Kampuni ya HBO ya Marekani kuwalipa wasanii wa Bongo Fleva, Soggy Doggy na Dataz Tsh. Milioni 700

Wild Flower

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2023
Posts
378
Reaction score
766
Kampuni ya Home Box Office (HBO) ya Marekani kuwalipa wasanii, Soggy Doggy na Dataz, kiasi cha Tsh Milioni 700 kwa kutumia wimbo wao "Sikutaki Tena" katika filamu ya "Sometimes In April" bila makubaliano.

Hukumu hii imetolewa Julai 26, 2024, katika Mahakama Kuu ya Tanzania, kanda ya Dar es Salaam. Wasanii hao waliwakilishwa na kampuni ya Markel Advocates, na kesi hiyo imeendeshwa kwa miaka 4.

Wimbo wa "Sikutaki Tena" ulitolewa mwanzoni mwaka 2000 na kurekodiwa katika Studio za Soundcrafters chini ya utayarishaji wa Enrico.
 
Great news kwa Soggy, hakika hii itakuwa ni malipo stahili kwa hustle zake. Mwamba masimulizi yake husema kuna siku alilipwa sh milioni sijui tatu huko mwanza hakuamini kwa sababu show zake daima ilikuwa ni sh laki moja na nusu humo. Hatimaye mziki umemlipa sawa na hadhi yake.
 
Sasa hapo atalipwa vipi na hiyo ofc ilikuwa inawakilishwa na nani huku kwenye mahakama zetu.
 
Kwanza kabisa hukumu imetolewa mahakama ya Tanzania, kampuni ya Kimarekani.

Una enforce vipi hukumu ya madai iliyopitishwa na mahakama ya Tanzania kwenye kampuni ya Kimarekani ambayo haina biashara Tanzania?
Ungeelewa hili ila mnasemaga sheria ngumu ukisoma sheria kuna course inaitwa private international law specifically kwenye recognition and enforcement of foreign judgement kama hizi nchi mbili wana makubaliano ya kurecognise na kuenforce simple tu watapata haki yao
 
Great news kwa Soggy, hakika hii itakuwa ni malipo stahili kwa hustle zake. Mwamba masimulizi yake husema kuna siku alilipwa sh milioni sijui tatu huko mwanza hakuamini kwa sababu show zake daima ilikuwa ni sh laki moja na nusu humo. Hatimaye mziki umemlipa sawa na hadhi yake.
Great news kwa Soggy au Dataz?! Nauliza kwa sababu naona Soggy ni kama ameshirikishwa tu!
 
Back
Top Bottom