Kanisa katoliki laja na mkakati wa kuleta orodha ya majina ya Watanganyika waliouawa October 29,2025

Kanisa katoliki laja na mkakati wa kuleta orodha ya majina ya Watanganyika waliouawa October 29,2025

Waliovunja kanisani kwa Gwajima wakiwa wameweka utepe wao watauwawa lini kama hiyo ndiyo adhabu?
Kwani hujui vibaka wote huchomwa moto ila wanaoiba kwa akili hawachomwi? Aliyenacho ataongezewa zaidi au maneno haya huyajui?
 
No wasifanye hiyo kazi na najua hawawezi kufanya. They are smart enough kuwahusisha na hilo. Hiyo ni sensa ya vifo na inahitajika kibali maalum Ili kufanya. Huo ni mtego.
TEC inajulikana kwa kuombea marehemu waliotangulia wapumzike kwa amani.
Hii sio sensa, hii ni taarifa ya waliokufa ili waombewe.

Kwa taarifa yako kabla ya ujio wa vitambulisho vya taifa, Katoliki inajua majina ya waumini wake na ilikuwa inasajiri walizaliwa lini na wapi, wazazi kina nani, wazazi wao wa ubatizo ni kina nani, waliosimamia ubatizo kina nani.

Utakuta age ya hawa akina Mama Maria Nyerere serikali haina document yoyote kujua alizaliwa lini ila kanisa linajua. Sasa cha ajabu nini kanisa kutaka kuombea waumini?
 
Mimi kama muislamu nitatoa ushirikiano kwa asilimia miamoja kwa viongozi wa TEC.huu unyama haupaswi kunyamaziwa nahaujali dini maana tumeuliwa mpaka mashehe wetu sisi waislamu.
Tukinyamza itakuwa ndio TABIA yao SUGU.

Kuzima MITANDAO na KUUA watu KIKATILI, halafu wanalazimisha MAISHA yaendelee.

Lazima haya mahuni yalipe, YAWAJIBIKE ili hali hii isijirudie.

Hawajauawa PANZI.
 
Back
Top Bottom