Kampuni Kutoka China Kujenga Daraja la Dar- Zanzibar

Kampuni Kutoka China Kujenga Daraja la Dar- Zanzibar

Kampuni ya China Overseas Engineering Group imeonesha Nia ya kujenga Daraja la km 40 Kati ya Dar na Zanzibar,Naibu Waziri Kasekenya amesema Bungeni..

My Take
Kama Daraja hili litajengwa linaweza kutumia nusu ya gharama za Kujenga SGR.

Swali Je Tunalihitaji Kwa Sasa?

Hii nzuri maana ile ndoto ya kwenda zenji kwa baiskeli itaenda kutimia😂😂😂
 
Kampuni ya China Overseas Engineering Group imeonesha Nia ya kujenga Daraja la km 40 Kati ya Dar na Zanzibar,Naibu Waziri Kasekenya amesema Bungeni..

My Take
Kama Daraja hili litajengwa linaweza kutumia nusu ya gharama za Kujenga SGR.

Swali Je Tunalihitaji Kwa Sasa?

Hizi ndo hoja muhimu kwa nchi.

Tumezoeshana hoja za nani anataka urais, mara huyu kachepuka, mara fulani pisi kali......

Turudi hapa tujadili maendeleo ya nchi yetu.

Daraja lijengwe nitaomba nifanye jogging ya kwenda zenji na kurudi
 
Serikali imeanza mazungumzo na Kampuni ya China Overseas Engineering Group Company (COVEC) ambayo imeonesha nia ya kuwekeza katika ujenzi wa daraja litakalo unganisha Tanzania Bara na Zanzibar.

Naibu Waziri wa Uchukuzi Godfrey Kasekenya amesema bungeni leo Aprili 28, 2023 kuwa Mazungumzo hayo yameanza Machi 11, 2023 na yalihusisha wataalamu kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi Sekta ya Ujenzi kwa upande wa Tanzania Bara na Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi kwa upande wa Zanzibar.

Akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Mwantum Dau Haji aliyetaka kujua mpango wa serikali kujenga daraja hilo, Naibu Waziri Kasekenya amesema bado mazungumzo yanaendelea na serikali inakusudia kujiridhisha na teknolojia zinazotumika katika ujenzi wa madaraja makubwa kabla ya kuanza ujenzi.

“Daraja hili litajengwa kwa kushirikiana na sekta binafsi kwa utaratibu wa PPP (Public-Private Partnership),” amesisitiza Kasekenya.

#HabarileoUPDATES
View attachment 2602214
Kwanza waanze kijiunganisha wenyewe Unguja na Pemba.

Baada ya kupata katiba mpya ndiyo tuanze kufikiria kuunganisha Zanzibar na Tanganyika kwa daraja kwa sababu mpaka sasa hakuna muafaka wa muungano huu tulionao!
 
Kampuni ya China Overseas Engineering Group imeonesha Nia ya kujenga Daraja la km 40 Kati ya Dar na Zanzibar,Naibu Waziri Kasekenya amesema Bungeni..

My Take
Kama Daraja hili litajengwa linaweza kutumia nusu ya gharama za Kujenga SGR.

Swali Je Tunalihitaji Kwa Sasa?

Hilo daraja likijengwa meli kutoka nje itabidi zitume njia ndefu kupita nyuma ya kisiwa cha Unguja.na boti za Bakhres zitaishia kusini ya Unguja maeneo ya Kizimkazi.
 
Hilo daraja likijengwa meli kutoka nje itabidi zitume njia ndefu kupita nyuma ya kisiwa cha Unguja.na boti za Bakhres zitaishia kusini ya Unguja maeneo ya Kizimkazi.
kisiwa cha Uingereza kimeunganishwa kwa daraja la chini kwa chinj, meli hazitaingiliwa njia zake, wanaweza fika hapo wakaweka hata daraja refu zaidi km myo Themes huko London

Sent from my Infinix PR652B using JamiiForums mobile app
 
Yaani tunaweza kujenga Daraja la Matrilioni lakini tunashindwa kujenga japo IRRIGATION SCHEME japo moja kwa kila KATA ya nchi hii na tunadai KILIMO cha UTI WA MGONGO...

Viongozi hawana mpango wa kuinua Uchumi wa Wananchi.... Madaraja hata yajae nchi nzima kama Wananchi hawana hela ni kazi bure...
Hii Nchi Ina matatizo sana ya Vipaombele,mambo yasiyo na msingi ndio Wanasiasa wanapenda Ili wapige
 
Kampuni ya China Overseas Engineering Group imeonesha Nia ya kujenga Daraja la km 40 Kati ya Dar na Zanzibar,Naibu Waziri Kasekenya amesema Bungeni..

My Take
Kama Daraja hili litajengwa linaweza kutumia nusu ya gharama za Kujenga SGR.

Swali Je Tunalihitaji Kwa Sasa?

Samahani, Meli kubwa zitwekewewa vipande maalum kwa ajiki ya kupenya sio? Au ndio itabidi ziizunguke Zanzibar? Nani atalipia gharama hiyo?
 
Hizi ndo hoja muhimu kwa nchi.

Tumezoeshana hoja za nani anataka urais, mara huyu kachepuka, mara fulani pisi kali......

Turudi hapa tujadili maendeleo ya nchi yetu.

Daraja lijengwe nitaomba nifanye jogging ya kwenda zenji na kurud
Waliowahi kwenda .Jee huko kwao wameshajenga daraja la kupita mkondo mkali kama wa magogoni au Nungwi.
 
Back
Top Bottom