Kanda ya Ziwa tusikilizwe kuhusu uwanja wa ndege. Haivumiliki tena

Kanda ya Ziwa tusikilizwe kuhusu uwanja wa ndege. Haivumiliki tena

kama hawana fedha ahadi za nini bora kusema ukweli hili la uwanja wa ndege wa Mwanza nchi nzima wana hasira nalo kwa vile linadharirisha hadhi ya nchi bora waufunge kwanza. Tujipange km nchi ni aibu kubwa hayo mabanda.
 
kama hawana fedha ahadi za nini bora kusema ukweli hili la uwanja wa ndege wa Mwanza nchi nzima wana hasira nalo kwa vile linadharirisha hadhi ya nchi bora waufunge kwanza. Tujipange km nchi ni aibu kubwa hayo mabanda.

..wawape Dp world wajenge uwanja wa ndege na kuuendesha.

..kulikuwa na sababu gani kujenga uwanja wa ndege Chato kabla ya Mwanza?
 
..nadhani Sgr ikitumika kwa abiria na kati ya Dar na Moro haitaendeshwa kibiashara, na itakuwa ikiendeshwa kwa ruzuku.

..kwa mtizamo Sgr isipofika Isaka, Mwanza, na Kigoma, kwa ajili ya mizigo, serikali itabeba mzigo wa hasara.
Kweli
 
..Hii hapa chini ni taarifa ya TRC. Walisema Dar mpaka Makutopora ilikuwa ikamilike NOVEMBA 2020.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli aweka jiwe la msingi awamu ya pili ya ujenzi wa reli ya kisasa(SGR) yenye urefu wa 426km kutoka Morogoro hadi Makutupora mkoani Dodoma, hatua hiyo itaifanya Tanzania kuwa na treni ya umeme itakayokwenda kwa kasi ya 160 kwa saa kwa treni ya abiria na 120 kwa saa kwa treni ya mizigo.

Akihutubia mjini Dodoma kabla ya kuweka jiwe la msingi, Rais Magufuli amesema kumalizika kwa ujenzi wa reli ya kisasa(SGR) itasaidia kutoa ajira 30,000 za moja kwa moja na ajira 60,000 zisizo za moja kwa moja. "Reli ya Kisasa na Banadari kavu itakayojengwa mjini Dodoma itasaidia kuleta maendeleo kwenye mikoa ya kati" alisema Rais Magufuli, pia aliongeza kuwa baada ya ujenzi wa reli ya kisasa kutoka Dar es Salaam hado Dodoma serikali itaendleza ujenzi huo hadi mkoani Mwanza kukamilisha km1.219.

Reli ya kisasa kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma yenye urefu wa km522 inajengwa na kampuni ya kituruki ya Yapi Markez. Ujenzi wa reli hii ya kisasa utasaidia usafirishaji wa abiria na mizigo kutoka na kwenda nchi za jirani za Uganda, Zambia, the Democratic Republic of the Congo, Burundi na Rwanda.

Naye Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa amesema kuwa reli hii itakuwa na uwezo wa kusafirisha Tani 10,000 za mizigo kwa mara moja. "Tunapoteza wateja kwenye bandari ya Dar es Salaam kutokana na kutokuwa na miundombinu ya kuaminika, lakini baada ya mradi huu tutaweza kuwarudisha wateja hao" alisema Waziri Mbarawa

Awamu ya pili ya ujenzi wa reli ya kisasa(SGR) kutoka Dar es Salaam hadi Makutupora mkoani Dodoma unatarajiwa kukamilika November 2020.
 
