Kampuni Kutoka China Kujenga Daraja la Dar- Zanzibar

Kampuni Kutoka China Kujenga Daraja la Dar- Zanzibar

Kampuni ya China Overseas Engineering Group imeonesha Nia ya kujenga Daraja la km 40 Kati ya Dar na Zanzibar,Naibu Waziri Kasekenya amesema Bungeni..

My Take
Kama Daraja hili litajengwa linaweza kutumia nusu ya gharama za Kujenga SGR.

Swali Je Tunalihitaji Kwa Sasa?

Awamu ya sita inajipanga kupiga hela ndefu sana
 
hahahaha, ni kipaumbele chetu kwasasa?.

hakuna maeneo mengine yanayohitaji quick investment na short time return kwasasa?

Kwanini asitafutwe muwekezaji na kuingia parnership na serikali tuchimbe chuma cha Liganga na Mchuchuma kwa haraka ili bei ya chuma ipungue, then tutafute kampuni with partner na watanzania wakajenga plant kwaajili ya kutengeneza electric cars na huku tunaweka nguvu kubwa ya kuchimba graphite pale Lindi vs mass production batteries plant kule kusini?
 
Wachina wako vizuri sana kwenye ujenzi wa miundombinu

Wamejenga Hong Kong–Zhuhai–Macau Bridge (HZMB) 55 km

images (1).jpeg


images.jpeg
 
hahahaha, ni kipaumbele chetu kwasasa?.

hakuna maeneo mengine yanayohitaji quick investment na short time return kwasasa?.

Kwanini asitafutwe muwekezaji na kuingia parnership na serikali tuchimbe chuma cha Liganga na Mchuchuma kwa haraka ili bei ya chuma ipungue, then tutafute kampuni with partner na watanzania wakajenga plant kwaajili ya kutengeneza electric cars na huku tunaweka nguvu kubwa ya kuchimba graphite pale Lindi vs mass production batteries plant kule kusini?..
Siku zote kama mtu hajui aendako hawezi kupotea njia.
 
Kwa kuwa kama ilivyo kawaida yetu kila awamu lazima iache alama yake, na miradi mingi mikubwa serikali ya sasa inayofanya ni ile iliyoachwa na Magufuli.

Ngoja tuone miradi mikubwa ya awamu hii itakuwa ni ipi, naona huu wa daraja la Dar - Zanzibar utakuwa kama tulivyoona ule wa Kigongo - Busisi ulioasisiwa na mwendazake kule Mwanza, kila mtawala lazima apakumbuke nyumbani kwanza.

Kama ikitokea siku ujenzi huo ukaanza, naona huo ndio utakuwa mwanzo wa mwisho wa biashara ya boti za kusafirisha watu, mwendo hapo utakuwa ni magari tu yanapishana kwenda Zanzibar.
 
Miradi mingi mikubwa serikali ya sasa inayofanya ni ile iliyoachwa na Magufuli, ngoja tuone miradi mikubwa ya awamu hii itakuwa ni ipi au kama huu wa daraja la Dar Zanzibar utakuwa mmojawapo kama tulivyoona Kigongo Busisi uliaasisiwa na mwendazake.
Umejuaje kama siyo wa Mama
 
Serikali imeanza mazungumzo na Kampuni ya China Overseas Engineering Group Company (COVEC) ambayo imeonesha nia ya kuwekeza katika ujenzi wa daraja litakalo unganisha Tanzania Bara na Zanzibar.

Naibu Waziri wa Uchukuzi Godfrey Kasekenya amesema bungeni leo Aprili 28, 2023 kuwa Mazungumzo hayo yameanza Machi 11, 2023 na yalihusisha wataalamu kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi Sekta ya Ujenzi kwa upande wa Tanzania Bara na Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi kwa upande wa Zanzibar.

Akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Mwantum Dau Haji aliyetaka kujua mpango wa serikali kujenga daraja hilo, Naibu Waziri Kasekenya amesema bado mazungumzo yanaendelea na serikali inakusudia kujiridhisha na teknolojia zinazotumika katika ujenzi wa madaraja makubwa kabla ya kuanza ujenzi.

“Daraja hili litajengwa kwa kushirikiana na sekta binafsi kwa utaratibu wa PPP (Public-Private Partnership),” amesisitiza Kasekenya.

#HabarileoUPDATES
View attachment 2602214
Bill kwa Tanganyika
 
hahahaha, ni kipaumbele chetu kwasasa?.

hakuna maeneo mengine yanayohitaji quick investment na short time return kwasasa?

Kwanini asitafutwe muwekezaji na kuingia parnership na serikali tuchimbe chuma cha Liganga na Mchuchuma kwa haraka ili bei ya chuma ipungue, then tutafute kampuni with partner na watanzania wakajenga plant kwaajili ya kutengeneza electric cars na huku tunaweka nguvu kubwa ya kuchimba graphite pale Lindi vs mass production batteries plant kule kusini?
Daaah upo serious na haya mawazo kweli kwa Taifa lenye viongozi wa mbeleko,wabinafsi na wajinga.

Tanzania hatuwezi kuendelea sababu tunaongozwa na wajinga.
 
Zanzibar ina hela gani za kujenga daraja wakati bajeti ya nchi nzima ya Zanzibar 2022/2023 ilikuwa Tsh trill. 2.5 kwanza itaweka dhamana ipi kuchukua mkopo wa bank labda kama alivyowahi kusema J.k kuwa walichonacho ni virungu vya polisi tu.
 
Back
Top Bottom