Jamani jamani msirukie mambo tu! Hakuambiwa mtu yeyote yule afunge! awe muislamu, mkristo, baniani, pagani au mtalii akitaka kula na ale. Kilichokatazwa ni kula HADHARANI tu! Au wenzetu hamfahamu maana ya neno HADHARANI?
Funga ya waislam ni kutokula mchana,kwa hiyo wamechagua mchana ili kukabiliana na vishawishi sasa inakuwaje tena hawataki vishawishi?maana usiku ni kujiachia tu.
Hivi ndugu yangu ndivyo unavyofahamu maana ya funga ya ramadhani? Unadhani ni kutokula mchana tu na usiku watu wako huru kufanya maasi? Hatukuchagua na wala hatufungi kwa kukabiliana na vishawishi bali ni kujikaribisha zaidi kwa mola wetu. Kuna mambo mengi yanayobatilisha saumu na ambayo tunatakiwa kuyaepuka ikiwa pamoja na hivyo vishawishi unavyovifikiria wewe.