Kuna bos wangu mmoja (wa zamani nikiwa niko kwenye ajira) ameshakunja almost 1b na mpaka saa hii hana hata 100 na kaz haja deliver the only advantage ni kwamba mradi una sua sua..siku ukiamka ghafla sijui atafanya nimi?!..mimi naangalia maana hata uwezo wa kuchangia 100k akiwekwa jela mimi sina 😂.
Hii nchi kuna watu wanaila kiulainiiiio wakt wengine tunapata tabuuu
 

RELI SGR YAJENGWA USIKU NA MCHANA KUFIKIA LENGO MIEZI 30


Mtanzania Digital
ByMtanzania Digital
October 17, 2017

0
1539

Facebook


Twitter


Pinterest


WhatsApp


kenya-railways-standard-gauge-railway-sgr-nairobi-mombasa-testride-mombasa-nairobi-stndard-gauge-railway-crbc-sgr-head-office-kenyan-professional-photographers-sgr-photos-130-300x169.jpg

Na LEONARD MANGOHA

MCHWA pamoja kuwa ni wadudu waharibifu kwa mali za binadamu, lakini wanayo sifa moja kubwa ya kufanya kazi usiku na mchana kwa ufanisi mkubwa.
Utendaji kazi unaoshuhudiwa katika ujenzi wa Reli ya Kati katika kiwango cha SGR Dar hadi Morogoro, inafanana kiutendaji kazi kama vile shughuli ya mchwa ya ujenzi wa usiku na mchana na Kampuni ya Kituruki ya Yapi Merkez, wakitimiza azma ya Rais John Magufuli ya Hapa Kazi Tu.

Ni wakati wa utekelezaji na si maneno marefu na kweli kazi inafanyika na usiku totoro kwa mafanikio na ufanisi mkubwa.

Baada ya kuwapo kwa taarifa za ujenzi wa reli ya kiwango cha kimataifa (standard gauge), hatimaye Februari 3 mwaka huu Kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli (Rahco), ilitiliana saini mkataba wa kuanza ujenzi wa mradi huo na kampuni ya Yapi Merkez ya Uturuki.

Baada ya hapo taratibu za ujenzi zikaanza ukiwamo ujenzi wa kambi zitakazotumika wakati wa ujenzi ikiwamo ile ya Ilala, Dar es Salaam, Soga, Pwani na Ngerengere Morogoro.

Wakati huo pia shughuli ya usanifu wa njia itakayopita reli uliendelea kama mkataba wa ujenzi huo ulivyotaka usanifu na ujenzi vifanyike pamoja, kazi ambayo inaelezwa kukamilika kwa asilimia mia moja.

Meneja Msaidizi wa Mradi huo, Mhandisi Chedi Masambaji, anasema kazi hiyo iliambatana na ile ya upimaji wa udongo wa eneo la njia ya reli ambayo pia imekamilika.
“Kama tulivyoweza kuona kuanzia Pugu hadi hapa Soga zaidi ya kilomita 100 ujenzi unaendelea vizuri na hivi karibuni mkandarasi ataanza kazi ya kupasua miamba,” anasema Mhandisi Masambaji.

Hadi sasa ujenzi huo unaendelea kwa shughuli mbalimbali kutekelezwa, ambapo tayari eneo lenye urefu wa kilomita 107 linaendelea na ujenzi likiwa kimegawanywa katika maeneo 10 ambapo yote hufanya kazi mchana na matano kati yake hufanya kazi usiku na mchana.

Mwishoni mwa wiki tulipata nafasi ya kutembelea mradi huo wakati wa usiku kuona maendeleo ya utekelezaji wake chini ya kampuni hiyo ya Kituruki.

Ni mwendo wa saa nne kutoka katikati ya Jiji la Dar es Salaam hadi kambi ya Soga kupitia Pugu, ukivuka milima mirefu na mabonde na wakati mwingine kulazimika kupita kwenye mahandaki shughuli mbalimbali zinaendelea kutekelezwa huku baadhi ya wafanyakazi wakilazimika kutumia kambi ndogo zinazohamishika kila baada ya kusogea umbali fulani.

Mradi huu unatekelezwa katika maeneo yaliyopitiwa na reli ya kati iliyojengwa na wakoloni mwaka 1905 na katika mazingira yasiyo na makazi ya watu, huduma za afya, maji wala nishati ya umeme.

Huenda maeneo hayo yana unafuu yakilinganishwa na wakati wa ukoloni kutokana na mabadiliko ya tabianchi, lakini bado mapori yenye vichaka vidogo na miti mirefu michache.

