Naunga mkono hoja, ilitakiwa kila Tarehe 12- 17 March iwe ni wiki ya JPM, kufanyike Tamasha kubwa Chato, mikutano, Marsha, semina, makongamano, hata maandamano yafanyike Chato kwa wiki nzima, Tuanzishe Tamasha la Utalii wa Makaburi, ndege zitafurika, Chato itajaa, Itachangamka na Magufuli mwenyewe huko aliko atafurahi!. Ile GS Hotel itakuwa Fully Booked mwezi mzima.
Tamasha hilo litafuatiwa na , Wiki ya Maadhimisho ya Miaka Mitatu ya awamu ya 6 Madarakani.
Hili Mnalionaje?.
P
HAPANA, Matamasha ni uharibifu wa pesa za umma. Nchi yetu inahitaji kila senti iliyoko mfukoni au draw zetu popote zilipo, yani tunamatatizo mengi sana na mengi kama siyo yote yanahitaji pesa. Hii michezo ya Mgeni rasmi, sijui kongamano, mikutano isiyo isha na isiyo na tija huikuti nchi zilizoendelea.
Hapa kwetu tumezidi, kuwasha mwenge ni shughuli ya mabilioni na itifaki za kijinga, kuuzima vile vile. Umeona juzi Arusha shughuli ya kuuwasha Mwenge, kauwasha MAJALIWA, hahaha we acha tu. Semina, makongano, na warsha ndio usiseme pesa zinaliwa kinachojadiliwa hakipo.
Nchi za wenzetu maeneo ya utalii yanajiendesha, pesa zinakusanywa zinahudumia eneo husika, zikizidi maboresho yanafanyika kuongeza haiba ya eneo husika. Nchi yetu pesa za utalii tunazisikia kwenye hotuba tu, hatufahamu zinakwenda wapi.
Tukiyaendeleza maeneo ya kumbukumbu na kuyaweka vizuri watalii watakuja kuyaangalia, na pesa zitaingia na tutafanya maboresho, sioni haja ya maandamano na warsha.
Na nchi za wenzetu hata huo utalii hautangazwi kiivyo, maeneo yanajulikana yako kwenye mitandao, na hayabadiriki.
Mfano nimewahi kuishi marekani, lakini sijawahi kuona popote LAS VEGAS inatangazwa, Lakini ukifika LAS VEGAS hutoamini, ndege zinavyopishana kuleta watalii wa nje na wa ndani, Mahoteli na kasino zimejaa, mitaani ndio usiseme, na Washington DC vile vile, na miji mingine.
Tofauti na kule hapa kwetu pesa nyingi huishia mifukoni na matumboni mwa wasimamizi. Utaona mara sare za vitenge kila siku, kila mkutano na sare yake na hiyo ni budget ya wizara.
Tuache haya mambo tuwe wazalendo wa kweli, pesa zitumike kwenye vitu halisi vyenye kuleta tija na thamani ya pesa ionekane, tuache ujanja ujanja, hatutaendelea kamwe.
Tuyatambulishe maeneo ya utalii, tuyaweke kwenye mazingira mazuri, kisha tuyahudumie ili yaendelee kutuingizia pesa, tulinde maliasili zetu, Huko Marekani Zoo kibao na ukiangalia wanyama 90% wametoka Tanzania, sasa jiulize mapato ya zoo Tanzania tunapa asilimia ngapi au kuna mfumo gani unatumika kulinda wanyama wetu walioko huko kwenye hizo zoo nje ya Tanzania.
Wanazaliana, je?tiunajua ni wangapi sasa na tunampango gani kuwarudisha au ndio tumetoa sadaka? Tuanachezea rasilimali ambazo walipaswa waje hapa kuziona tuanwapelekea huko nje, halafu mbuga zetu tuna kata vitalu tena tunawakabidhi wao ndio waendeshe sisis tunapewa asilimia kadhaa yani kodi, kwanini?
Uzalendo tunamuachia nani?
Kaka ni mengi ya kuzungumza lakini tuishie hapo, nimesema HAPANA kwa wazo lako.