Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nikisoma unayoandika Naona moja Kati ya haya mawiliBiblia inatamka wazi kuwa hukumu itaanzia nyumba ya Mungu sababu haimpi utukufu Mungu sasa hivi kwenye Corona wanasayansi ndio wanapewa utukufu na maaskofu masista wachungaji na mapadre tujiandae kuzika wengi zaidi ya hao kuanzia maaskofu mapadre wachungaji masista nk hawa waliokufa cha mtoto .Narudia hukumu ya Mungu imeanza kanisani.Yeyote asiyekiri Mungu Kuwa Bwana na Mwokozi kwenye Corona ajiandae kuondoka na Corona.Watengeneze mambo yao saa yeyote wanaondoka
Usilifanye jambo 'serious' kiasi hiki kuwa rahisi namna hii ulivyolielezea hapa... what a saddest moment! Wapumzike kwa amani. Corona ipo; wananchi tuchukue tahadhari tujiepushe na kauli za wanasiasa matapeli! Ukifa umekufa wewe ni simamnzi kwa familia yako huyo anayekudanganya hakuna Corona wala hatakuwa na msaada wowote kwa familia yako in your absence!
Utatuzi unaanza kwa kukubali tatizo lipo na kutoa data.Marekani wamekufa, Italia wamekufa, wazungu wengi wamekufa na wanaendelea kufa. Hawa ndiyo wataalamu na wanasayansi wa dunia, wanajua kujihami kuliko sisi, na watu makini na wenye maendeleo kuliko sisi. Hawa watu wameweka lockdown lakini korona imewafuata mpaka majumbani, hata viongozi wa nchi zao wamepatwa na huu ugonjwa. Swali ni Je? Nini unaweza kuwa utatuzi? Tusaidiane kutafakari tusiache misimamo ya kisiasa itutawale.
huko kwenu hakukuwa na mabadiliko? Huku kwetu kulikuwa na full sanitizer na barakoa na padre alikuwa ndo anaongoza ibada huku amevaa barakoa
Huko nako wametangaza sala na kujifukizia?Marekani wamekufa watu nusu milioni. Vipi kule nako ukweli ukoje?
Je unataka kusema kuwa sisi hapa Tanzania hatujapambana? Au unataka mpaka tufanye copy and paste kama wanavyofanya mataifa mengine bila kuangalia hali halisi ya mazingira yetu?Ungekuwa unafuatilia ungejua kuwa pamoja na kufa wengi bado wanapambana sana,yaani hakuna kujibweteka na kusema hatujui cha kufanya.na kwa sasa wameshapewa chanjo na wanaanza kuondoa lockdown pole pole.makadilio yao ni kuwa june mambo yatakuwa mswano na kurudi hali ya kawaida.
Kupatikana kwa chanjo pia ni juhudi kubwa.
Hata kwa kufuata uwiano, kwa kila watu 100,000/= walioathirika ni wengi sana na waliokufa ni wengi sana!!Kumbuka pia population ya Marekani ni zaidi ya watu 332,000,000 (milioni mia tatu thelethini na mbili). Jaribu kuweka uwiano wa waliokufa na population yake, kwa Marekani na kwa Tanzania
Labda huko kwenu ila huku kwetu alivaa plus waumini tunavaa barakoa na ibada ni fupi fupi hakuna kuimba kwaya.Kunawa mikono ipo tangu zamani ni wewe tu na akili yako ila padri hakuvaa barakoa hata kwenye kupaka majivu ile jumatano hakuvaa.
Ni vigumu sana kumfanya mtu kama huyo kuelewa somo kama hilo ulilompa, kwa sababu yeye tayari analo jibu; hata kama si jibu sahihi ambalo ni kinyume na somo sahihi analopewa.Utatuzi unaanza kwa kukubali tatizo lipo na kutoa data.
Huko kote ulikotaja wamekubali tatizo lipo na wametoa data.
Tanzania serikali haitaki kutoa data, hili ni tatizo, ndiyo maana makanisa yanaanza kuona bora yatoe data zao.
Ushaelewa somo?
Ulimsikia nani akizuia watu kuchukua tahadhari?AISEE TAKWIMU NI KUBWA SANA HIZI NA VIONGOZI BADO HAWATAKI KU ADMIT KUWA UGONJWA UPO ILI TUCHUKUE TAHADHARI.