Uwapo wa reli ya kati unaweza kuwa msaada katika ukelekezaji wa mradi huu hata pale mvua zitakapoanza kunyesha kwa mizigo hiyo itasafirishwa kwa treni.
Kwa sababu reli hiyo inajengwa karibu na reli ya kati, hii itarahisisha ubebaji mizigo na ndiyo itakayotumika kupeleka kokoto na mataruma.

Mkurugenzi Mtendaji wa Rahco, Masanja Kadogosa, anasema wameamua mradi huo ujengwe usiku na mchana ili kuhakikisha unakamilika katika muda uliopangwa wa miezi 30 iliyoanzia Mei mwaka huu.

Kadogosa anasema hadi sasa jumla ya kilomita 107 zinaendelea na ujenzi kwa hatua mbalimbali ikiwa ni pamoja na ujenzi wa tuta la reli ambalo limekwishajengwa kwa zaidi ya kilomita 30.
Kadogosa anaeleza kuwa mwezi mmoja uliopita walipotembelea mradi huo Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa, alimtaka mkandarasi kuongeza kasi ya ujenzi kwa kujenga usiku na mchana.
“Kama tunavyoona hilo limeanza kutekelezwa, leo tumefika hapa usiku huu tumewakuta mafundi wakiendelea, sasa ili tuweze kwenda haraka zaidi tumeamua kuongeza ‘site’ (maeneo ya ujenzi) kutoka sita hadi kufikia 10.
“Unaposimamia mradi mkubwa kama huu unakuwa na ratibajedwali ya utendaji kazi inayokuongoza kwa siku kadhaa unatakiwa kuwa wapi, tunashukuru kwa sababu kazi inakwenda kama ilivyopangwa, maeneo hayo yote kumi hujengwa mchana na usiku matano kati ya hayo kazi hufanyika mchana na usiku,” anasema Kadogosa.

Kwa sasa kazi zinazoendelea ni zile zinazohusu ujenzi pekee kwa sababu mkandarasi anaendelea na ujenzi wa tuta na baada ya muda ujenzi wa tuta utakwenda sambamba na kazi nyingine ikiwamo ujenzi wa madaraja na karavati.
“Kazi ya ujenzi wa tuta ndiyo ngumu kwa sababu huchukua asilimia 60 ya ujenzi, yenyewe itakamilika kwa miezi 18 ya kwanza, uwekaji mataruma, kokoto, ufungaji wa reli na ujenzi wa mifumo ya umeme na mawasiliano ni asilimia 40 tu ya ujenzi wote na huenda haraka haraka.

Kadogosa anawataka makandarasi wazawa walioajiriwa kwa shughuli mbalimbali katika mradi huo kuhakikisha wanafanya kazi zao kwa uhakika na haraka na ikiwa hawawezi kufanya hivyo waondoke wenyewe.

Hadi sasa mradi wa ujenzi wa reli hiyo katika kipande cha Dar es Salaam hadi Morogoro chenye urefu wa kilomita 205 za njia kuu na 95 za njia za kupishania treni, utakaogharimu Sh trilioni 2.6 umeajiri zaidi ya watu 800 wakiwamo makandarasi, wafanyakazi, vibarua na watoa huduma mbalimbali.

Kwa mujibu wa Kadogosa ujenzi wa reli hiyo kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza, unatarajiwa kuajiri watu zaidi ya 600,000 hadi utakapokamilika, idadi hiyo inajumuisha wafanyakazi, vibarua na watoa huduma wengine wakiwamo mama lishe na wachuuzi wa vitu mbalimbali.

Anafafanua kuwa ajira hizo zitaendelea kuongezeka kulingana na kazi inavyofanyika, ambapo kwa wakati huu idadi ni ndogo kutokana na kazi inayotekelezwa ni ya ujenzi tu hivyo kazi nyingine zitakapoanza itaongezeka.
“Haiwezekani kuajiri watu wote wanaohitajika kwa wakati mmoja kwa sababu hawatakuwa na kazi ya kufanya, kadiri tunavyoendelea watu wengi zaidi wataajiriwa kadiri ya mahitaji halisi na yaliyoainishwa” anasema Kadogosa.

