Kampuni ya PAF Promotion yampeleka Mahakamani Mwakinyo, yamdai fidia ya mamilioni

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Kesi dhidi ya bondia wa ngumi za kulipwa Nchini, Hassan Mwakinyo ambayo imefunguliwa na Kampuni ya PAF Promotion inatarajia kutajwa kwa mara ya kwanza Novemba 13, 2023 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu, A.H. Msumi ikiwa na jumla ya madai 8 ya msingi.

Kampuni hiyo imewasilisha madai hayo kupitia wito wa kesi uliotolewa na Mahakama ambapo PAF imeiomba Mahakama itamke kwamba bondia huyo amevunja mkataba wa kupigana.

Madai ya pili, PAF imeiomba Mahakama kumtaka Mwakinyo aombe radhi kwa kuichafua kutokana na kutoa taarifa za uongo kupitia Vyombo vya Habari alivyotumia kuichafua Kampuni na Wakurugenzi wake.

Madai ya tatu, PAF imeiomba Mahakama ilipwe fidia ya Shilingi 142,500,000 (Milioni 142.5) kutokana na hasara ya kukosa mapato iliyotegemea kutoka kwa wadhamini.

Madai ya nne, imeiomba Mahakama kumtaka Mwakinyo arejeshe fedha Dola za Marekani 3,000 alizopewa kuelekea pambano hilo alilotakiwa kupigana.
Mwakinyoo.jpg

Madai ya tano, PAF imeomba kurejeshewa Shilingi Milioni 8 yakiwa ni malipo ya kulipia ukumbi.

Madai namba sita, PAF imeomba kurejeshewa Shilingi 1,287,500 ikiwa ni gharama za malazi ya mpinzani wa bondia huyo.

Madai namba saba, PAF imeomba kurejeshewa Shilingi 3,832,000 ambayo ni gharama za tiketi za ndege za mpinzani wake pamoja na Wasaidizi wake.

Aidha, mbali ya madai hayo, PAF kupitia wakili wake, Herry Kauki wa Kampuni ya Wakili ya Shepron Attorneys ya Dar es Salaam, imeomba Mahakama kulipwa jumla ya Shilingi milioni 150 ikiwa ni madhara ya jumla waliopata baada ya bondia huyo kushindwa kupanda ulingoni tofauti na mkataba wake aliosaini.

Ikumbukwe Septemba 29, 2023, Mwakinyo hakupanda ulingoni katika pambano lililoandaliwa na PAF kwa kile alichonukuliwa akisema ni waratibu hao kukiuka masharti.

Chanzo: boxinghubtz
PIA SOMA
- Bondia Hassan Mwakinyo amepata pigo la kwanza katika kesi aliyofunguliwa na Promota

- Hatimaye wakili wa Mwakinyo kafika mahakamani leo
 
Kesi dhidi ya bondia wa ngumi za kulipwa Nchini, Hassan Mwakinyo ambayo imefunguliwa na Kampuni ya PAF Promotion inatarajia kutajwa kwa mara ya kwanza Novemba 13, 2023 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu, A.H. Msumi ikiwa na jumla ya madai 8 ya msingi.

Kampuni hiyo imewasilisha madai hayo kupitia wito wa kesi uliotolewa na Mahakama ambapo PAF imeiomba Mahakama itamke kwamba bondia huyo amevunja mkataba wa kupigana.

Madai ya pili, PAF imeiomba Mahakama kumtaka Mwakinyo aombe radhi kwa kuichafua kutokana na kutoa taarifa za uongo kupitia Vyombo vya Habari alivyotumia kuichafua Kampuni na Wakurugenzi wake.

Madai ya tatu, PAF imeiomba Mahakama ilipwe fidia ya Shilingi 142,500,000 (Milioni 142.5) kutokana na hasara ya kukosa mapato iliyotegemea kutoka kwa wadhamini.

Madai ya nne, imeiomba Mahakama kumtaka Mwakinyo arejeshe fedha Dola za Marekani 3,000 alizopewa kuelekea pambano hilo alilotakiwa kupigana.
View attachment 2792048
Madai ya tano, PAF imeomba kurejeshewa Shilingi Milioni 8 yakiwa ni malipo ya kulipia ukumbi.

