Kampuni Kutoka China Kujenga Daraja la Dar- Zanzibar

Huijui bongo hilo haliwezekani bakhresa ameshusha kitu kipya juzi tu kuna watu hii nchi wanafanya wanavyotaka kwa maslahi yao binafsi watapiga vita hyo kitu
Bakhresa ni mdogo sana, hilo daraja lazima lijengwe. Hii itakuwa zawadi ya mama nyumbani kwao. Waliosoma Cuba wamenielewa
 
Kama daraja lijengwe ziwa Tanganyika to congo, pale pana biashara ya maana itafutwe mahala ambapo kina sio kirefu cha kutisha iwekwe daraja.

Kwa Zanzibar mradi hautalipa
Ziwa tanganyika kina ni kirefu hatari, ajali za kule ukitizama watu wamezama jirani tu na ufukwe, kule kuna bonde la ufa samaki wanakufa kwa uzee.
 
Ni sawa, kuwe na route ya Daladala... Dar - Zanzibar (Unguja au Pemba)
 
That's true,, anasukuma hii agenda Ili isaidie Zanzibar tu, becoz Bara haifaidiki kiasi hicho na Daraja la Zanzibar na hizo PESA zingefanya kitu kikubwa sana kwa maendeleo ya wabara.
 
Samahani lakini usinichoke tuendelee kueleweshana. Umeelezea vizuri pia. Changamoto nayoiona hapo ni kwamba, Zanzibar ni nchi kamili tofauti na kigamboni.

Sijajua interaction ipoje, lakini naona interaction siyo kubwa sana kutokana na vizingiti vilivyopo upande wa Zanzibar kwa Watanzania bara.

Binafsi naona interaction ingekuwa ni kubwa sana na hayo magari elfu 1 yangekuwa yanapita hilo daraja kama nchi ingekuwa ni moja na Zanzibar ingekuwa ni kama Kigamboni, hivyo movement ingekuwa ni kubwa sana kwa Watanzania bara kwenda Zanzibar kwa magari kila siku.

Lakini kwa sasa Mtanzania bara haruhusiwi kumiliki ardhi Zanzibar, hivyo kupunguza movements kwa sababu ni Watanzania bara wachache wataokuwa tayari kuishi Zanzibar kwa kupanga maisha yao yote. Hata hao Watanzania bara ambao wamejenga na kumiliki ardhi kinyemela wanajidanganya tu kwa sababu sheria haiwalindi. Hii ni tofauti na Kigamboni ambapo mtu yoyote anaweza kwenda kujenga na kuishi huko, hivyo daraja la huko kuwa na wateja wengi.
 
Ndio maana nimeuliza, Watanzania bara watapata faida gani?
 
Litakua jambo zuri sana kwa tz. huu mradi, utakuwepo kweli na kufanikiwa, kutakua na faida sana na wafanyabiasha, kuligana na znz, inavyopokea wageni??
 
Ni sawa, kuwe na route ya Daladala... Dar - Zanzibar (Unguja au Pemba)
Ndoto hiyo ya Dar / Unguja inaweza ikatimia karne ijayo lakini hii ya Unguja Pemba haipo kabisa.Pale Nungwi vikosi vya kutoka Afrika Kusini viliakhirisha kazi ya kuiangalia meli ya Spice iliyozama pale na watu wake.Walisema hawana vifaa vya kukaribia iliko.Ni kilomita kadhaa chini ya bahari. Nguzo itajengwa wapi ?
 
Kwa hiyo underwater tunnel Bridge la kuunganisha Kigamboni na Posta limekuwa gumu ila la Zanzibar inawezekana? Kweli kila zama na kitabu chake!
Tupunguze ubinafsi wa waziwazi!!!
 
Huku inchini kuna uhaba wa Barabara bora na uhitaji ni mkubwa kweli kweli ila watu mnapanga kutumia pesa kutengeza daraja ambao ukiuliza msukumo wake ni nini mtatuambia muungano ambao Zanzibar wenyewe wanaukataa.

Kwann Zanzibar hawajiiti Tanzania Visiwani ila mnataka sisi tujiite Tanzania bara.
 
Waulize wazambia,wachina wanamalengo ya kuitawala africa
Acha ujinga wa kusikiliza propaganda za marekani na vibaraka wake.

Wewe kama una akili timamu tazama katika mahusiano ya US na Tanzania au Africa na Mahusiano ya China na Africa au Tanzania ni yapi yana manufaa.

Hapo kuanzia nguo, simu vifaa vya ndani, mashuka, vyombo unapikia hadi jiko la gesi mchina amefanya yake, marekani ukiachia program za tv tena movie na internet ni kipi cha direct amekufanyia?
 

Wachina wabarikiwe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…