Kampuni inayomiliki Tigo yabadili jina, sasa ni Honora Tanzania

Ni kwamba wawekezaji hupewa miaka 5 ya operation bila kulipa kodi then baada ya huo mda ndonhuanza kulipa kodi. Jamaa wanafanya 3 ama 4 years wanauza kwa madai wamepata hasara. Atakayekuja anaaza tena miaka 5 bure kudadeki
Ni sheria gani inawapa mwanya huu mkuu
 
Michezo ya kawaida Sana hiyo kwa King Maker Rostam Aziz. Ni wakati wake wa kula mema ya nchi baada ya miaka 2015-2021 kukomeshwa na lile jabali. King maker hakoso kuwa dalali wa DPW huyu. Huwa ni dalali wa mambo makubwamakubwa kama DPW
 

Hii ni kwel kabisa mkuu
 
Tigo, Voda na Airtel wanapata hasara za kutunga tu, ki uhalilisia jamaa wanamake profit sana
 
Sheria ipi inatoa mwanya huu mkuu
Kampuni za kigeni zinatangaza hasara miaka miwili au mitatu mfululizo harafu baadae wanatangaza kuuza umiliki kwenye kampuni nyingine kwa kubadili majina wanaanza upya mambo ya Tax sio wale waliopata hasara tena ndio maana utaona Airtel na Tigo wanavyocheza na huo mwanya kila baada ya muda wanabadili majina tuu...ipo kwenye Income Tax Act...
 
...Ni namna ya kukwepa Kodi TU. Muda wa Nafuu Kwa Muwekezaji imekwisha. Wanabadilisha jina na kudai ni Muwekezaji Mpya ili Wapate Nafuu nyingine!
Bongo tunaliwa TU !
Mic ina miaka 30 unaweza kutuelezea ulichoongea kinaingia vipi hapa?
 
Hii mbona ni muda tu, hiyo ni barua kwa business partner wao ndio wamechelewa kuitoa.

Kwa kifupi hii siyo habari.
Kitu pekee kinachonishangaza kwanini kampuni nyingi hata kama zinamilikiwa na watz lazima wakazifungulie nje
 
Acha uzushi kijana
 
Duuuh huu uboya sasa...mfanyabiashara mdogo amewekewa tozo kibao kabla hata ya kupata leseni wafanyabiashara wakubwa wanapiga hela wanasepa..
Sera mojawapo ya nchi kuvutia foreign investors ni kuwapa tax holidays ya miaka mitano ili kujiimalisha then baada ya hapo wanaanza kulipa. Kama wanaingia hasara wanasepa zao.
 
Kitu pekee kinachonishangaza kwanini kampuni nyingi hata kama zinamilikiwa na watz lazima wakazifungulie nje
Ungekuwa kwenye mfumo ungeelewa kirahisi sana.

Rwanda ukitaka kufunguwa kampuni checklist ni vitu vichache tu.

Sasa njoo Tanzania, TRA peke yake kupata Tax clearance na Vat registration check list ni vitu 16, ni upuuzi mtupu.

Njoo kwenye certificate sasa, ndio utacheka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…