Kampuni ya utalii yapigwa faini kwa kuwaruhusu Watalii kula hadharani Zanzibar

Kamisheni ya Utalii Zanzibar imethibitisha kuipiga faini ya dola 500 kampuni ya utalii ya Organisateur Francophone Tours and Travel kwa kuruhusu watalii kula hadharani katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhan.

Katika taarifa Afisa wa Uhusiano wa Tume ya Utalii Zanzibar Mohamed Nassor Bajuni alisema kampuni hiyo ilikiuka miongozo na maagizo yaliyotolewa kwa wafanyabiashara wa utalii wakati huu wa mfungo wa Ramadhani.

''Toka kuanzishwa kwa kamisheni huo tunatoa notisi maalumu kwa kipindi cha mwezi wa Ramadhani kuhusiana na suala hili'' alisema Bw.

Muongoza watalii wa kampuni hiyo, Khamis M. Kahogo pia amezuiliwa kufanya shughuli zozote za utalii kwa muda wa miezi mitatu," aliongeza kusema.

Kamisheni hiyo imesisitiza umuhimu wa kufuata desturi na mila za visiwa vya Zanziba hasa wakati huu wa mfungo wa Ramadhan.
kwa nini hawajakamata Watalii?
 
Imani na na matendo ya imani kwa Mungu wa kweli haihitaji kutumia nguvu za kimwili. Kufunga kwa ajili ya mambo ya kiroho kunahitajika imani na uvumilivu. Ni kujizuia kula kwa muda uliopanga wewe binfsi au kupangwa na dini au madhehebu yako. Haijalishi utakiona chakula mbele yako au utamwona mtu akila mbele yako. Wala hutakiwi kumshutumu au kumlaumu anayekula, kwani yeye hiyo funga haimhusu, inakusuhu wewe. Unachotakiwa ni kuonyesha ukomavu wako wa imani, kwamba pamoja na kusikia harufu nzuri ya chakula au kukiona chakula mbele yako, kamwe hutashawishika kutamani kula. Unatakiwa ushinde hilo jaribu.

Mimi nikiamua kufunga hamu ya chakula huwa inapotea kabisa, hata nikimwona mtu anakula siwezi kukwazika au kutamani kula kwa namna yoyote hadi nimalize funga yangu.
Wanakula usiku wa manane, asubuhi wanasikia njaa😂
 
Kwa hiyo kula chakula polisi ziwani mchana kweupe , pale,magereza mchana kweupe na nyuki mchana kweupe nk eneo la wazi ni kula sirini mwezi wa Ramadhani?
Watu wanakula na kunywa maeneo hayo ila huwez kuona mtu kakamatwa humo ndani.
 
Kula nyumbani kwako huguswi. Wakiristo wa Zanzibar wanajifanya kama siasa za Chama tawala na upinzani kwamba nitafanya maandamano hufanyi. Dawa yao ni hiyo tu ukila hadharani
 
Kamisheni ya Utalii Zanzibar imethibitisha kuipiga faini ya dola 500 kampuni ya utalii ya Organisateur Francophone Tours and Travel kwa kuruhusu watalii kula hadharani katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhan.
........''Toka kuanzishwa kwa kamisheni huo tunatoa notisi maalumu kwa kipindi cha mwezi wa Ramadhani kuhusiana na suala hili'' alisema Bw.

Muongoza watalii wa kampuni hiyo, Khamis M. Kahogo pia amezuiliwa kufanya shughuli zozote za utalii kwa muda wa miezi mitatu," aliongeza kusema.

Kamisheni hiyo imesisitiza umuhimu wa kufuata desturi na mila za visiwa vya Zanziba hasa wakati huu wa mfungo wa Ramadhan.
Inamaana ZNZ ni nchi kamili? masuala ya union matter inaanzaje kuyatolea matamko zuio na adhabu,au kampuni na watalii wote ni wa ndani?
 
Imani na na matendo ya imani kwa Mungu wa kweli haihitaji kutumia nguvu za kimwili. Kufunga kwa ajili ya mambo ya kiroho kunahitajika imani na uvumilivu. Ni kujizuia kula kwa muda uliopanga wewe binfsi au kupangwa na dini au madhehebu yako. Haijalishi utakiona chakula mbele yako au utamwona mtu akila mbele yako. Wala hutakiwi kumshutumu au kumlaumu anayekula, kwani yeye hiyo funga haimhusu, inakusuhu wewe. Unachotakiwa ni kuonyesha ukomavu wako wa imani, kwamba pamoja na kusikia harufu nzuri ya chakula au kukiona chakula mbele yako, kamwe hutashawishika kutamani kula. Unatakiwa ushinde hilo jaribu.

Mimi nikiamua kufunga hamu ya chakula huwa inapotea kabisa, hata nikimwona mtu anakula siwezi kukwazika au kutamani kula kwa namna yoyote hadi nimalize funga yangu.
Umenena vyema ndugu katika imani.
 
Wewe wacha porojo hizo sheria zipo znz wewe mtanganyika inakuuma kitu gani? Tii sheria bila shuruti huwezi baki kwenu tanganyika
 
Jirani kaamua kushinda na njaa kwa hiari yake,ila anataka na majirani tusile,hizi dini kuna namna tunapaswa kuwa nazo makini.HAWA DINI YAO hata wakibaki wao duniani bado watajitoa muhanga.
Sheria zipo znz wewe mtanganyika inakuuma kitu gani sii ubaki kwenu tanganyika ujinga ni mzigo pole sana
 
Sasa hivi sio polisi chombo cha muungano chini ya katiba ya muungano tena kukamata wala chakula mchana nashukuru polisi Zanzibar kujivua hilo jukumu la kamata wala chakula mchana wameachia hiyo kamisheni ndio wajijue impact yake kwa hatua zao badala ya kulitwika jeshi la polisi zigo mwisho wa siku

Zanzibar kila taasisi ibebe zigo lake

Polisi muungano huo mziki kaeni nao mbali ili hata kesi za katiba zikija msije bebeshwa zigo jumba bovu likawaangukia puuuuuu na IGP wenu

Kila mtu apambane na hali yake asitupie zigo kwa mwingine
Wewe wacha porojo znz wana sheria zao wana serikali yao wana katiba yao kula hadharani mchana wa Ramadhani znz ni kosa la jinai tii sheria bila shuruti huwezi baki kwenu tanganyika
 
Mjinga ni wewe sheria zipo znz wewe mtanganyika inakuuma kitu gani sii ubaki kwenu tanganyika ujinga ni mzigo pole sana
Hizo sheria ni kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar au kuruani?

Kama ni katiba nielimishe...

Kama mumezitoa kitabu kitakatifu nahitaji elimu pia...

Kama hamkuzitoa huko nataka kujua nyinyi ni waislam safi kuliko Saudia au Dubai?
 
Paragraph ya mwisho imemaliza mzizi wa fitna.
 
Back
Top Bottom