HUKO WALIKO WANAONA AIBU KUKUBALIANA NA UKWELI KUWA CORONA INAUA WAPENDWA WETU.
We unatetea nini wakati Tz haitoi takwimu !!. America unaowasema kila siku wanatoa takwimu zisizo na uongo.Hao mapadri na masista waliofariki ni kwa sababu mbali mbali ikiwemo changamoto ya upumuaji (Na si kila changamoto ya upumuaji ni corona). Halafu ni Takwimu ya Tanzania nzima kwa miezi miwili!! Si kwa siku moja au wiki moja kwa jimbo moja!!
Kwa hiyo si ajabu sana maana vifo kwa kiwango hicho hata kabla ya Corona watu walikuwa wanafariki kwa sababu mbali mbali ikiwemo matatizo ya upumuaji. Matatizo ya upumuaji hayakuanzia kwenye corona!! Ukitaka kujua kuwa mkono wa Mungu bado unatuhifadhi, uliza nchi kama ya Marekani kuwa kwa miezi miwili ni mapadri na masista wangapi wamefariki katika kipindi Cha miezi miwili?
Ila tahadhari tuchukue, bila kutishana!! Serikali iliacha kuweka takwimu hadharani maana zilikuwa zinatumiwa na maadui wa Taifa kupandikiza hofu kwa watu!! Tayari hii takwimu ya vifo vya mapadri na masista tayari watu washaanza kuitumia kupandikiza hofu na kutoa taswira potofu kuhusu kiwango cha tatizo la corona!
Niwaombe watanzania wenzangu, tujizuie kutoa takwimu ambazo kwanza hauna uhakika nazo, (kwamba wamekufa ni sawa lakini nini sababu ya kufa kwao, hauna uhakika!).
Umejuaje kuwa Tanzania hatujaathirika Sana? Kwani tumeathirika kwa kiasi gani ambacho wewe unakiona si kuathirika Sana? Embu Tupe takwimu tulinganishe?Je unataka kusema kuwa sisi hapa Tanzania hatujapambana? Au unataka mpaka tufanye copy and paste kama wanavyofanya mataifa mengine bila kuangalia hali halisi ya mazingira yetu?
Mbona wale unaowasifu ndio wameathirika zaidi? Tutawezaje kuiga mbinu ambazo waliozitumia hazikuwasaidia kivile?
Tanzania tumepambana kivyetu kwa kumtanguliza Mungu na kwa kuchukua tahadhari zilizo katika uwezo wetu na zinaendana na mazingira yetu na zimetusaidia Sana!! Mungu ametuponya na ataendelela kutuponya!!
labda huko kwenu ila huku kwetu alivaa plus waumini tunavaa barakoa na ibada ni fupi fupi hakuna kuimba kwaya.
Kujitoa ufahamu haikuwahi kuwa solution ya tatizo loloteKanisa limepoteza Imani hivyo wanavuna walichopanda.
Tunasahau hata wimbi la Kwanza hatukulishinda kwa nguvu zetu.
Petro alianza kuzama majini baada ya kupoteza imani.
Baada ya kutotangaza hawajafa?Huko nako wametangaza sala na kujifukizia?
Hauhitaji takwimu ili kujua kiwango cha vifo vya Corona maana vinatokea kwenye jamii tunayoishi pamoja!! Vikiwa vingi utajua tu! Tumshukuru Mungu hatujafika huko, na tuombe tusifike huko!! Takwimu hazikusaidii mtu binafsi!We unatetea nini wakati Tz haitoi takwimu !!. America unaowasema kila siku wanatoa takwimu zisizo na uongo.
Corona ipo na inakula vichwa ipendavyo . Na kama hujaguswa kwa namna yoyote una bahati ya mtende
Hivi hawa maaskofu kama wako serious kwanini wasifunge kabisa makanisa? Kwani kuna mtu atawazuia?Ni sawa kabisa haikatazwi mkuu. Sijawahi kushuhudia mtu akipelekwa polisi kwa kosa la kuvaa barakoa.
Tatizo ni mihemko ya watu kila tamko la corona wanataka kuligeuza kisiasa zaidi. Jilinde linda na uwapendao.
Kwanini wasifunge kabisa makanisa ili tuone kweli wako serious kuliko hii ya kuallamika tu?Kujitoa ufahamu haikuwahi kuwa solution ya tatizo lolote