Kampuni Kutoka China Kujenga Daraja la Dar- Zanzibar

Wameshirikisha washika dau lakini kwenye huo mpango?

Kuna watu wamenunua Boti mpya na za kisasa zinatoa huduma huko, usije mradi kuanzishwa lakini ukashindwa kukamilika.

I'm just thinking loud 🤔
 
Inalipa mara elfu zaidi ukilinganisha na namna tunavyoibiwa. Mama ameshaanza kulalamika watu wanaiba fedha. Pengine ukilinganisha kile ambacho tayari tumeshaibiwa mpaka muda huu, ni fedha nyingi mno kuliko hiyo itakayojenga daraja hilo
 
Itapunguza gharama asee, haiwezekani safari ya lisaa na nusu unapigwa 30,000
 
Jemedari mkuu Magufuli angelikuwa hai ningeamini hilo jambo linawezekana bila upembuzi yakinifu lakini hawa waliopo ni michakato tu!
wewe wacha utani hapa! Hivi kwa miaka yote Magufuli alipokuwa rais wa tanzania alipeleka mradi gani Zanzibar? Mnasema kajenga hili na kile huku na kule barabara, maji nk hebu niambie ni mradi gani alioupeleka Zanzibar ikiwa Zanzibar ni sehemu ya Tanzania? Hakuna hata mradi mmoja uliofanywa na serikali ya Tanzania katika kisiwa cha unguja au pemba wakati wa uhai wa magufuli. Magufuli asingeliruhusu kabisa idea ya kujenga daraja kuwa reality hata siku moja. Magufuli hakuwa hakuwa akiitakia mema zanzibar. Kumbuka kuwa project zake nyingi alikuwa akizielekeza katika sehemu ambazo CCM strong hold tu!
 
Hatuna pesa za kupotezea baharini kiholela. Huu mpango usitishwe mara moja!
 
Hili wazo nilikuwa nalo miaka kibao ila kama wameamua Safi sana

Golden Gate Bridge [emoji563] lina miaka 86 tangu lijengwe, kwa hiyo sisi bado tuko nyuma sana maana hatujui hata matumizi ya ardhi na hata maji

Leo hata mito yetu ingetumika sana kwa kusafirisha mbogamboga na matunda ila unaambiwa usisigee sijui mita ngapi
Wakati wenzetu duniani wanaitumia kwa umwagiliaji na Usafiri

Naona Mchina anatuamsha
 
Hilo daraja halina tija yoyote ile kwa Watanganyika. Kama Wazanzibari wanaweza kujenga kwa gharama zao ili waje Tanganyika kwa urahisi, wajenge.
kwa kuwa rais katoka kule usishtuke mpaka tumefika kusikia wimbo huu, wa kujipendekeza wapo biz kuzifukuzia fursa za teuzi. Hakuna tofauti na wale waliojipendekeza kujenga airport na vinginevyo kijijini Chato.
 
Yaani tunaweza kujenga Daraja la Matrilioni lakini tunashindwa kujenga japo IRRIGATION SCHEME japo moja kwa kila KATA ya nchi hii na tunadai KILIMO cha UTI WA MGONGO...

Viongozi hawana mpango wa kuinua Uchumi wa Wananchi.... Madaraja hata yajae nchi nzima kama Wananchi hawana hela ni kazi bure...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…