Kampuni Kutoka China Kujenga Daraja la Dar- Zanzibar

Awamu ya sita inajipanga kupiga hela ndefu sana
 
hahahaha, ni kipaumbele chetu kwasasa?.

hakuna maeneo mengine yanayohitaji quick investment na short time return kwasasa?

Kwanini asitafutwe muwekezaji na kuingia parnership na serikali tuchimbe chuma cha Liganga na Mchuchuma kwa haraka ili bei ya chuma ipungue, then tutafute kampuni with partner na watanzania wakajenga plant kwaajili ya kutengeneza electric cars na huku tunaweka nguvu kubwa ya kuchimba graphite pale Lindi vs mass production batteries plant kule kusini?
 
Siku zote kama mtu hajui aendako hawezi kupotea njia.
 
Kwa kuwa kama ilivyo kawaida yetu kila awamu lazima iache alama yake, na miradi mingi mikubwa serikali ya sasa inayofanya ni ile iliyoachwa na Magufuli.

Ngoja tuone miradi mikubwa ya awamu hii itakuwa ni ipi, naona huu wa daraja la Dar - Zanzibar utakuwa kama tulivyoona ule wa Kigongo - Busisi ulioasisiwa na mwendazake kule Mwanza, kila mtawala lazima apakumbuke nyumbani kwanza.

Kama ikitokea siku ujenzi huo ukaanza, naona huo ndio utakuwa mwanzo wa mwisho wa biashara ya boti za kusafirisha watu, mwendo hapo utakuwa ni magari tu yanapishana kwenda Zanzibar.
 
Miradi mingi mikubwa serikali ya sasa inayofanya ni ile iliyoachwa na Magufuli, ngoja tuone miradi mikubwa ya awamu hii itakuwa ni ipi au kama huu wa daraja la Dar Zanzibar utakuwa mmojawapo kama tulivyoona Kigongo Busisi uliaasisiwa na mwendazake.
Umejuaje kama siyo wa Mama
 
Bill kwa Tanganyika
 
Daaah upo serious na haya mawazo kweli kwa Taifa lenye viongozi wa mbeleko,wabinafsi na wajinga.

Tanzania hatuwezi kuendelea sababu tunaongozwa na wajinga.
 
Zanzibar ina hela gani za kujenga daraja wakati bajeti ya nchi nzima ya Zanzibar 2022/2023 ilikuwa Tsh trill. 2.5 kwanza itaweka dhamana ipi kuchukua mkopo wa bank labda kama alivyowahi kusema J.k kuwa walichonacho ni virungu vya polisi tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…