Tetesi: Kampuni ya Yapi Merkezi kuchunguzwa kwa rushwa na kuingilia mambo ya ndani Tanzania

Hakuna upigaji acha kukariri
Alafu pia hao wanaweza pia kukosea Kama wanavyokosea wengine, sio malaika hao.
 
Hakuna upigaji acha kukariri
Alafu pia hao wanaweza pia kukosea Kama wanavyokosea wengine, sio malaika hao.
Narudia kukuambia, hawa waturuki ni wakandarasi wa kimataifa! Zingatia hili
Kama suala la upigaji hulioni ... Pole sana.
 
Natamani kuufahamu JPM aliwaroga kwa uchawi upi nyie watu!! Kwahiyo unajifanya umesahau kwamba huyo Mturuki aliletwa na utawala wa JPM? Yaani unajisahaulisha hicho kipande cha daraja kinachotajwa kilijengwa wakati wa huyo huyo JPM na hitilafu yake iligundulika wakati wa huyo huyo JPM!! Unataka kujisahaulisha hata kipande cha Dar Moro kimechukua miaka kadhaa wakati wa huyo huyo JPM! Wakati wewe na wenzako mnajisahaulisha, pitia huu uzi hapa chini kisha tujuze ikiwa wakati huo JPM alikuwa keshafariki

Nimeona daraja la waya (cable stayed bridge) la SGR Kamata likivunjwa, shida nini?

 
Narudia kukuambia, hawa waturuki ni wakandarasi wa kimataifa !!. Zingatia hili


Kama suala la upigaji hulioni ... Pole sana.
Sawa wa kimataifa. Kwahiyo wakifanya mambo ya ovyo yaachwe eti kisa waliletwa na JPM?! Hilo daraja hitilafu zilionekana tangu wakati JPM yupo hai kwahiyo unashangaza unapodai eti JPM ndio alikuwa dawa ya watu kama hawa wakati matatizo ya hao jamaa yalianza tangu wakati JPM yupo hai
 
Ndio anaundiwa zengwe achomolewe....
Anaundiwa zengwe na nani?! Kwani kwa mfano lile daraja ambalo tangu zamani lilishasemwa lipo chini ya kiwango lilijengwa na nani?! Hivi ulishajiuliza kingetokea nini kama lile daraja lingekuwa maporini huko na watu kufungasha virago mara baada ya "kukamilika" kwake?!
 
 
Hawa waliletwa na nani kwa utaratibu upi ?
 
Inaonekana walishakamuliwa na awamu ya 5 na sasa wanapigwa mkwara ili wakamuliwe na awamu ya 6. Waturuki wanachunwa kama mbuzi.
 
Sioni dalili sgr kuish miak ya HV ksribuni humuoni kina about na bm wanazidi kuingiza vyuma vipya kila siku Tena kwa root za dar moro
 
Huko uarabuni hakuna mito, milima na misitu.
 
Usalama wa Taifa kweli wanaangalia huu uozo ukiendelea na hakuna kinachotokea!
 

Hiyo ya kuhakikishiwa uwepo wa fedha hakuna anayeujua ukweli maana tumeona mengi baada ya huyo aliyetuhakikishia kuondoka.

Ile reli ya Mchina fedha ilikuwa inatoka kwake (sina hakika kama ilikuwa mkopo au la) na wafanyakazi asilimia kubwa ilikuwa wanatoka kwake sasa hapo hakukuwa na kitu cha kuchelewesha.
 
Mazezeta ya mwendazake ni janga la taifa
 
chanzo cha habari:thetanzaniapost.com

Vyombo vya ulinzi na usalama nchini Tanzania vimeanza uchunguzi dhidi ya Makamu Mwenyekiti wa Kampuni ya Ujenzi ya Yapı Merkezi Bwana Erdem Arioglu. Vyanzo mbalimbali vinaeleza kuwa Arioglu anatuhumiwa kuwa sababu kubwa ya kuchelewa kukamilika kwa mradi wa SGR huku akiwatendea visivyo makandarasi wa Kitanzania kwa kuwacheleweshea malipo yao. Raia huyo wa Uturuki pia anatuhumiwa kuingilia siasa za ndani za Tanzania kwa kutoa rushwa kwa Wabunge mbalimbali kukwamisha miradi mbalimbali ya maendeleo kupitia michango yao Bungeni. Bunge la Tanzania linatarajiwa kutoa taarifa baada ya uchunguzi huku baadhi ya Wabunge wakitaka raia huyo wa Uturuki kuondolewa nchini mara moja.

Mbali na tuhuma hizo kampuni hiyo pia inatajwa kuendelea kuipa Tanzania hasara ya mabilioni kutokana na ujenzi wa chini ya viwango katika baadhi ya maeneo. Eneo mojawapo ni kipande cha daraja la Nkurumah eneo la Kamata jijini Dar es Salaam ambapo kampuni hiyo iliamuriwa kuvunja na kuanza ujenzi upya baada ya kuonekana liko chini ya kiwango ikiwemo muonekana wa wazi wa nyufa kama inavyoonekana pichani!.

Katika baadhi ya maeneo ya mradi huo usanifu umekiuka angalizo kwenye njia za maji na kuzifunga jambo ambalo linahatarisha usalama wa matumizi ya mradi huo pale utakapokamilika.Athari za jambo hili zinaelezwa kuwa zitailetea nchi maafa makubwa zaidi kama ajali na hasara za ukarabati wa mabilioni pale ambapo mradi huo utakamilika.

Katika tuhumu hizo imeelezwa kwamba serikali imeunda timu ya uchunguzi huku timu nyingine ya siri ikihakiki shughuli na rushwa katika mradi huo kabla ya kutoa ripoti rasmi

Je, ujasusi wetu hupo bize na kulinda ccm mpaka haya yanatokea
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…