Kampuni Kutoka China Kujenga Daraja la Dar- Zanzibar

Kampuni Kutoka China Kujenga Daraja la Dar- Zanzibar

Kampuni ya China Overseas Engineering Group imeonesha Nia ya kujenga Daraja la km 40 Kati ya Dar na Zanzibar,Naibu Waziri Kasekenya amesema Bungeni..

My Take
Kama Daraja hili litajengwa linaweza kutumia nusu ya gharama za Kujenga SGR.

Swali Je Tunalihitaji Kwa Sasa?

Ally Nacha.
 
Ni heri wazanzibar wajenge daraja kuuganisha visiwa vyao.(Unguja na Pemba)
 
Kampuni ya China Overseas Engineering Group imeonesha Nia ya kujenga Daraja la km 40 Kati ya Dar na Zanzibar,Naibu Waziri Kasekenya amesema Bungeni..

My Take
Kama Daraja hili litajengwa linaweza kutumia nusu ya gharama za Kujenga SGR.

Swali Je Tunalihitaji Kwa Sasa?

Ina maana likishajengwa boti zitakua hazina kazi!?nauliza tu naomba kufahamu!
 
Naomba unisaidie! Ni faida gani Watanzania bara watazipata kutokana na daraja hilo tofauti na sasa?
Tutapata faida kubwa tukijenga Daraja kutoka mjini Dares-Salaam Mpaka Zanzibar kwani kila gari itakayo pita katika daraja hilo itatozwa karibu Shilingi Elfu 20. Tuchukulie kwa mfano kila siku kuna magari 1000 yanayo kwenda mjini Zanzibar aka yatakayo pita katika hilo daraja tutapata karibu shilingi Millioni 20 kwa siku moja tu. Chukuliwa kwa mwezi tutapata shilingi Millioni 600 kwa mwaka tutapara shilingi Billioni 7 na Millioni 200. Tutaweza kurudisha pesa yetu tuliyoitengeneza kwa muda wa miaka 40 tu. Na tutapata wageni wengi kutoka nje ambao watakao kuja na kwenda Zanzibar kwa ajili ua Utalii. Na hao wageni watatuingizia pesa ya kigeni dollar kwa wngi tu.Tofauti na hivi sasa Serikali inapata pesa kidogo kutoka bandari kwa kuwatoza wafanya biashara wa boti zinazokwenda mjini Zanzibar Boti za akina Bakhressa na Wafanya Biashara wenzake.Hata Ulaya madaraja kama hayo yapo mengi tu na yanawaingizia Serikali vipato vya pesa vingi kila mwaka Serikali inafaidika kwa kupata vipato vya kulipia madaraja kama hayo. Tofauti na Serikali yetu ikitengeneza Mabarabara hawapati kitu Serikali kuhusu mabarabara kuliko daraja kama hilo. Chunguza daraja la kigamboni Serikali inapata kiasi gani cha pesa kila siku? Kisha utapata jibu kuwa daraja la Dar to Zanzibar litakuwa na faida kubwa zaidi kuliko Daraja la kigamboni. Wakiwepo wasimamizi wazuri tutafaidika sana kutokana na hilo daraja.

d4e6b723-9142-4edf-a902-4372411858f4.jpg
 
Sina wasi wasi hili daraja ni ndoto tu halitajengwa katika karne hii. Wachilia mbali mambo ya gharama eneo linapotaka kujengwa litahitaji mipango mikubwa sana. Ikitajwa kujengwa baina ya Dar es salaam na Zanzibar lazima daraja hilo litaingia./Litatokea maeneo ya mpakani baina ya dAR na Bagamoyo sijui ni Bunju au wapi pale.Eneo hilo bado lina mawimbi makali ya bahari na bahari inapochafuka ndio kazi zaidi. Hilo daraja itabidi liwe pana ili kutoa njia za uokozi na si njia mbili tu.Tuseme kumetokea kimbunga cha ghafla na gari ziko katikati ya daraja.Lazima ziwe na njia ya kukatisha safari na kurudi ilikotoka.Haitowezekana gari ikishaelelekea Zanzibar basi iwe ni kwenda tu.Hii siku ikitokea athari hiyo ya hali mbaya basi tutapoteza watu wengi baharini.
Mawazo yako yapo finyu sana Serikali mpaka imeamuwa kutaka kutengeneza Daraja ukae ukijuwa kila kitu kitakuwa kipo sawa tofauti na mawazo yako uliyo nayo. Wewe nenda kaangalie Daraja la kigamboni jinsi lilivyo tengenezwa na wachina?
Je daraja la Dar mpaka Zanzibar litakuwaje ukubwa wake?

d4e6b723-9142-4edf-a902-4372411858f4.jpg
 
Serikali imeanza mazungumzo na Kampuni ya China Overseas Engineering Group Company (COVEC) ambayo imeonesha nia ya kuwekeza katika ujenzi wa daraja litakalo unganisha Tanzania Bara na Zanzibar.

Naibu Waziri wa Uchukuzi Godfrey Kasekenya amesema bungeni leo Aprili 28, 2023 kuwa Mazungumzo hayo yameanza Machi 11, 2023 na yalihusisha wataalamu kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi Sekta ya Ujenzi kwa upande wa Tanzania Bara na Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi kwa upande wa Zanzibar.

Akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Mwantum Dau Haji aliyetaka kujua mpango wa serikali kujenga daraja hilo, Naibu Waziri Kasekenya amesema bado mazungumzo yanaendelea na serikali inakusudia kujiridhisha na teknolojia zinazotumika katika ujenzi wa madaraja makubwa kabla ya kuanza ujenzi.