Madai namba sita, PAF imeomba kurejeshewa Shilingi 1,287,500 ikiwa ni gharama za malazi ya mpinzani wa bondia huyo.

Madai namba saba, PAF imeomba kurejeshewa Shilingi 3,832,000 ambayo ni gharama za tiketi za ndege za mpinzani wake pamoja na Wasaidizi wake.

Aidha, mbali ya madai hayo, PAF kupitia wakili wake, Herry Kauki wa Kampuni ya Wakili ya Shepron Attorneys ya Dar es Salaam, imeomba Mahakama kulipwa jumla ya Shilingi milioni 150 ikiwa ni madhara ya jumla waliopata baada ya bondia huyo kushindwa kupanda ulingoni tofauti na mkataba wake aliosaini.

Ikumbukwe Septemba 29, 2023, Mwakinyo hakupanda ulingoni katika pambano lililoandaliwa na PAF kwa kile alichonukuliwa akisema ni waratibu hao kukiuka masharti.
Mbombo ngafu
 
Hawa waliofungua kesi ni wajinga, yaani mtu umemlipa dola 3000 halafu unataka akurejeshee dola 50,000+ hapo wataambulia Dola 3000 tu na gharama za kesi, waache utapeli na wakumbuke kesi ya Madai hafungwi mtu, na kila biashara inapaswa iwe na Bima kuensure unforeseen liabilities kama hizi, kwahiyo wakawadai kampuni yao ya Bima.
 
Kuna kitu hujakielewa bado.,iko hivi yule bwana mdogo aliingia vibaya sehemu hivyo atapatikana na kila aina ya kosa,kila aina ya fidia
SIendeshwi na Chuki, if jambo litaamuliwa mahakamani.
Mwakinyo atashinda hiyo kesi, imekaa kipumbavu na imefunguliwa na watu wapumbavu.
Ikimuendea vibaya sana ni kurudisha hiyo 3k.
 
Sheria haiko hivyo mkuu lazima alipe cost zote ambazo kampuni imeingia
Hajui kwamba huko Mahakamani kuna kulipa Gharama, kulipa Faini na Kulipa Fidia....,.yote huzingatiwa kulingana na Kesi...

Mwankinyo kwenye kulipa Gharama na Fidia kwa kusababisha Hasara na usumbufu kwa walalamikaji hachomoki kama alikiuka mkataba.

Atawajibika kwa Upumbavu wake...

Sent from my M10_Max using JamiiForums mobile app
 
Sheria haiko hivyo mkuu lazima alipe cost zote ambazo kampuni imeingia
Kutokana na janja janja za bongo Itakua ngumu kuproove kwamba wanaoiwezo wakuingiza hela zote hizo, hapo itaombwa financial statement ya hiyo kampuni na mwenendo wao wa kulipa kodi unakuta hawajawahi kudeclare profit wala kuingiza zaidi ya Million 50.
 
[emoji23][emoji23][emoji23]
Thamani ya mkataba million 6.
Fidia unataka karibu Nusu billion
Tuache masihara kama Mwakinyo wanampa million 6, hao mabondia wengine wanapewa Tsh ngapi?
Magumi yote yale?
Atajifunza na kuelewa thamani ya Mkataba ni nini!? Watu wanaweka Hela kuvuna mabilioni sio ujinga ....Atalipa Gharama ya upuuzi wake.

Sent from my M10_Max using JamiiForums mobile app
 
[emoji23][emoji23][emoji23]
Thamani ya mkataba million 6.
Fidia unataka karibu Nusu billion
Tuache masihara kama Mwakinyo wanampa million 6, hao mabondia wengine wanapewa Tsh ngapi?
Magumi yote yale?
Ushangai Nchi yako ikikiuka mikataba inavyolipishwa Mabilioni 300 na ujinga, unashangaa ya Mwankinyo!!!

Hapa atajifunza ...kapitishwa njia Ngumu hata kaa haamini ....mjinga yule

Back
Top Bottom