beefinjector
JF-Expert Member
- Jul 23, 2009
- 2,458
- 2,496
Kama ni mahakama ya Tanzania hawapati hiyo hela.Kampuni ya Home Box Office (HBO) ya Marekani kuwalipa wasanii, Soggy Doggy na Dataz, kiasi cha Tsh Milioni 700 kwa kutumia wimbo wao "Sikutaki Tena" katika filamu ya "Sometimes In April" bila makubaliano.
Hukumu hii imetolewa Julai 26, 2024, katika Mahakama Kuu ya Tanzania, kanda ya Dar es Salaam. Wasanii hao waliwakilishwa na kampuni ya Markel Advocates, na kesi hiyo imeendeshwa kwa miaka 4.
Wimbo wa "Sikutaki Tena" ulitolewa mwanzoni mwaka 2000 na kurekodiwa katika Studio za Soundcrafters chini ya utayarishaji wa Enrico.
Hizo ni ndoto.Ungeelewa hili ila mnasemaga sheria ngumu ukisoma sheria kuna course inaitwa private international law specifically kwenye recognition and enforcement of foreign judgement kama hizi nchi mbili wana makubaliano ya kurecognise na kuenforce simple tu watapata haki yao
Kwani kishalipwa?Hbo walikuwa na wanasheria wao toka ofisi zao south Afrika. Mna wivu mzee soggy kapata kibunda
Sio lazima. Kesi ya madai inaweza kuendeshwa na upande mmoja wa wadai na hukumu kutolewa bila ya wadaiwa kuwepo.Kama kesi imeendeshwa miaka minne lazima jamaa itakuwa walikua wanakuja.
Mahakama za Tanzania hazina nguvu ya kisheria Marekani. HBO kamwe hawawezi kulipa hizo hela kwa hukumu iliyotolewa Tanzania. Kina Soggy wangekuwa wajanja wangefungua hiyo kesi Marekani kama alivyofanya P Funk.Mbona unaashumu kushindikana tu? Kwanini usiashumu kulipwa haraka bila mkwamo? Wale sio waswahili they have got reputation to protect, payment is swift and instant after exhausting all possible legal avenues.
Hivyo wanaweza kutumia hukumu ya huku kufile upya ikatumika kama rejea. Halafu kama nyimbo ni yao na kweli ilitumika bila makibaliano wenzetu hawanaga shida sana, unless kuwe na picha picha au janja janja.Nakwambia hivii, hapo Tanzania tu watu wanashinda kesi za madai na hawapewi haki zao, itakuwa huko nje ambako hata hiyo recognition of foreign judgement uliyoitaja hujui kama ipo na kama ipo ipo vipi?
Wamarekani wana visa sana kwenye sheria, wanajiona mfumo wao tu ndio unatoa haki huko kwingine kote takataka, wanakataa hata sheria za kimataifa kuwahusu askari wao wanaofanya vibaya vitani, itakuwa hizo sheria za Tanzania ambazo wao wanaona zinatoka kwenye mahakama za kufuata amri kutoka juu?
Hiyo kampuni ingeshitakiwa kwenye mahakama ya Marekani kungekuwa na uwezekano mkubwa wa kulipa.
Hizi mahakama za Tanzania Mmarekani akisema tu nimeonewa kwa sababu wamemtetea mtu wao kwao kinyume na haki hukumu haina nguvu Marekani hiyo.
Mpaka hapa kila kitu nimeandika kutoka kichwani kwa uzoefu wangu wa kufuatilia mambo tu.
Sasa naweka references za kisheria, yafuatayo si yangu tu, ni sheria.
Uzuri wa Marekani kila kitu kipo mtandaoni. Nimeona nisiandike kutoka kichwani tu, nikupe sheria ya Marekani inavyosema.
Wanasema hivii.
"Under U.S. law, an individual seeking to enforce a foreign judgment, decree or order in this country must file suit before a competent court."
"The United States is not party to any treaty on the recognition and enforcement of foreign judgments, nor are there federal laws governing foreign judgments."
Enforcement of Judgments
In many foreign countries, as in most jurisdictions in the United States, the recognition and enforcement of foreign judgments is governed by local domestic law and the principles of comity, reciprocity and res judicata (that is, that the issues in question have been decided already).travel.state.gov
Enforcement of Foreign Judgments Laws and Regulations Report 2024-2025 United States
Enforcement of Foreign Judgments Laws and Regulations covering issues in United States of Country Finder, General Regime, Enforcement, Other Mattersiclg.com
Maana yake ukitaka ku enforce judgement, decree au order ya mahakama ya nje nchini Marekani, inabidi u file suit upya Marekani.
Sio lazima. Kesi ya madai inaweza kuendeshwa na upande mmoja wa wadai na hukumu kutolewa bila ya wadaiwa kuwepo.
Kwani kishalipwa?
Endeleeni kuota.Wewe unaongea kujifurahisha tu hata hujasikiliza taarifa iliyotolewa. Kama unaumia kijana kula m700 shauri yako. Hakuna utachofanya penda usipende keshakula tuzo na hbo wanalipa hawana mba mba mba
Naomba kujuzwa hapa,kama HBO walijua/wanajua hukumu yeyote huku Bongo Haina impact kwao huko USA kwanini ndani ya miaka yote 4 walikuwa wanahudhuria mahakamani kupitiwa wanasheria wao.Kushinda kesi Tanzania hakuna bearing katika kampuni ya Kimarekani.
Marekani haitambui hukumu za nchi za kigeni mpaka kesi irudiwe tena Marekani na mdai ashinde upya.
Tanzania yenyewe haina mambo mengi sana ya sheria kwenye nyanja hizi za burudani.
🤣🤣Wewe wakati waendelea kushangaa wenzako HBO wako serious walihudhuria kesi, mawakili wake walikuja.
Kwa nini unachukulia kwamba HBO ni wahuni wahuni tu?Naomba kujuzwa hapa,kama HBO walijua/wanajua hukumu yeyote huku Bongo Haina impact kwao huko USA kwanini ndani ya miaka yote 4 walikuwa wanahudhuria mahakamani kupitiwa wanasheria wao.
Si wangeuchuna tu huko kwani chochote kitakachoamuliwa hakuna madhara kwao?
Sijawachukulia wahuni nimeuliza ili nipate uelewa wa kisheria.Kwa nini unachukulia kwamba HBO ni wahuni wahuni tu?
HBO wanaweza kuleta wanasheria wao Tanzania kujifunza sheria za Tanzania tu. Yani wakaitumia hii kesi kama darasa la kujifunza sheria za Tanzania kwa projects zao za baadaye.
After all, gharama walizotumia kuleta wanasheria wao kwenye kesi hii tayari zitakuwa zishazidi hiyo pesa inayodaiwa $250,000.
Kampuni kubwa zina sababu nyingi za kumaliza kesi kwa kutumia mifumo rasmi, badala ya kukimbia kesi.Sijawachukulia wahuni nimeuliza ili nipate uelewa wa kisheria.
Hiyo ya kuleta wanasheria huku ili wajifunze ni assumptions zako au ndo wao wamesema walikuja kujifunza Sheria za Bongo?
Last paragraph, wameuza Mbuzi kwa kesi ya kuku.
Kuna mdau kasema mwanzo walikubali kumaliza hili swala nje ya mahakama lakini kiwango walichooffer kwa kina Soggy ni kidogo ndo maana waliamua kwenda Mbele