Chato. That is wrong.
 
Mkuu unajua amewahi kufanya kazi zipi nchini za ukandarasi? Hapa nataka kujua kama ana uzoefu au ndiyo mpigaji madili wa Ikulu kafanya yake.

Mayanga yupo sababu ya JPM. Toka akiwa waziri huyo ni mtu wake. JPM aache kupendelea Chato maana watanzania wote wanamtazama.
Very pathetic
 
Reactions: BAK
Jamaa ni janga la Taifa huyu na ndani ya CCM wastaafu wengi wameanza kumsemea hovyo baada ya kutoridhishwa na muelekeo anakotaka kuipeleka nchi. Msekwa naye katoa kauli ya kumpa uenyekiti wa CCM Rais utaratibu huo utazamwe upya. Wanaona hakuna namna ya kumdhibiti huyu uchwara. Na kama kweli watashindwa kumdhibiti 2020 ili wamuweke pembeni basi ataiacha nchi yetu ikiwa katika hali mbaya sana.

Mayanga yupo sababu ya JPM. Toka akiwa waziri huyo ni mtu wake. JPM aache kupendelea Chato maana watanzania wote wanamtazama.
Very pathetic
 
Maswali kama haya wapeni wabunge wenu wakaulize bungeni.

Tunahangaika kuulizana JF, toka 2016 uwanja unajengwa, wabunge wenu hawasemi kitu hali kuwa pesa wanaidhinishwa tu. Wanaidhinisha pasipokujua mchakato na sababu za ujenzi?

Thubutu,
labda kama unataka kutolewa nje ya Bunge na kifungo juu!
kule kinachotakiwa ni mapambio tu!
 
Labda nami niongeze swali lingine hapa, kwa sasa ni viwanja vingapi vya kimikoa vinajengwa nchini? La mwisho,hivi ni kweli bilioni chini ya 50 inaweza ikajenga uwanja na ukawa na vigezo vyote vya kuitwa wa kimataifa? Kama ndivyo tungeujenga Kibaha, nadhani utakuwa ni wa kisasa zaidi ya wa Julius.
 
Madictator wengi huwa wanaanzaga kujenga viwanja vya ndege vijijini kwao....then hotel ya nyota5
Stay tune na kichwa namba8
 
Hivi managing director na executive director ni nani mmiliki wa kampuni? Sorry, kuuliza si ujinga waungwana, haya mambo mimi ni mgeni.
Inategemea, Umiliki wa kampuni ni kuwa na hisa nyingi, lakn hao wote ni watendaji wakuu wa kampuni, ikiwamo CEO wa kampuni. Kama kampuni ni ya mke na mme wamiki ninwao, kama ni ya partners, ni hao wamiliki.
 
Mkuu unajua amewahi kufanya kazi zipi nchini za ukandarasi? Hapa nataka kujua kama ana uzoefu au ndiyo mpigaji madili wa Ikulu kafanya yake.
Mradi mkubwa ninaokumbuka vizuri ni ule wa ujenzi wa barabara pamoja na daraja la Mbutu! Huu mradi naukumbuka kwa sababu ulitumiwa na CCM kwenye kampeni za uchaguzi mdogo Igunga baada ya Rostam kuachia ngazi!!!

Hata hivyo, sina uhakika huu mradi kama ulienda vizuri manake mwaka jana Mbunge wa Serengeti alimripua bungeni huyu Stephen Matiko kwamba yeye pamoja na wakandarasi wenzake wamelamba 14 Billion lakini hakuna cha maana kilichofanyika!!
 
I wish mnge fahamu hio MANYANGA ina maana gani wala msinge jisumbua
 
ili upewe Tenda ya kujenga au project yeyote ambayo ni sensitive kama airport pamoja na kukidhi vigezo vya usajili pia kigezo kikuu ni CV inayoonyesha umewahi kufanya kazi sawa na uliyoomba sehemu fulani...

Mawazo ya kujenga airport yanaweza yasiwe mabaya kama mtoa mawazo na mtoa hela kuna future business plan wameshaiweka kiasi cha kuwepo faida wakati wa matumizi, Mtoa mawazo ya kujenga labda ameshaona umuhimu wa uwanja kibiashara kutokana na mazingira atakayoyatengeneza baada ya ujenzi kukamilika, tumpe nafasi na muda..

Kiwango cha ujenzi kulingana na data za bwana Barafu ambaye tunamuamini kwa uwezo wake katika masuala ya aviation humu JF bila shaka ni kiwango sawa na KIA na JKNIA hivyo basi ukweli ni kwamba tumedhamiria kujenga uwanja wa Kimataifa ambao ili zitue ndege kubwa lazima ubora na usalama uwe first priority, JE HUYU MKANDARASI TULIYEMPA HII KAZI AMESHAWAHI KUFANYA KAZI KAMA HII MAHALI GANI TENA DUNIANI.. NA KAMA JIBU NI NDIYO JE UWANJA HUO NI WA UKUBWA GANI NA UKO WAPI?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…