Swala la mtu kuoa akiwa hana chochote inategemea na wazazi wake kuwa walihitaji kuwaona wajukuu wao wasife hawajawaone huwajwahi sikia kitu kama hichi, pia huwa wanawaambia tunachokula tutakula wote. nina wasiwasi hujakulia nyumbani kijijini kabisa nadhani haya ungeyaelewa kwa mapana zaidi na usingepata tabu kuweka hoja, ebu uliza experience ya nyumbani kwenu kwa ma bibi na mababu unakotoka huko. ukiwa mdogo kama umekulia kijijini umesoma hadi darasa la 7 au hadi form 4 haya sio mageni ni ya kawaida sana. Wameru huwa wanawapa mashamba wanao wanaanzia hapo maisha, sasa hayo mengine kama mwanamke alikuwa wa aina gani na alishindwa kusaidiana na huyo mwanaume kutafuta basi hapo ni kitu kingine, mwanamke pia alikuwa dhaifu kwann wasisaidiane kwenda kutafuta. kumbuka misingi ya kuona ni muhimu sana.
Sema ww kama ww huwezi kumpa mwanaume mahari, usiwasemee wengine maana misingi ya kukutana na huyo mwanaume wako ni taofauti kidogo, nazungumzia misingi unielewe hapo, wapo wengi walio pewa mahari na wake zao wameoa na wana watoto wana heshima na maisha yako vizuri hata huwezi jua. familia ina furaha. weka uzi ambao utakao waita waliowahi tolewa mahari na wake zao utaona watajibu wangapi na uwaombe wakupe experience ya maisha, unaweza ukajikuta ww ulikosea sana.
Mimi binafsi nilipewa pesa na mwanamke nikaenda kutoa mahari kwao, maisha yangu yalivyo huwezi amini, mkewangu akinipa maji anapiga magoni na tunaishi maisha mazuri sana tu ana adabu na heshima ni kubwa sana.