Meneja mradi wa Rahco, Mhandisi Maizo Magedzi, anasema kwa sasa kuna jumla ya mitambo 189 inayofanya kazi na itaendelea kuongezwa kadiri kazi itakavyoendelea.
Wakati wa mvua kazi haitaweza kuendelea vizuri kuna wakati tutalazimika kusimama kwa sababu mitambo itakuwa inakwama, lakini tutajitahidi kutumia mitambo ambayo matairi yake hayashiki tope, tayari mingine iko bandarini,” anasema Mhandisi Mgedzi.

Meneja Mradi wa Kampuni ya Yapi inayojenga reli hiyo, Abdullah Kilic, anasema hadi sasa wanaendelea vizuri na ujenzi wa reli hiyo inayotakiwa kukamilika katika kipindi cha miezi 30 ili kuhakikisha wanakamilisha katika muda waliokubaliana.
Uwezo wa kampuni hii katika utekelezaji wa miradi mikubwa ya aina hii si wa kutiliwa shaka kutokana na sababu mbalimbali ikiwamo uwezo wa Taifa la Uturuki katika masuala ya ujenzi ambayo katika dunia ni ya nne baada ya Marekani, China na Urusi.

Kwa kiasi kikubwa uchumi wa Uturuki unategemea sekta ya ujenzi ambayo ndiyo inayochangia zaidi katika pato la taifa kila mwaka ikifuatiwa na utalii.
Noman Sigara King ni Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Miundombinu, anasema hana wasiwasi na uwezo wa kampuni ya Yapi katika utekelezaji wa miradi mikubwa ya reli, kwa kuwa ameshuhudia mradi reli ya kiwango cha kimataifa inayounganisha Bara la Ulaya na Asia iliyojengwa kwa ustadi mkubwa nchini Uturuki.
Silaha nyingine kubwa ambayo kampuni hii inaweza kujivunia katika utekelezaji wa mradi huu ni wingi na ubora wa mitambo wanayotumia katika ujenzi. Kiushindani kampuni hiyo imebeba dhamana ya kuwa mbadala wa kampuni za Kichina ambazo zimehodhi soko la Tanzania na Afrika Mashariki.

Umuhimu wa SGR
Treni itakayotumia reli hiyo itakuwa na uwezo wa kusafirisha mizigo tani milioni 17 kwa mwaka, uzito ambao ni zaidi ya mara tatu ya uzito wa treni inayotumika sasa ambayo husafirisha tani milioni 5 tu kwa mwaka.
Itakuwa na uwezo wa kubeba tani 30 kwa behewa moja. Haya yatakuwa ni mapinduzi makubwa katika sekta ya usafirishaji nchini na hivyo kudai uzalishaji mkubwa zaidi.

Ikumbukwe kuwa treni hiyo itakuwa na uwezo wa kubeba tani 10,000 za mizigo kwa mara moja, uzito amabao ni sawa ule wa mizigo inayoweza kubebwa na malori ya ‘semi trailer’ 500.
Maana yake hapa ni kwamba, barabara zetu zitadumu kwa muda mrefu zaidi tofauti na hivi sasa, ambapo zimekuwa zikilazimika kufanyiwa marekebisho ya mara kwa mara tena muda mfupi tu baada ya kuanza kutumika kutokana kwa kutegemewa katika kusafirisha mizigo mizito zaidi ya uwezo wake.

cc bagamoyo, Mayor Quimby
 
Pamoja na hayo yote mamiradi makubwa bara na zanzibar ka-kiwanja kadogo tu hadhi ya min international Mwanza imeshindikana. kuna jambo limejificha. hatimaye litajulikana tu. wacha tusubiri dana dana za wanasiasa.
 
Tumieni ule wa chato wajinga ninyi wakati jiwe anajenga international Airport porini kama Mobutu kule Gbadolite mlikuwa mnashangilia badala ya kushauri basi tumieni huo huo au uzeeni ng'ombe mkajenge mwingine wenyewe
 
Leo nimemsikiliza Musukuma akizungumzia kuchelewesha kuhusu jengo la uwanja wa ndege wa Mwanza na miundo mbinu yake kuufanya uwe wa kimataifa.