“Daraja hili litajengwa kwa kushirikiana na sekta binafsi kwa utaratibu wa PPP (Public-Private Partnership),” amesisitiza Kasekenya.

#HabarileoUPDATES
View attachment 2602214
d4e6b723-9142-4edf-a902-4372411858f4.jpg
 
Hili daraja kwa faida ya nani?

Zanzibar wanapanga kujenga bandari kubwa sana. Hilo daraja ni sehemu ya mpango huo.

Likijengwa, inaweza kuwa kifo cha Bandari yetu ya Dar. Wa Tanganyika tuamke!

Daraja la nini? Kwa trafiki gani ya magari kati Dar ma Zanzibar? Azam Marine inatosha kwa usafiri wa kawaida wa abiria. Hela yote ya Banfari itaenda Zanzibar. Akili kumkichwa.
 
Tutapata faida kubwa tukijenga Daraja kutoka mjini Dares-Salaam Mpaka Zanzibar kwani kila gari itakayo pita katika daraja hilo itatozwa karibu Shilingi Elfu 20. Tuchukulie kwa mfano kila siku kuna magari 1000 yanayo kwenda mjini Zanzibar aka yatakayo pita katika hilo daraja tutapata karibu shilingi Millioni 20 kwa siku moja tu. Chukuliwa kwa mwezi tutapata shilingi Millioni 600 kwa mwaka tutapara shilingi Billioni 7 na Millioni 200. Tutaweza kurudisha pesa yetu tuliyoitengeneza kwa muda wa miaka 40 tu. Na tutapata wageni wengi kutoka nje ambao watakao kuja na kwenda Zanzibar kwa ajili ua Utalii. Na hao wageni watatuingizia pesa ya kigeni dollar kwa wngi tu.Tofauti na hivi sasa Serikali inapata pesa kidogo kutoka bandari kwa kuwatoza wafanya biashara wa boti zinazokwenda mjini Zanzibar Boti za akina Bakhressa na Wafanya Biashara wenzake.Hata Ulaya madaraja kama hayo yapo mengi tu na yanawaingizia Serikali vipato vya pesa vingi kila mwaka Serikali inafaidika kwa kupata vipato vya kulipia madaraja kama hayo. Tofauti na Serikali yetu ikitengeneza Mabarabara hawapati kitu Serikali kuhusu mabarabara kuliko daraja kama hilo. Chunguza daraja la kigamboni Serikali inapata kiasi gani cha pesa kila siku? Kisha utapata jibu kuwa daraja la Dar to Zanzibar litakuwa na faida kubwa zaidi kuliko Daraja la kigamboni. Wakiwepo wasimamizi wazuri tutafaidika sana kutokana na hilo daraja.

View attachment 2604379
Hela ndogo sana hizo. Hili daraja litakuja kuua Bandari ya Dar. Je Bandari inaingiza kiasi gani kwa siku?
Hilo daraja ni sehemu ya mpango wao na Dr Mwinyi keshasema watajenga Bandari kubwa sana kule Zanzibar.
Katika hali ya kawaida, unategemea magari 1,000 yapite daraja hilo kwa shughuli zipi?
Watanganyika tuamke. Tusije tukaua Bandari ya Dar
 
Huu mpango ulianza kipindi cha awamu ya nne baadae ukaachwa baada ya kuonekana z'bar haina pesa.kwa sasa wanalazimisha.Nimeamini kweli remote ipo kule msoga
 
Huu mpango ulianza kipindi cha awamu ya nne baadae ukaachwa baada ya kuonekana z'bar haina pesa.kwa sasa wanalazimisha.Nimeamini kweli remote ipo kule msoga
Kama daraja lijengwe ziwa Tanganyika to congo, pale pana biashara ya maana itafutwe mahala ambapo kina sio kirefu cha kutisha iwekwe daraja.

Kwa Zanzibar mradi hautalipa
 
Na hela itakayotumika kukamilisha hiyo shughuli ni kutoka Tanganyika bara......ahhhh sorry Tanzania bara.
Pesa ya Tanganyika halafu ikaue mgodi wetu wa dhahabu unaoitwa Bandari ya Dar. Kuna janja jamja iko hapo.
 
Wameshirikisha washika dau lakini kwenye huo mpango?

Kuna watu wamenunua Boti mpya na za kisasa zinatoa huduma huko, usije mradi kuanzishwa lakini ukashindwa kukamilika.

I'm just thinking loud [emoji848]
Kuna mwingine kaongeza ya VIII
 
Kama daraja lijengwe ziwa Tanganyika to congo, pale pana biashara ya maana itafutwe mahala ambapo kina sio kirefu cha kutisha iwekwe daraja.

Kwa Zanzibar mradi hautalipa
Kabisa.Ni bora ujengwe huko.maana huko kunaidadi ya watu kubwa sana kwa congo.Kwa zanzibar tunapoteza pesa tu lakini hakuna cha maana.
 
Hilo daraja likijengwa meli kutoka nje itabidi zitume njia ndefu kupita nyuma ya kisiwa cha Unguja.na boti za Bakhres zitaishia kusini ya Unguja maeneo ya Kizimkazi.
Unajua ni wapi linajengwa?
 
Miradi ya Viongozi wa Tanzania inashangaza sana ,just imagine anachoongea huyu bwana hapa kina logic kabisa ila wenye akili ndogo Huwa hawaelewi
Wenye akili ndogo kama wewe sio?
Nini kitakuzuia kwenda kununua nyanya kwenye ghorofa?
 
Back
Top Bottom