Kampuni ya HBO ya Marekani kuwalipa wasanii wa Bongo Fleva, Soggy Doggy na Dataz Tsh. Milioni 700

Kampuni ya HBO ya Marekani kuwalipa wasanii wa Bongo Fleva, Soggy Doggy na Dataz Tsh. Milioni 700

Kwanza kabisa hukumu imetolewa mahakama ya Tanzania, kampuni ya Kimarekani.

Una enforce vipi hukumu ya madai iliyopitishwa na mahakama ya Tanzania kwenye kampuni ya Kimarekani ambayo haina biashara Tanzania?
Hata mimi ndio nashangaa kampuni iko marekani unaishtaki kwenye mahakama ya Tanzania hapo kuna muingiliano gani.
 
Sasa assume kesi imeisha na mahakama imeamuru hiyo kampuni ilipe halafu kwa mfano wakashindwa kulipa mtawafanya nini?maana hawana assets zozote Tanzania

Mbona unaashumu kushindikana tu? Kwanini usiashumu kulipwa haraka bila mkwamo? Wale sio waswahili they have got reputation to protect, payment is swift and instant after exhausting all possible legal avenues.
 
Ungeelewa hili ila mnasemaga sheria ngumu ukisoma sheria kuna course inaitwa private international law specifically kwenye recognition and enforcement of foreign judgement kama hizi nchi mbili wana makubaliano ya kurecognise na kuenforce simple tu watapata haki yao
Nakwambia hivii, hapo Tanzania tu watu wanashinda kesi za madai na hawapewi haki zao, itakuwa huko nje ambako hata hiyo recognition of foreign judgement uliyoitaja hujui kama ipo na kama ipo ipo vipi?

Wamarekani wana visa sana kwenye sheria, wanajiona mfumo wao tu ndio unatoa haki huko kwingine kote takataka, wanakataa hata sheria za kimataifa kuwahusu askari wao wanaofanya vibaya vitani, itakuwa hizo sheria za Tanzania ambazo wao wanaona zinatoka kwenye mahakama za kufuata amri kutoka juu?

Hiyo kampuni ingeshitakiwa kwenye mahakama ya Marekani kungekuwa na uwezekano mkubwa wa kulipa.

Hizi mahakama za Tanzania Mmarekani akisema tu nimeonewa kwa sababu wamemtetea mtu wao kwao kinyume na haki hukumu haina nguvu Marekani hiyo.

Mpaka hapa kila kitu nimeandika kutoka kichwani kwa uzoefu wangu wa kufuatilia mambo tu.

Sasa naweka references za kisheria, yafuatayo si yangu tu, ni sheria.

Uzuri wa Marekani kila kitu kipo mtandaoni. Nimeona nisiandike kutoka kichwani tu, nikupe sheria ya Marekani inavyosema.

Wanasema hivii.

"Under U.S. law, an individual seeking to enforce a foreign judgment, decree or order in this country must file suit before a competent court."

"The United States is not party to any treaty on the recognition and enforcement of foreign judgments, nor are there federal laws governing foreign judgments."





Maana yake ukitaka ku enforce judgement, decree au order ya mahakama ya nje nchini Marekani, inabidi u file suit upya Marekani.
 
Hata mimi ndio nashangaa kampuni iko marekani unaishtaki kwenye mahakama ya Tanzania hapo kuna muingiliano gani.
Marekani haitambui hukumu za mahakama za nchi nyingine mpaka mdai afungue kesi upya katika mahakama competent ya Marekani na kushinda tena huko.

Haijasaini mkataba wowote wa kutambua hukumu za mahakama za nchi za kigeni.
 
Court broker tutaenda ata uko marekani kukamata Mali zao
Marekani haitambui hukumu za mahakama za kigeni, haijasaini mkataba wa kutambua hukumu hizo.

Ili hukumu hizo ziwe valid, kesi mpya inatakiwa kuanzishwa nchini Marekani kwenye mahakama yenye nguvu stahiki za kuisikiliza.

Ukipeleka court brokers wako wa Tanzania washike mali bila kufungua kesi upya Marekani utaonekana mwizi tu na hata shaba wanaweza kupigwa kama wezi tu.
 
Marekani haitambui hukumu za mahakama za kigeni, haijasaini mkataba wa kutambua hukumu hizo.

Ili hukumu hizo ziwe valid, kesi mpya inatakiwa kuanzishwa nchini Marekani kwenye mahakama yenye nguvu stahiki za kuisikiliza.

Ukipeleka court brokers wako wa Tanzania washike mali bila kufungua kesi upya Marekani utaonekana mwizi tu na hata shaba wanaweza kupigwa kama wezi tu.
Hatari,kweli uko ndio duniani,uku kwetu court broker wanadaka ata ndege za serikali
 
Back
Top Bottom