Hali hii kwa sasa inatoa picha kama alivyosema Msukuma dharau kwa kanda ya ziwa haijalishi Makonda ni Mwenezi au Dotto ni Naibu Waziri Mkuu,kisiasa haitatosha kuwashawishi wananchi ambao ni wazi wanaonekana kutengwa kupitia uwanja huu, Songwe umejengwa, Arusha, Tanga,Dodoma,Tabora, Kigoma lakini kwenye mpango wa sasa uwanja huu haumo.

Ni nani anayeupiga vita. Rais kwa hili tunaomba uingilie kati kwa jinsi utakavyoona inafaa. Aidha barabara njia nne za kuingia jijini zimetupiliwa mbali hakuna anayezungumzia kwenye Mpango. Nadhani miji kama Mwanza Mbeya ni wakati wa kujenga njia nne kama ilivyo kwa Dar.

Kura ziko nyingi sana kwenye maeneo haya siyo ya kufanyia mzaha. Makonda pata maelezo ya miradi hii uondoe lawama.
Kwa hiyo umehama kutetea machalii umehamia Kanda ya Ziwa ambao Huwa unawaponda Kila siku? 🤣🤣
 
Vipi Mkurugenzi Mkuu wa TAA unakuwa mwongo kweupe Mktaba wa Ujenzi wa Jengo la Abiria uwanja wa ndege Mwanza kusainiwa Mwezi February 2024 ,mbona hamna kitu na ulikiri kuwa mtatekeleza maelekezo ya Rais mara moja. This is insurbodination sir to the higher authorities. Angalia vinginevyo toa taarifa kwao kwa nini umeshindwa kufanya hivyo.
 
Acheni kuifundisha serikali majukumu yake,wananchi hamtakiwi kuwa watu wa maneno maneno bali vitendo hakuna mabadiriko yanapatikana kwa maneno maneno.. kama mkiamua jambo fulani hamlitaki na mkaandamana kwa umoja na uwingi pasipo kukata tamaa jambo lenu litapita tu

Viongozi wabishi na wasiojitambua mtawatoa kwenye sanduku la kura na hata kama mtahitaji mabadiliko kikatiba,utawala,Sheria ama mtu fulani awajibishwe hamtashindwa nguvu yenu ikiwa Moja kwa uwingi wenu hakuna litashindikana.

Swala la kura litaonekana kama halina nafasi ktk mageuzi mnayoyataka hiyo nikwasababu wananchi husika mmetaka iwe hivyo,lkn mkitaka kura yenu iwe na nguvu hamshindwi ni maarifa kidogo tu yanahutajika ktk Kila kichwa cha mtanzania basi nchi inabadilika nakuwa nchi ya ahadi yenye asali na maziwa.
Kati ya viwanja vya ndege vya mikoani, flow kwenye uwanja wa Mwanza ni ya juu sana. ndege zote za ATCL zinazohudumia njia hiyo hazijawahi kutojaza pamoja na kuwa zinapiga ruti tatu hadi nne kwa siku. Jengo lile lilikuwa linajengwa vizuri sana kwa haraka wakati wa Magufuli lakini nadhani alikufa nalo. Ujenzi wa viwanja vya Mwanza na Songwe ulianza pamoja lakini Songwe imekwisha
 
Tukisema jiwe alikosea kupeleka airport kijijini mnakaza fuvuz. Haya sasa, huo mradi ungepelekwa Mwanza si ingekuwa poa sana?
 
Siungi mkono hoja hii kwasababu uwanja wa ndege sio hitaji la walio wengi Mwanza. Usafiri wa ndege ni hitaji la few matajiri wachache wapanda ndege. Kanda ya Ziwa bado ni Kanda primitive, hivyo wananchi waliowengi bado wanatumia primitive means of transport, usafiri wetu mkuu kutembea kwa miguu vichochoroni, na barabarani, baada ya miguu ni baiskeli, boda boda, bajaji na magari. Kwa sasa Busisi barabara inakwenda kukamilika. Kwa wale wahitaji kuruka, zile ndege zetu za asili za kupaa zipo!.

