Waulize wazambia,wachina wanamalengo ya kuitawala africaDuh biashara za watu zinaanza wekwa wasiwasii
Ila wachina mmetutoa sana waafrica kwa miradi yenu na bidhaa zenuu
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Waulize wazambia,wachina wanamalengo ya kuitawala africaDuh biashara za watu zinaanza wekwa wasiwasii
Ila wachina mmetutoa sana waafrica kwa miradi yenu na bidhaa zenuu
Exactly mkuuMUUNGANO BRIDGE ITAPENDEZA
ova
Kampuni ya China Overseas Engineering Group imeonesha Nia ya kujenga Daraja la km 40 Kati ya Dar na Zanzibar,Naibu Waziri Kasekenya amesema Bungeni..
My Take
Kama Daraja hili litajengwa linaweza kutumia nusu ya gharama za Kujenga SGR.
Swali Je Tunalihitaji Kwa Sasa?
Itapunguza gharama asee, haiwezekani safari ya lisaa na nusu unapigwa 30,000Serikali imeanza mazungumzo na Kampuni ya China Overseas Engineering Group Company (COVEC) ambayo imeonesha nia ya kuwekeza katika ujenzi wa daraja litakalo unganisha Tanzania Bara na Zanzibar.
Naibu Waziri wa Uchukuzi Godfrey Kasekenya amesema bungeni leo Aprili 28, 2023 kuwa Mazungumzo hayo yameanza Machi 11, 2023 na yalihusisha wataalamu kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi Sekta ya Ujenzi kwa upande wa Tanzania Bara na Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi kwa upande wa Zanzibar.
Akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Mwantum Dau Haji aliyetaka kujua mpango wa serikali kujenga daraja hilo, Naibu Waziri Kasekenya amesema bado mazungumzo yanaendelea na serikali inakusudia kujiridhisha na teknolojia zinazotumika katika ujenzi wa madaraja makubwa kabla ya kuanza ujenzi.
“Daraja hili litajengwa kwa kushirikiana na sekta binafsi kwa utaratibu wa PPP (Public-Private Partnership),” amesisitiza Kasekenya.
#HabarileoUPDATES
View attachment 2602214
Labda yeye ni mvuvi!Kwa nini? Bridge Highway si ndio Itaongeza utamu zaidi?
wewe wacha utani hapa! Hivi kwa miaka yote Magufuli alipokuwa rais wa tanzania alipeleka mradi gani Zanzibar? Mnasema kajenga hili na kile huku na kule barabara, maji nk hebu niambie ni mradi gani alioupeleka Zanzibar ikiwa Zanzibar ni sehemu ya Tanzania? Hakuna hata mradi mmoja uliofanywa na serikali ya Tanzania katika kisiwa cha unguja au pemba wakati wa uhai wa magufuli. Magufuli asingeliruhusu kabisa idea ya kujenga daraja kuwa reality hata siku moja. Magufuli hakuwa hakuwa akiitakia mema zanzibar. Kumbuka kuwa project zake nyingi alikuwa akizielekeza katika sehemu ambazo CCM strong hold tu!Jemedari mkuu Magufuli angelikuwa hai ningeamini hilo jambo linawezekana bila upembuzi yakinifu lakini hawa waliopo ni michakato tu!
Hadi wakatengeneza na kisiwa bandia! Naelewa unachoongea hapaWachina wako vizuri sana kwenye ujenzi wa miundombinu
Wamejenga Hong Kong–Zhuhai–Macau Bridge (HZMB) 55 km
View attachment 2602251
View attachment 2602252
Hatuna pesa za kupotezea baharini kiholela. Huu mpango usitishwe mara moja!Serikali imeanza mazungumzo na Kampuni ya China Overseas Engineering Group Company (COVEC) ambayo imeonesha nia ya kuwekeza katika ujenzi wa daraja litakalo unganisha Tanzania Bara na Zanzibar.
Naibu Waziri wa Uchukuzi Godfrey Kasekenya amesema bungeni leo Aprili 28, 2023 kuwa Mazungumzo hayo yameanza Machi 11, 2023 na yalihusisha wataalamu kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi Sekta ya Ujenzi kwa upande wa Tanzania Bara na Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi kwa upande wa Zanzibar.
Akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Mwantum Dau Haji aliyetaka kujua mpango wa serikali kujenga daraja hilo, Naibu Waziri Kasekenya amesema bado mazungumzo yanaendelea na serikali inakusudia kujiridhisha na teknolojia zinazotumika katika ujenzi wa madaraja makubwa kabla ya kuanza ujenzi.
“Daraja hili litajengwa kwa kushirikiana na sekta binafsi kwa utaratibu wa PPP (Public-Private Partnership),” amesisitiza Kasekenya.
#HabarileoUPDATES
View attachment 2602214
Na bado kule South China Sea wamejenga visiwa zaidi ya 10 ili kulilinda eneo laoHadi wakatengeneza na kisiwa bandia! Naelewa unachoongea hapa
Ok wajipange watakuwa wanaenda PembaWameshirikisha washika dau lakini kwenye huo mpango?
Kuna watu wamenunua Boti mpya na za kisasa zinatoa huduma huko, usije mradi kuanzishwa lakini ukashindwa kukamilika.
I'm just thinking loud [emoji848]
Kama wanatujengea BURE naungana nawe. WACHINA MMBARIKIWE SANA.Halafu anakuja mtu from nowhere eti ni heri ya mzungu kuliko mchina
Wachina mmbarikiwe sana,
kwa kuwa rais katoka kule usishtuke mpaka tumefika kusikia wimbo huu, wa kujipendekeza wapo biz kuzifukuzia fursa za teuzi. Hakuna tofauti na wale waliojipendekeza kujenga airport na vinginevyo kijijini Chato.Hilo daraja halina tija yoyote ile kwa Watanganyika. Kama Wazanzibari wanaweza kujenga kwa gharama zao ili waje Tanganyika kwa urahisi, wajenge.