Kanda ya Ziwa tusikilizwe kuhusu uwanja wa ndege. Haivumiliki tena

lakini afadhali hao kuliko banda la kuku la Mwanza airport
 
Mama akitupatia daraja la kigongo na uwanja wa kimataifa, mwanza kazi atakuwa amemaliza aje kula samaki tu, wasukuma wanasema "mayu wa mbasa"
 
Kwa kutumia akili ya kawaida tu, ili kuilaumu serikali kwa haki, tujiulize;
Ni ndege ngapi za safari za kimataifa zinatua na kuruka kwenye viwanja vya Mwanza na Songwe?
Idadi ya ndege kwa ujumla kwa siku?
Baba wa taifa, pamoja na kuwa Rais kwa miaka zaidi ya ishirini, hakujenga barabara ya lami Butiama kwa sababu ya idadi ya magari ya kuwa ndogo.
Tunahitaji kuwa na fikra za kitaifa zaidi (statesmen) badala ya ubinafsi wa kikinga.
Hawa watu wenye fikra kama hizo wahitaji elimu ya ubinadamu kwanza.
 
Na haya ndiyo mawazo tunayotaka, kwamba ule uwanja ingawa ulijengwa na Marehemu Magufuli, siyo mali ya marehemu. Uwanja ni mali ya umma na uendelezwe, ufunguliwe utumike kama ulivyokusudiwa.
Tatizo ni kuhusisha maendeleo na siasa, hapo ndio tunakwama, anapokuja kiongozi mwingine anaanza kusema au kudhani mtangulizi wake alikuwa na mawazo au nia tofauti ya vitu alivyoviweka. Vision ya Taifa inakosekana, Uwanja wa ndege unajulikana na matumizi yake yanajulikana , sasa tunakwama wapi?
 
Naunga mkono hoja, ilitakiwa kila Tarehe 12- 17 March iwe ni wiki ya JPM, kufanyike Tamasha kubwa Chato, mikutano, Marsha, semina, makongamano, hata maandamano yafanyike Chato kwa wiki nzima, Tuanzishe Tamasha la Utalii wa Makaburi, ndege zitafurika, Chato itajaa, Itachangamka na Magufuli mwenyewe huko aliko atafurahi!. Ile GS Hotel itakuwa Fully Booked mwezi mzima.

Tamasha hilo litafuatiwa na , Wiki ya Maadhimisho ya Miaka Mitatu ya awamu ya 6 Madarakani.

Hili Mnalionaje?.

P
 
Kwani chattle international airport umekuwaje?
 
Naunga mkono hoja ijumaa nitakuwa tayari chattle.
 
kipi kinaanza kujenga uwanja kwanza au ndege za kimataifa kutua tuzione ndipo tujenge uwanja,uwanja ndiyo unaoleta ndege. uwanja wa Mwanza ni strategic mno kwa maziwa makuu na Afrika ya Kati na magharibi mama hili usiliache jenga jengo la kisasa pale,ingawa vita ni kubwa kuanzia TAA na Wizara yenyewe.
 
Chato Airport ibakie hivyo hivyo ili kizazi kijacho kitambue kuwa Tanzania iliwahi kutawaliwa na kiongozi mwongo na mbinafsi. Sisi Chato ndiyo kama Gbadolite ya Mobutu see seko.
 
Chato Airport ibakie hivyo hivyo ili kizazi kijacho kitambue kuwa Tanzania iliwahi kutawaliwa na kiongozi mwongo na mbinafsi. Sisi Chato ndiyo kama Gbadolite ya Mobutu see seko.
Tukiiacha inakuwa siyo sawa, Chato ni Tanzania, Na tunahitaji kuuendeleza ili vizazi vijavyo visituone wapuuzi/Wajinga, kwamba uwanja upo badala ya kuuendeleza na tuutumie tukauacha kwa sababu za kisiasa, ambazo hazina tija yoyote.

Pesa za wananchi zilitumika hivyo tunahitaji tija kwenye matumizi hayo.

Tutenganishe siasa zetu na maendeleo ya nchi yetu. Viongozi wafanye maswala ya policies na usimamizi bora wa rasilimali zetu, uongo wao wabaki nao wenyewe.
 