Msitishie kuhusu kura 2025 ni kura bwelele!. Tayari tumepewa Doto Biteko huyo ndiye Waziri Mkuu ajaye, Makonda huyo anakuja kuingia Bungeni kuwa Waziri. Luhaga Mpina huyo kwa sasa anapiga sana kelele, soon atatupiwa fupa lenye bonge la nyama, atanyamaza!. 2025 kura zote Kanda ya Ziwa ni kule kule kwa siku zote!.
Mnataka tupewe nini tena wakati nchi yote ni yetu!.

P
Mi napingana nawe sio tu kwa sababu nami ni wa huko, ila nadhani kukarabati au kupanua viwanja vya ndege ni sehemu moja tu ya mahitaji yetu kanda ya ziwa. Tuna hitaji kupanua barabara zetu na kuziwekea miundo mbinu kama mitaro na pia tujenge mifereji ya maji machafu kama huko kwa wenzetu.

Tusipofanya leo huko mbele itakuwa shida sana. Tukifanya sasa tutaokoa pesa nyingi sana, Kwasababu kupanua viwanja kuna ambatana na kulipa fidia za makazi ya watu, kubomoa nyumba za watu na kujenga uwanja mkubwa na wa kisasa. Leo hii gharama sio kubwa,kulipa fidia,na hata kujenga, hivyo tufanye leo badala kusubiria miaka 50 ijayo.

Pia nisingependa suala la ujenzi au uboreshaji miundo mbinu yoyote ikahusishwa na SIASA zetu hizi. Haya mambo tungeyatenganisha tungekuwa mbali sana. Tizama mafuriko yanavyo tuathiri kila mwaka nyakati za mvua, tunapata hasara kubwa sana kukarabati na ukarabati usio isha kwa sababu hatuna mipango endelevu.

Naamini umeenda Dodoma karibuni, Tizama Magufuli City, Ina pendeza lakini miundo mbinu bado inaendelea kujengwa, ili kuujenga mji. Wenzetu huko Marekani,Ulaya,Asia au niseme nchi zilizoendelea, Wanaanza kuweka miundombinu, kama mifereji ya maji machafu, Cable za umeme au mawasiliano ardhini na kujenga barabara kabla hata hawajaanza kujenga majengo. Huku kwetu tunafanya kinyume tunaanza kujenga majengo kisha ndio tunaanza kutafuta namna za kuweka mitaro, au kupitisha cable za mawasiliano.

Wangeweka city planners au Urban development planners waweke pla za miaka 200 ijayo, waangalie population growth rate na wajenge miji yenye kukudhi vigezo vyenye mahitaji yetu kwa muda mrefu kuliko hii kila bajeti tunaweka pesa za kukarabati barabara na ukarabati wenyewe ndio ule unauona kila mara, unakuta kampuni zetu hizi wanapika lami kwenye mapipa kwa kuni za kuokoteza.

Kama hitaji la viwanja litakuwepo miaka 50 ijayo kwanini wasijenge leo kikubwa kukidhi mahitaji ya miaka 50 ijayo? Tuwe na plans za muda mrefu sio, hizi za kupangwa wakati wa uchaguzi zisizotekelezeka.

Hao wana siasa nimewaacha sitaki hata kuwaongelea sioni sababu kwa sasa.
 
Acheni kuifundisha serikali majukumu yake,wananchi hamtakiwi kuwa watu wa maneno maneno bali vitendo hakuna mabadiriko yanapatikana kwa maneno maneno.. kama mkiamua jambo fulani hamlitaki na mkaandamana kwa umoja na uwingi pasipo kukata tamaa jambo lenu litapita tu

Viongozi wabishi na wasiojitambua mtawatoa kwenye sanduku la kura na hata kama mtahitaji mabadiliko kikatiba,utawala,Sheria ama mtu fulani awajibishwe hamtashindwa nguvu yenu ikiwa Moja kwa uwingi wenu hakuna litashindikana.

