Kamwe usilipize kisasi kwa mtu awaye yote

nawasamehe sana watu.japo Wachache nawa u....😕😕😕😕😕
 
Ukikomaa kulipa kisasi basi kabla ya kulipiza kisasi, chimba makaburi mawili - moja lako mwenyewe na lingine la huyo uliyempania kwa kisasi.
Usitutishe.....yaani mtu anateka watu, anawakata vichwa na kuwamwagia Tindikali....na kuwapoteza lakini watu wamwache tu aendelee na kazi hiyo?
 
Yoyote atakae ingia kwenye 18 zangu napambana nae. Huruma hadi lini? Na kwanini aje akuanze? Labda kuna kitu anakitaka
Hii mind set ndio imeifanya Israel imekuwa Super Power na China pia.

Mtu anakuibia hela ukimlipisha wapumbavu wanasema ungesamehe tu.

Sijui ni laana au vipi.

Kuna ile mtu anakukosea unaona kabisa ni Bahati Mbaya na kuna yule anafanya hadi anajidai na kujitangaza wazi wazi.

Huku unaumia yeye anacheka.
 
Kweli bhana, unakuta mkosaji wa kwanza alifanya ubaya bila kuupanga kihiivyo.

Ila anayelipa kisasi anapangilia kabisa nitafanya hivi na nitamuumiza na yeye kwa staili hii. Huyu ndiye mbaya kuliko mbaya wa mwanzo
 
Kweli bhana, unakuta mkosaji wa kwanza alifanya ubaya bila kuupanga kihiivyo.
Huu wa bila kuupanga unajulikana na unakuwaga wazi.

Mfano mtu anakuja kukupora Shamba lako na wala halijawahi kuw lake. Aka team na mashahidi wa uongo mwisho anafanikiwa kubeba Nyumba yako.

Huo ni bahati mbaya?
 
Kuna kitu kinaitwa karma, always unayoyafanya dunia hii yata kurudia. So kama imetokea mtu ame expierience hayo atulie, amuombe Mungu ampe neema ya kusamehe. After katika time yake hapa duniani, vilichokuliwa vitatudishwa, either vije vile vile au bora zaidi
Na walikufanyizia ubaya yatawakuta ni suala la muda. So until then endelea na maisha, utakuwa suprised namna mambo yatakavyobadilika
 
Kama tungeishi kama utakavyo basi tusingekua na Mahakama,wala watu wasingekua wanawafungulia kesi watu waliowafanyia mabaya,

Imagine Dunia ingekuaje? Unamfanyia mtu jambo baya ukijua kua atakusamehe!

Jino kwa jino,ubaya ubaya,kisasi ni muhimu sana ili kuleta heshima kwenye jamii.
 
Moja ya sababu ya umaskini ktk Nchi zetu ni kuhendekeza misamaha kwa Wala Rushwa na Mafisadi.

Mtu anakula hela ya umeme wa Mikoa mitatu. Na anaachwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…