Kampuni ya ElSewedy Electric Co inayotengeneza bwawa la umeme Rufiji imewekewa vikwazo, haitaweza kukopesheka nje

Daah tumekwisha Ndege ndio hizo zimedorora Stiglers nayo ndio hiyo kilichobakia ni Sgr hii ni mikosi ya kujitakia ya kumpiga Tundu Lissu risasi
Kumbe haya makampuni hayana uwezo wa kifedha, yanategemea kukopa toka kwa mabeberu. Nilijiuliza sana hawa waarabu utaalamu wa kujenha haya majitu makubwa hivi na expertise ya hali ya juu wameutoa wpi? Kumbe ni ubia na wazungu.....Norwegians ambao wako juu sana katika oil and gas exploration ... ambayo inajumuisha na vitu kama dams etc etc!
Hoja yangu, why not go to Norway directly ukawapa tender ya kujenga mradi huo? I stand to be corrected! It seems to me, huyu Elsawedy ni middle man ?????
 
Aisee tafadhali sana. ACHA KUMUITA MHESHIMIWA "TAUSI" [emoji2]
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kampuni ya Elsewedy Electic ya Misri inayojenga bwawa la umeme Rufiji imewekewa vikwazo kuweza kupata mikopo kwa sababu ya ushiriki wake kwenye ujenzi wa hilo bwawa.

Inatuhumiwa kushirikiana na serikali ya Tanzania kuharibu mojawapo ya hifadhi chache za asili zilizosalia Duniani ya Selou.

Hii inaweza kupelekea kukosa mikopo ya nje ya kugharamia mradi wa Umeme(Stiglers Gorge) ambao serikali yetu inautekeleza.

ElSewedy Electric Co - Council on Ethics
 
Mkataba ni kati yetu sisi na Elsewedy mkataba kati ya Elsewedy na wafadhili wake ambao mojawapo ni sweden sisi hautuhusu.
Ni wajibu wa Elsewedy kutafuta mfadhili mwingine ili wakamilishe mradi wetu tuwalipe chao.
Kama umewahi kujenga mradi wowote kwa kupitia kampuni utaelewa kuwa mkataba wa kampuni na wafadhili wake wewe haukuhusu.
Isitoshe mradi wa Stiglers unajengwa na kampuni mbili tanzu, iwapo Elsewedy watashindwa kupata mfadhili mradi utaendelea japo utachelewa kukamilika.
Naona wachangiaji wengi wamechangia kwa chuki kiasi cha kupofusha uwezo wao wa kupambanua mambo madogo kama haya.
Kufurahia kufeli kwa huu mradi ni upumbavu mkubwa kwasababu huu mradi sio JPM ni mradi wa Watanzania wote na vizazi vijavyo.
 
Nimeona hiyo. Wanatuhumu kuhusika kuharibu mazingira! Jiwe kuna janga anatutafuta siyo bure. Brazil wangetaka basi kule Amazon wangezalisha malaki ya megawatt za umeme ila wanaiangalia dunia.
 
Norges bank ni Norwegian bank sio Sweden bank.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…