Swala la kura litaonekana kama halina nafasi ktk mageuzi mnayoyataka hiyo nikwasababu wananchi husika mmetaka iwe hivyo,lkn mkitaka kura yenu iwe na nguvu hamshindwi ni maarifa kidogo tu yanahutajika ktk Kila kichwa cha mtanzania basi nchi inabadilika nakuwa nchi ya ahadi yenye asali na maziwa.
🆒👍👌👏🤝🙏🔊
 
Mi napingana nawe sio tu kwa sababu nami ni wa huko, ila nadhani kukarabati au kupanua viwanja vya ndege ni sehemu moja tu ya mahitaji yetu kanda ya ziwa. Tuna hitaji kupanua barabara zetu na kuziwekea miundo mbinu kama mitaro na pia tujenge mifereji ya maji machafu kama huko kwa wenzetu.

Tusipofanya leo huko mbele itakuwa shida sana. Tukifanya sasa tutaokoa pesa nyingi sana, Kwasababu kupanua viwanja kuna ambatana na kulipa fidia za makazi ya watu, kubomoa nyumba za watu na kujenga uwanja mkubwa na wa kisasa. Leo hii gharama sio kubwa,kulipa fidia,na hata kujenga, hivyo tufanye leo badala kusubiria miaka 50 ijayo.

Pia nisingependa suala la ujenzi au uboreshaji miundo mbinu yoyote ikahusishwa na SIASA zetu hizi. Haya mambo tungeyatenganisha tungekuwa mbali sana. Tizama mafuriko yanavyo tuathiri kila mwaka nyakati za mvua, tunapata hasara kubwa sana kukarabati na ukarabati usio isha kwa sababu hatuna mipango endelevu.

Naamini umeenda Dodoma karibuni, Tizama Magufuli City, Ina pendeza lakini miundo mbinu bado inaendelea kujengwa, ili kuujenga mji. Wenzetu huko Marekani,Ulaya,Asia au niseme nchi zilizoendelea, Wanaanza kuweka miundombinu, kama mifereji ya maji machafu, Cable za umeme au mawasiliano ardhini na kujenga barabara kabla hata hawajaanza kujenga majengo. Huku kwetu tunafanya kinyume tunaanza kujenga majengo kisha ndio tunaanza kutafuta namna za kuweka mitaro, au kupitisha cable za mawasiliano.

Wangeweka city planners au Urban development planners waweke pla za miaka 200 ijayo, waangalie population growth rate na wajenge miji yenye kukudhi vigezo vyenye mahitaji yetu kwa muda mrefu kuliko hii kila bajeti tunaweka pesa za kukarabati barabara na ukarabati wenyewe ndio ule unauona kila mara, unakuta kampuni zetu hizi wanapika lami kwenye mapipa kwa kuni za kuokoteza.

Kama hitaji la viwanja litakuwepo miaka 50 ijayo kwanini wasijenge leo kikubwa kukidhi mahitaji ya miaka 50 ijayo? Tuwe na plans za muda mrefu sio, hizi za kupangwa wakati wa uchaguzi zisizotekelezeka.

Hao wana siasa nimewaacha sitaki hata kuwaongelea sioni sababu kwa sasa.
Kwa dunia ya leo uwanja wa ndege siyo anasa tena ni usafiri wa haraka unaohitajika, hili halibishaniwi,kupanua mabarabara ni muhimu lakini uwanja wa ndege nao ni muhimu. Wananchi wanafuatilia kwa karibu mno ujenzi wa uwanja wa ndege wa Mwanza kwa vile inaonekana hata waliopewa TAA wanazembea ingawa walilalamika kutoshirikishwa sasa yako wapi? kumbe ilikuwa maneno tu.
 
. Jengo lile lilikuwa linajengwa vizuri sana kwa haraka wakati wa Magufuli lakini nadhani alikufa nalo. Ujenzi wa viwanja vya Mwanza na Songwe ulianza pamoja lakini Songwe imekwisha
Kama kichwa chako kingekuwa kinafanya kazi sawa saws usingeandika huo utumbo.

Magufuli angekuwa na akili asingetumia zile TSH 70 Billion kujenga uwanja wenye runway ya kimataifa kijijini kwake Chato.

Hivi kiwanja hicho kinatumikaje kwa sasa? Isijeikawa imekuwa Gbadolite nyingine
 
Back
Top Bottom