Tetesi: Kampuni ya Yapi Merkezi kuchunguzwa kwa rushwa na kuingilia mambo ya ndani Tanzania

Mwacheni JPM apumzike jamani, mkichunguza, mnamuumbua
 
Shame kabisa, kwenye huo Mradi Jiwe alijaza Maaskari wengi, walishindwa Kujua hizo hujuma na kuzizuia wakiwa on ground?
 
Ukute wanataka aondoke Yapi Merkezi,wamtafute ambaye atawapa wao ten percent.
Na atakayepewa ni yule mchina wa rais wa mawe! Firina zote hizi anazileta yeye ili mchina aweke mzigo mezani wa kumsaidia kwenye kampeni za kugombania kijiti ma maadam! Mama hajamshtukia huyo mvaa bendera Hadi Sasa.
 
..mturuki amechelewesha sana huu mradi.

..haiwezekani dar to moro ichukue miaka 5 na bado mradi haujakabidhiwa.

..mchina alijenga reli ya tazara, dsm to kapirimposhi, na akakabidhi mradi ndani ya miaka 5.

cc Proved
Jee munampa fedha za kufanyia kazi kwa wakati?

Halafu unalinganisha mchina wa enzi ya Mao Zedong na leo hii wapi kwa wapi? Miaka 50+ nyuma!
 
Acha hizo, ingekuwa enzi za mwendazake ningekutaka uvae jezi ya Chadema kisha upite barabara ya stesheni, huko ungejua kuwa CCM na vyombo vya usalama ni mapacha.
Hahahaa au wakuone mko watu kama kumi tu mna jambo lenu. Ilifika mahali hata vikundi vya Saccos vikawa vinazuiwa wakidhani wanajadili mambo ya Chadema.
 
Shame kabisa, kwenye huo Mradi Jiwe alijaza Maaskari wengi, walishindwa Kujua hizo hujuma na kuzizuia wakiwa on ground ?
Tunaambiwa vyomba vya usalama( vipenyo) viko kila mahali sasa mbona kila kona tunapigwa vyenyewe huwa vina kazi gani?
 
Huyu Bimkubwa kuna mambo mazito kama SGR na Nyerere Dam hayatilii maanani yeye kakazana na COVID 19 tu na mikopo sijui anachukua ya kazi gani.

Hivi wachina si wapo? Si muwape hiyo miradi ya kimkakati? au kuna maelekezo ya Msoga?
 
..mturuki amechelewesha sana huu mradi.

..haiwezekani dar to moro ichukue miaka 5 na bado mradi haujakabidhiwa.

..mchina alijenga reli ya tazara, dsm to kapirimposhi, na akakabidhi mradi ndani ya miaka 5.

cc Proved
Akina Majaliwa Kassimu walikuwa wanashinda mitandaoni kutwambia tangu 2019 mradi umefika asilimia 75%πŸ˜€πŸ˜€
 
Jee munampa fedha za kufanyia kazi kwa wakati?

Halafu unalinganisha mchina wa enzi ya Mao Zedong na leo hii wapi kwa wapi? Miaka 50+ nyuma!

Kipande cha Dar to Moro serikali ilisema tunatumia fedha za ndani, na tulihakikishiwa kwamba fedha hizo zipo.

Binafsi nilitegemea miaka hii ujenzi utakamilika kwa haraka kuzidi wakati wa Tazara kwasababu ya maendeleo ya kiteknolojia na uwepo wa vifaa na mitambo ya ujenzi bora zaidi.

Nimelinganisha Dar to Moro vs Dar to Kapirimposhi. Sioni mantiki ya mkandarasi wa Sgr kuchelewa kukamilisha kipande kidogo hicho kwa wakati.
 

..kipande nilichohoji ucheleweshaji wake ni Dar to Morogoro.

..maelezo ya serikali yalikuwa kipande hicho kinajengwa kwa kutumia fedha za ndani, sio mkopo, donors / wafadhili.

..sijahoji kuhusu Moro Dom Makutupora. Lakini pia ninavyokumbuka fedha za kipande hicho ni mkopo toka kwa mabenki ya ulaya / mabeberu.

..mimi nilikuwa mmoja wa wanaJF waliotetea Yapi Merkez waliposhinda tender. Niliangalia rekodi yao ya ujenzi Dubai, Qatar, etc nikaamini wako vizuri. Sijui ni kwanini wamechelewesha mradi huu kwa kiwango hiki.

..hata Wachina wakichelewesha kazi tutahoji kulikoni. Tunatakiwa tu-demand kazi zenye kiwango zinazokamilika kwa wakati.
 
Ujenzi wa dar Moro ni fedha za ndani na mkopo kutoka AFDB. Na huu mkopo wa AFDB mbona ulikuwa wazi tu. ni Kama ilivyokuwa Daraja la tanzanite ambalo limejengwa kwa mkopo na pesa za ndani. Yote haya yalikuwa reported kwa umma.

Sasa ikiwa pesa za mkopo zinachelewa na hata za ndani haziendi kwa wakati unataka ujenzi ufikie wapi?
 
Wewee wa ajabu! Hii kampuni si ililetwa na JPM? Kwa hiyo ndiye aliyehongwa?
Wakati wa JPM, kazi ilipigwa kwelikweli na hii hii kampuni.

Kwa ufupi Hawa wakandarasi ni wakandarasi wa kimataifa, sio wakuokota , wanefanya ujenzi nchi mbalimbali.

Kwa Sasa wameamua kua hivo ili kuendana na Serikali ya Sasa ya Samia ilojaa upigaji na kutowajibika .

Lini Samia amewah fanya angalau ziara yenye lengo la kufatilia utendaji kazi ??.( Ukinielewa hapo, Utajijua wee ni Mpumbavu namba Moja).
 
Wewee wa ajabu! Hii kampuni si ililetwa na JPM? Kwa hiyo ndiye aliyehongwa?
Hakuna kampuni inaletwa na raisi, utaratibu unaotumika ni single source. Ndio maana unaona hata kipande cha Tabora kwenda kigoma kapewa mchina.

Leo Tanesco wamesaini mkataba na kampuni ya uarabuni Masdar kuzalisha umeme mg 2000. Unataka kusema mama Samia ndio kawaleta hao Masdar?

Acheni kukariri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…