Kampuni ya utalii yapigwa faini kwa kuwaruhusu Watalii kula hadharani Zanzibar

Kampuni ya utalii yapigwa faini kwa kuwaruhusu Watalii kula hadharani Zanzibar

Bila kuathiri mjadala wenu naomba kupinga hoja yako. Kuna waarabu ambao ndo matajiri unaowazungumzia. Utajiri wao hautokani na Imani yao. Na pia sio kipimo cha akili. Top ten za form four na form six zimejaa watu gani? Tuseme pia dini zao zinachangia? Form four Zanzibar matokeo hufananaje ikiwa dini zinachangia akili ya mtu?
Mwisho dini haina uhusiano unaotaka kutuaminisha.
Dini ni Mfumo wa maisha ya binaadamu, dini yao inachangia sana mafanikio yao , akili ni uwezo wa kupambana na mazingira uliyopo siyo vyeti kama wengi mnavyoamini , its about priorities kama unataka kuajiriwa pambana sana na mfumo wa elimu na ufaulu ila wenye akili wengi hawapendi kuajiriwa na tangu mwanzo wa elimu huwa anajitahidi apate elimu ya kuweza kupambana ili amudu biashara zake
Na mfumo wa maisha pia unaekekeza jinsi ya kufanya biashara na miiko ya biashara, jinsi ya kuoa, kurithisha na kadhalika ingawa binaadamu tuna tamaa zetu wale wanaoshika miiko ya biashara kama dini inavyotaka 99% wanafanikiwa
Ndio maana nimemwambia huyo aliyesema waislamu hawana akili nimemwambia wengi wana akili ndio maana wameweza kumudu mazingira yao vizuri kuliko yeye aliyekariri anasubiri kuajiriwa
 
Na wanaofunga London, Stockholm, St. Petersburg, China, India na Brazil wanyongwe pia?
Kwa nini wanyongwe?

Hizo nchi zina uhuru wa kuabudu.

Nchi za kiislamu hazina uhuru wa kuabudu, zinalazimisha kila mtu afuate dini yao.
 
Funga ya waislam ni kutokula mchana,kwa hiyo wamechagua mchana ili kukabiliana na vishawishi sasa inakuwaje tena hawataki vishawishi?maana usiku ni kujiachia tu.
 
Sasa hivi sio polisi chombo cha muungano chini ya katiba ya muungano tena kukamata wala chakula mchana nashukuru polisi Zanzibar kujivua hilo jukumu la kamata wala chakula mchana wameachia hiyo kamisheni ndio wajijue impact yake kwa hatua zao badala ya kulitwika jeshi la polisi zigo mwisho wa siku

Zanzibar kila taasisi ibebe zigo lake

Polisi muungano huo mziki kaeni nao mbali ili hata kesi za katiba zikija msije bebeshwa zigo jumba bovu likawaangukia puuuuuu na IGP wenu

Kila mtu apambane na hali yake asitupie zigo kwa mwingine
Huelewi wewe ulichoandika. Hao kamisheni ya utalii wanashitaki polisi na unachukuliwa au unaitwa polisi na unasomewa vifungu vya sheria ulivyokiuka na unalipa faini na adhabu nyingine kama kufungiwa mwongoza watalii.
 
Allah pia kasema Usiibe fedha za Umma Allah kasema usiibe kura lakini hii Serikali ya Mapinduzi inaangalia tu nani kala nini kajamba wapi...
Kuiba ni kosa kisheria na hukumu ni mahakama. Kula Ramadan mchana siyo kosa ni dhambi na adhabu ni bakora. Ukiiba hupigwi bakora.
 
Mtu akienda kutalii Zanzibar huwa anataka kuona Nini!?
Anyway hope siku Moja wataacha kuhangaika na kwenda mahali salama zaidi kutalii
 
Kwa nini wanyongwe?

Hizo nchi zina uhuru wa kuabudu.

Nchi za kiislamu hazina uhuru wa kuabudu, zinalazimisha kila mtu afuate dini yao.
Nilikuwa nampa changamoto ya ukali wake wa kutaka watu wanyongwe kisa kula. Na hapo kuna nchi zina Waislam wachache kama ilivyo Zanzibar kuwa na wakristo... wachache... Na wanasema ni sheria wambie wakupe kifungu uone kama watakipata... Si kwa katiba, sheria za nchi wala Quran inayowapa uhalali wa kuzuia watu kula. Ni mihemko tu
 
Inasikitisha sana...


Cc: Mahondaw
Inasikitisha sana kivipi? Kila nchi duniani ina sheria zake, hulazimishwi kwenda kwenye nchi hizo lakini ukiamua kwenda ni lazima ufate sheria za nchi. Ikiwa unatoka katika nchi inayoruhusu kuvuta bangi hadharani haimaanishi kuwa ukienda nchi zinazokataza uvutaji wa bangi wewe uvute. Zanzibar inakataza kula HADHARANI wakati wa mwezi wa ramadhani, watu wote wanajua na watembezaji watalii wanajua na walikumbushwa kitambo, sasa tatizo ni nini hapo?
 
View attachment 2949051
👆Na hawa Wazanzibari walioko Uarabuni wanaozuiwa kula Futari mpaka wenye Dini yao wafuturu Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inaongeleaje?
Serikali ya zanzibar imewahusu nini yanayotendeka katika nchi nyengine? Sisemi kinachofanyika hapo ni sawa ila nashangaa kwa nini unahusisha na serikali ya zanzibar. Hili halihusu serikali ya zanzibar kama ilivyokuwa haiwahusu nyinyi watanganyika kinachofanyika zanzibar.
 
Apelekwe mahakamani kwa kula...
Umetumia kitu gani kwani kwenye kula daku mnakunywa na pombe???
sheria ya zanzibar haikatazi mtu kula wakati wa ramadhani, inakata kula HADHARANI mchana. Halazimishwi mtu kwenda zanzibar wakati wowote ule ila ufate sheria zake kama hukubaliani nazo usiende!!!!
 
Imani na matendo ya imani kwa Mungu wa kweli haihitaji kutumia nguvu za kimwili. Kufunga kwa ajili ya mambo ya kiroho kunahitajika imani na uvumilivu. Ni kujizuia kula kwa muda uliopanga wewe binafsi au kupangwa na dini au madhehebu yako. Haijalishi utakiona chakula mbele yako au utamwona mtu akila mbele yako. Wala hutakiwi kumshutumu au kumlaumu anayekula, kwani yeye hiyo funga haimhusu, inakusuhu wewe. Unachotakiwa ni kuonyesha ukomavu wako wa imani, kwamba pamoja na kusikia harufu nzuri ya chakula au kukiona chakula mbele yako, kamwe hutashawishika kutamani kula. Unatakiwa ushinde hilo jaribu.

Mimi nikiamua kufunga hamu ya chakula huwa inapotea kabisa, hata nikimwona mtu anakula siwezi kukwazika au kutamani kula kwa namna yoyote hadi nimalize funga yangu.
Huenda Upo sahihi lkn hapa sheria na taratibu hazijawekwa kwa kuzingatia maoni binafsi.
Hayo ni maoni yako yanaheshiniwa ila huo ndio utaratibu wa Wazanzibar asiyeweza kuufuata kipindi hiki na aondoke Zanzibar
Ni sawa leo ufike Saudia then uanze kumkiss Demu wako hadharani kwakuwa huko kwenu una uhuru wa jambo hilo Bro ......
Maisha ni rahisi sana Vumilieni
 

Attachments

  • IMG-20240331-WA0055.jpg
    IMG-20240331-WA0055.jpg
    50.2 KB · Views: 1
Back
Top Bottom