Kanisa Katoliki lapoteza Mapadri 25 na Watawa 60 kwa tatizo la upumuaji ndani ya miezi miwili

Ifike nyakati tuamke akili ya mtu mmoja na mawazo yake haviwezi kuongoza mamilioni ya watu bila ya kuwa na watu sahihi nyuma yake yeye qnajiona ndiye mtu mwenye akili kubwa ni dhambi sana
 
Nikisoma unayoandika Naona moja Kati ya haya mawili
1. Umetoroka Mirembe Hospital
2. Umetoka kunywa gongo Bila kula, kisha ukavuta bangi

Ukapitiliza na kuja JF kutoa pumba zako
 
Usilifanye jambo 'serious' kiasi hiki kuwa rahisi namna hii ulivyolielezea hapa.

"...huyo anayekudanganya hakuna corona...".

Huyu pamoja na kwamba "hatakuwa na msaada wowote kwa familia...", hawezi kujiondoa kwenye wajibu alioshindwa kuutimiza.

Kwa hiyo sio jambo rahisi tu la kusema "wananchi tuchukue tahadhari...".

Wakati wananchi wakichukua tahadhari dhidi ya corona, wasipuuze pia kuchukua tahadhari kwa wanaoshindwa kutimiza wajibu kwa wananchi wao.
 
Utatuzi unaanza kwa kukubali tatizo lipo na kutoa data.

Huko kote ulikotaja wamekubali tatizo lipo na wametoa data.

Tanzania serikali haitaki kutoa data, hili ni tatizo, ndiyo maana makanisa yanaanza kuona bora yatoe data zao.

Ushaelewa somo?
 
Kunawa mikono ipo tangu zamani ni wewe tu na akili yako ila padri hakuvaa barakoa hata kwenye kupaka majivu ile jumatano hakuvaa.
huko kwenu hakukuwa na mabadiliko? Huku kwetu kulikuwa na full sanitizer na barakoa na padre alikuwa ndo anaongoza ibada huku amevaa barakoa
 
Je unataka kusema kuwa sisi hapa Tanzania hatujapambana? Au unataka mpaka tufanye copy and paste kama wanavyofanya mataifa mengine bila kuangalia hali halisi ya mazingira yetu?

Mbona wale unaowasifu ndio wameathirika zaidi? Tutawezaje kuiga mbinu ambazo waliozitumia hazikuwasaidia kivile?

Tanzania tumepambana kivyetu kwa kumtanguliza Mungu na kwa kuchukua tahadhari zilizo katika uwezo wetu na zinaendana na mazingira yetu na zimetusaidia Sana!! Mungu ametuponya na ataendelela kutuponya!!
 
H
Kumbuka pia population ya Marekani ni zaidi ya watu 332,000,000 (milioni mia tatu thelethini na mbili). Jaribu kuweka uwiano wa waliokufa na population yake, kwa Marekani na kwa Tanzania
Hata kwa kufuata uwiano, kwa kila watu 100,000/= walioathirika ni wengi sana na waliokufa ni wengi sana!!
 
Kunawa mikono ipo tangu zamani ni wewe tu na akili yako ila padri hakuvaa barakoa hata kwenye kupaka majivu ile jumatano hakuvaa.
Labda huko kwenu ila huku kwetu alivaa plus waumini tunavaa barakoa na ibada ni fupi fupi hakuna kuimba kwaya.
 
Utatuzi unaanza kwa kukubali tatizo lipo na kutoa data.

Huko kote ulikotaja wamekubali tatizo lipo na wametoa data.

Tanzania serikali haitaki kutoa data, hili ni tatizo, ndiyo maana makanisa yanaanza kuona bora yatoe data zao.

Ushaelewa somo?
Ni vigumu sana kumfanya mtu kama huyo kuelewa somo kama hilo ulilompa, kwa sababu yeye tayari analo jibu; hata kama si jibu sahihi ambalo ni kinyume na somo sahihi analopewa.
 
AISEE TAKWIMU NI KUBWA SANA HIZI NA VIONGOZI BADO HAWATAKI KU ADMIT KUWA UGONJWA UPO ILI TUCHUKUE TAHADHARI.

HUKO WALIKO WANAONA AIBU KUKUBALIANA NA UKWELI KUWA CORONA INAUA WAPENDWA WETU.
Ulimsikia nani akizuia watu kuchukua tahadhari?
 
We unatetea nini wakati Tz haitoi takwimu !!. America unaowasema kila siku wanatoa takwimu zisizo na uongo.

Corona ipo na inakula vichwa ipendavyo . Na kama hujaguswa kwa namna yoyote una bahati ya mtende
 
Umejuaje kuwa Tanzania hatujaathirika Sana? Kwani tumeathirika kwa kiasi gani ambacho wewe unakiona si kuathirika Sana? Embu Tupe takwimu tulinganishe?
 
Huyu aliyetoa hii takwimu atawajibika kwa taharuki na hofu inayoonekana kuibuka pasipo sababu yoyote!

Hivi ni kweli kwa miezi miwili kwa Tanzania nzima kwa sababu mbalimbali (unazoweza kufikiria kama ajali, magonjwa nk) ikiwemo changamoto ya upumuaji (na si kila changamoto ya upumuaji ni corona), kufariki kiasi hicho kwa jamii hiyo ni ajabu?

Je kabla ya corona walikuwa hawafi au walikuwa wanakufa wangapi?
Hivi ukiuliza kwa nchi zingine kama Marekani watu wa jamii hiyo (mapadri na masista) kwa miezi miwili wamekufa wangapi?? Kama ukipata hiyo takwimu utamshukuru Sana Mungu kuwa kuihifadhi Tanzania dhidi ya Corona!!
 
Ni sawa kabisa haikatazwi mkuu. Sijawahi kushuhudia mtu akipelekwa polisi kwa kosa la kuvaa barakoa.

Tatizo ni mihemko ya watu kila tamko la corona wanataka kuligeuza kisiasa zaidi. Jilinde linda na uwapendao.
labda huko kwenu ila huku kwetu alivaa plus waumini tunavaa barakoa na ibada ni fupi fupi hakuna kuimba kwaya.
 
Kanisa limepoteza Imani hivyo wanavuna walichopanda.

Tunasahau hata wimbi la Kwanza hatukulishinda kwa nguvu zetu.

Petro alianza kuzama majini baada ya kupoteza imani.
Kujitoa ufahamu haikuwahi kuwa solution ya tatizo lolote
 
We unatetea nini wakati Tz haitoi takwimu !!. America unaowasema kila siku wanatoa takwimu zisizo na uongo.

Corona ipo na inakula vichwa ipendavyo . Na kama hujaguswa kwa namna yoyote una bahati ya mtende
Hauhitaji takwimu ili kujua kiwango cha vifo vya Corona maana vinatokea kwenye jamii tunayoishi pamoja!! Vikiwa vingi utajua tu! Tumshukuru Mungu hatujafika huko, na tuombe tusifike huko!! Takwimu hazikusaidii mtu binafsi!
 
Ni sawa kabisa haikatazwi mkuu. Sijawahi kushuhudia mtu akipelekwa polisi kwa kosa la kuvaa barakoa.

Tatizo ni mihemko ya watu kila tamko la corona wanataka kuligeuza kisiasa zaidi. Jilinde linda na uwapendao.
Hivi hawa maaskofu kama wako serious kwanini wasifunge kabisa makanisa? Kwani kuna mtu atawazuia?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…