Kampuni ya Adani yasaini Mkataba wa miaka 30 kuendesha Gati ya 2 ya Bandari (Zamani TICTS)

PHD za shukrani kwa kuwauzia nchi, unauza bandari alafu unarudi kwa wananchi kuendelea kuwakamua zaidi tozo Kila sehemu nasikia Kuna tozo ya Kila lakini ya simu na vingamuzi inakuja.
Unajua maana ya neno kuuza?, ni ubia wa kibiashara na dunia nzima upo.

DP World anaendesha bandari za London na Southampton na huko UK wameuza bandari zao kwa mwarabu? Stupid argument.
 
Nimepitia kwa haraka haraka Adani ataendesha hiyo gati kupitia TICTS maana ndiye ana mitambo na muajiri mkuu 😃 Karamagi bado anaendelea kulisongesha gurudumu 🔥🔥🔥
TICTS aliyeondoshwa tangu 2021 itakuwa aliyeandika hilo andiko hana taarifa kamili.

Alizingua kwenye mikataba na akapigwa chini na ndiye aliyekuwa nyuma ya malalamiko mengi ya maaskofu kupinga uwekezaji mzima wa DPW Hapo TPA.
 
..bandari ya Dsm ingekuwa uchochoro Dp world wasingevutiwa nayo.

..maadamu Dp world na Adani wamepewa kazi hapo bandarini tunahitaji kuona matokeo chanya.

..tunatarajia Dsm ndio iwe bandari bora ktk Pwani ya Afrika Mashariki.
Muwe muda wa kufanya kazi ya kina pia muepuke kuwa wasambazaji wa maneno ya roho mbaya na vinyongo.
 
Je tuna taarifa hizi au tunafunga macho

Dark side of Adani, the Indian tycoon linked to controversial JKIA deal

Adani Group has been subject to multiple government investigations ... Dark side of Adani, the Indian tycoon linked to controversial JKIA deal.
Parliament of Australia
www.aph.gov.auPDF
A short history of corruption, destruction and criminal activity. adanifiles.com.au


Adani is an Indian mining and energy company seeking to build the world's biggest new coal mine in central Queensland's Galilee Basin — the Carmichael mine.





X
· x.com
Dark side of Adani, the Indian tycoon linked to controversial JKIA deal


Dark side of Adani, the Indian tycoon linked to controversial JKIA deal Dark side of Adani, the Indian tycoon linked to controversial JKIA deal.
 
Kwani kuuliza kwanini mapadri hawatowa waraka kwa hawa wahindi ni udini?

Mimi nadhani haelewi kuwa udini unamaanisha Waislam tu.
 
Kila mtu ana his dark side maishani including wewe mwenyewe. Kinachotakiwa ni namna gani una deal na dark side.

Ingekuwa dark side ya Adani ni shida basi asingekuwa second top Billionaire in India
 
Sasa hiyo ndiyo rekodi mbaya? Au huo ndiyo msuli na uwezo wa biashara. Mimi naiona ni positive aspect. Haji Tanzania kama limbukeni wa biashara
Sidhani kama unaelewa cash flow nchi iliyogawa bure kwenye hii mikataba.

Hii mikataba ya Ambani itawatesa watanzania wenye akili mbele.

Mtu kama wewe ata ukianbiwa TPA kipindi cha Magufuli walikuwa wanatoa gawio la karibu billlion 500 na mwaka huu wametoa billion 150 tu.

Magufuli kaondoka kawaongezea kina cha bahari ili kupokea meli kubwa na kuwekeza kwenye ‘ganch to port cranes kwenye magati sita’ angekuwa yupo hai sasa hivi TPA gawio lingekuwa trillion.

Ni bahati mbaya chuki zidi ya Magufuli zimefunika macho yenu ya ukweli, leo mnatetea mikataba ya miaka 30 kwa mtaji wa million 500 hiyo ni DPW na uwekezaji wao kweli ungeongeza ufanisi ila TPA inalipa hilo deni kwa miaka mitatu tu na kuwapa uvunaji labda wa miaka 4, mkataba miaka 30.

Watu kama nyie mnashida kubwa sana hata sijui mnasaidiwa vipi.

Huyo mama anauza nchi

Ukifikiria na misitu anayotoa kwa mamlaka za serikali na kuwapa waarabu kuvuna faida za Carbon trade wao.

Bado kuna mapori tengefu keshagawa kimya kimya yenye madini watu wanachimba huko Singida, haitoshi kwake sasa hivi anataka kugawa mbuga wakachimbe bila ya kufanya ‘environmental impact assessment’.

Yaani hana huruma hata chembe na mali za Tanganika na ndio nyumbani kwake (huyo mzanzibari jina tu).

It’s beyond me watu mnaotetea upuuzi unaondelea kwenye hiyo nchi.
 
Kila mtu ana his dark side maishani including wewe mwenyewe. Kinachotakiwa ni namna gani una deal na dark side.

Ingekuwa dark side ya Adani ni shida basi asingekuwa second top Billionaire in India
Kama ana vuna kutoka kwenye nchi zisizo na utawala Bora , ataacha kuwa katika ngazi hiyo .na ni watu wengi tu wanatajirika, sababu ya mikataba ya namna hiyo, ndio maana tumeona ya Yule singha singha WA iptl, n.k
 
Achana na magawio FEKI ya Magufuli marehemu mpika takwimu. Wakati wa Magufuli hata TTCL na MNH walikuwa wanatoa GAWIO wakati walikuwa wana operate kwa hasara au taasisi huduma . Nonsense

Ni msitu gani ametoa? Sema tu wewe ni mbumbumbu wa biashara ya carbon credit na hunting.

Hakuna mtu anaweza kuuza ardhi ya Tanzania kwa vile ardhi ya Tanzania ni mali ya Serikali, wananchi au wawekezaji kukodishwa kwa kipindi maalum. Team Wapotoshaji HOVYO
 
Kama ana vuna kutoka kwenye nchi zisizo na utawala Bora , ataacha kuwa katika ngazi hiyo .na ni watu wengi tu wanatajirika, sababu ya mikataba ya namna hiyo, ndio maana tumeona ya Yule singha singha WA iptl, n.k
Kwanini sasa tusitumie mtaji wake kupiga hatua??
 
Karamagi na Manek, ndiyo wametuletea bilionea wa India bwana Adani au wao wenyewe wamejibadolisha status na kununia hisa za kwenye kampuni tanzu ya Adani TZ Ltd.Hakuna jipya
 
Ni vigumu mtu wa kawaida kuelewa nini kinaendelea kwenye huu mchezo wa kununuana makampuni kupeana gati etc etc. Mwisho wa yote ni nchi kuumizwa. Hapo hao DPW tuliyoambiwa ndio wamepewa kandarasi ndio kusema wao wanatoa tena kandarasi kwa kampuni zingine?..Na jina la TPA linatumika? Yaani ni ubabaishaji mtu kwa vile vigogo wanajidai nchi haina uwezo na wanakabidhi uwekezaji za nchi kuvunwa na wageni ili mradi wao wanajaza matumbo yao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…