HAPANA, Matamasha ni uharibifu wa pesa za umma. Nchi yetu inahitaji kila senti iliyoko mfukoni au draw zetu popote zilipo, yani tunamatatizo mengi sana na mengi kama siyo yote yanahitaji pesa. Hii michezo ya Mgeni rasmi, sijui kongamano, mikutano isiyo isha na isiyo na tija huikuti nchi zilizoendelea.

Hapa kwetu tumezidi, kuwasha mwenge ni shughuli ya mabilioni na itifaki za kijinga, kuuzima vile vile. Umeona juzi Arusha shughuli ya kuuwasha Mwenge, kauwasha MAJALIWA, hahaha we acha tu. Semina, makongano, na warsha ndio usiseme pesa zinaliwa kinachojadiliwa hakipo.

Nchi za wenzetu maeneo ya utalii yanajiendesha, pesa zinakusanywa zinahudumia eneo husika, zikizidi maboresho yanafanyika kuongeza haiba ya eneo husika. Nchi yetu pesa za utalii tunazisikia kwenye hotuba tu, hatufahamu zinakwenda wapi.

Tukiyaendeleza maeneo ya kumbukumbu na kuyaweka vizuri watalii watakuja kuyaangalia, na pesa zitaingia na tutafanya maboresho, sioni haja ya maandamano na warsha.

Na nchi za wenzetu hata huo utalii hautangazwi kiivyo, maeneo yanajulikana yako kwenye mitandao, na hayabadiriki.

Mfano nimewahi kuishi marekani, lakini sijawahi kuona popote LAS VEGAS inatangazwa, Lakini ukifika LAS VEGAS hutoamini, ndege zinavyopishana kuleta watalii wa nje na wa ndani, Mahoteli na kasino zimejaa, mitaani ndio usiseme, na Washington DC vile vile, na miji mingine.

Tofauti na kule hapa kwetu pesa nyingi huishia mifukoni na matumboni mwa wasimamizi. Utaona mara sare za vitenge kila siku, kila mkutano na sare yake na hiyo ni budget ya wizara.

Tuache haya mambo tuwe wazalendo wa kweli, pesa zitumike kwenye vitu halisi vyenye kuleta tija na thamani ya pesa ionekane, tuache ujanja ujanja, hatutaendelea kamwe.

Tuyatambulishe maeneo ya utalii, tuyaweke kwenye mazingira mazuri, kisha tuyahudumie ili yaendelee kutuingizia pesa, tulinde maliasili zetu, Huko Marekani Zoo kibao na ukiangalia wanyama 90% wametoka Tanzania, sasa jiulize mapato ya zoo Tanzania tunapa asilimia ngapi au kuna mfumo gani unatumika kulinda wanyama wetu walioko huko kwenye hizo zoo nje ya Tanzania.

Wanazaliana, je?tiunajua ni wangapi sasa na tunampango gani kuwarudisha au ndio tumetoa sadaka? Tuanachezea rasilimali ambazo walipaswa waje hapa kuziona tuanwapelekea huko nje, halafu mbuga zetu tuna kata vitalu tena tunawakabidhi wao ndio waendeshe sisis tunapewa asilimia kadhaa yani kodi, kwanini?

Uzalendo tunamuachia nani?

Kaka ni mengi ya kuzungumza lakini tuishie hapo, nimesema HAPANA kwa wazo lako.
 
kwani chato ni Mwanza hiyo ni Geita fahamu mipango ya serikali ilivyo.Dont shout.Msijifiche kwenye kichaka cha uwepo wa uwanja wa Chatto.Kiwanja cha Mwanza kinatumika na wote ukiwemo wewe mwenyewe mpinga maendeleo.
 
Uwanja wa kimataifa si ulishajengwa chato..
Pale kitobuni mwa utalii kanda ya ziwa?!
Muulize Ndumbaro
 
Kamati za Bunge zilizotembelea Mwanza na Kanda ya Ziwa kwa nini hazipitii au kuzungumzia mradi wa ujenzi wa jengo la abiria La Airport Mwanza wakati kuna pesa za walipa kodi zimeingia hapo? kupitia halmashauri na serikali kuu kulikoni?
 
Mkataba umesainiwa leo ujenzi wa jengo uanze hofu yangu ni capacity ndogo ya kubeba watu. ingeongezwa kutoka 200 hadi 300.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…