Kanisa Katoliki lapoteza Mapadri 25 na Watawa 60 kwa tatizo la upumuaji ndani ya miezi miwili

Kanisa Katoliki lapoteza Mapadri 25 na Watawa 60 kwa tatizo la upumuaji ndani ya miezi miwili

Ifike nyakati tuamke akili ya mtu mmoja na mawazo yake haviwezi kuongoza mamilioni ya watu bila ya kuwa na watu sahihi nyuma yake yeye qnajiona ndiye mtu mwenye akili kubwa ni dhambi sana
 
Biblia inatamka wazi kuwa hukumu itaanzia nyumba ya Mungu sababu haimpi utukufu Mungu sasa hivi kwenye Corona wanasayansi ndio wanapewa utukufu na maaskofu masista wachungaji na mapadre tujiandae kuzika wengi zaidi ya hao kuanzia maaskofu mapadre wachungaji masista nk hawa waliokufa cha mtoto .Narudia hukumu ya Mungu imeanza kanisani.Yeyote asiyekiri Mungu Kuwa Bwana na Mwokozi kwenye Corona ajiandae kuondoka na Corona.Watengeneze mambo yao saa yeyote wanaondoka
Nikisoma unayoandika Naona moja Kati ya haya mawili
1. Umetoroka Mirembe Hospital
2. Umetoka kunywa gongo Bila kula, kisha ukavuta bangi

Ukapitiliza na kuja JF kutoa pumba zako
 
.. what a saddest moment! Wapumzike kwa amani. Corona ipo; wananchi tuchukue tahadhari tujiepushe na kauli za wanasiasa matapeli! Ukifa umekufa wewe ni simamnzi kwa familia yako huyo anayekudanganya hakuna Corona wala hatakuwa na msaada wowote kwa familia yako in your absence!
Usilifanye jambo 'serious' kiasi hiki kuwa rahisi namna hii ulivyolielezea hapa.

"...huyo anayekudanganya hakuna corona...".

Huyu pamoja na kwamba "hatakuwa na msaada wowote kwa familia...", hawezi kujiondoa kwenye wajibu alioshindwa kuutimiza.

Kwa hiyo sio jambo rahisi tu la kusema "wananchi tuchukue tahadhari...".

Wakati wananchi wakichukua tahadhari dhidi ya corona, wasipuuze pia kuchukua tahadhari kwa wanaoshindwa kutimiza wajibu kwa wananchi wao.
 
Marekani wamekufa, Italia wamekufa, wazungu wengi wamekufa na wanaendelea kufa. Hawa ndiyo wataalamu na wanasayansi wa dunia, wanajua kujihami kuliko sisi, na watu makini na wenye maendeleo kuliko sisi. Hawa watu wameweka lockdown lakini korona imewafuata mpaka majumbani, hata viongozi wa nchi zao wamepatwa na huu ugonjwa. Swali ni Je? Nini unaweza kuwa utatuzi? Tusaidiane kutafakari tusiache misimamo ya kisiasa itutawale.
Utatuzi unaanza kwa kukubali tatizo lipo na kutoa data.

Huko kote ulikotaja wamekubali tatizo lipo na wametoa data.

Tanzania serikali haitaki kutoa data, hili ni tatizo, ndiyo maana makanisa yanaanza kuona bora yatoe data zao.

Ushaelewa somo?
 
Kunawa mikono ipo tangu zamani ni wewe tu na akili yako ila padri hakuvaa barakoa hata kwenye kupaka majivu ile jumatano hakuvaa.
huko kwenu hakukuwa na mabadiliko? Huku kwetu kulikuwa na full sanitizer na barakoa na padre alikuwa ndo anaongoza ibada huku amevaa barakoa
 
Ungekuwa unafuatilia ungejua kuwa pamoja na kufa wengi bado wanapambana sana,yaani hakuna kujibweteka na kusema hatujui cha kufanya.na kwa sasa wameshapewa chanjo na wanaanza kuondoa lockdown pole pole.makadilio yao ni kuwa june mambo yatakuwa mswano na kurudi hali ya kawaida.

Kupatikana kwa chanjo pia ni juhudi kubwa.
Je unataka kusema kuwa sisi hapa Tanzania hatujapambana? Au unataka mpaka tufanye copy and paste kama wanavyofanya mataifa mengine bila kuangalia hali halisi ya mazingira yetu?

Mbona wale unaowasifu ndio wameathirika zaidi? Tutawezaje kuiga mbinu ambazo waliozitumia hazikuwasaidia kivile?

Tanzania tumepambana kivyetu kwa kumtanguliza Mungu na kwa kuchukua tahadhari zilizo katika uwezo wetu na zinaendana na mazingira yetu na zimetusaidia Sana!! Mungu ametuponya na ataendelela kutuponya!!
 
H
Kumbuka pia population ya Marekani ni zaidi ya watu 332,000,000 (milioni mia tatu thelethini na mbili). Jaribu kuweka uwiano wa waliokufa na population yake, kwa Marekani na kwa Tanzania
Hata kwa kufuata uwiano, kwa kila watu 100,000/= walioathirika ni wengi sana na waliokufa ni wengi sana!!
 
Kunawa mikono ipo tangu zamani ni wewe tu na akili yako ila padri hakuvaa barakoa hata kwenye kupaka majivu ile jumatano hakuvaa.
Labda huko kwenu ila huku kwetu alivaa plus waumini tunavaa barakoa na ibada ni fupi fupi hakuna kuimba kwaya.
 
Utatuzi unaanza kwa kukubali tatizo lipo na kutoa data.

Huko kote ulikotaja wamekubali tatizo lipo na wametoa data.

Tanzania serikali haitaki kutoa data, hili ni tatizo, ndiyo maana makanisa yanaanza kuona bora yatoe data zao.

Ushaelewa somo?
Ni vigumu sana kumfanya mtu kama huyo kuelewa somo kama hilo ulilompa, kwa sababu yeye tayari analo jibu; hata kama si jibu sahihi ambalo ni kinyume na somo sahihi analopewa.
 
AISEE TAKWIMU NI KUBWA SANA HIZI NA VIONGOZI BADO HAWATAKI KU ADMIT KUWA UGONJWA UPO ILI TUCHUKUE TAHADHARI.

HUKO WALIKO WANAONA AIBU KUKUBALIANA NA UKWELI KUWA CORONA INAUA WAPENDWA WETU.
Ulimsikia nani akizuia watu kuchukua tahadhari?
 
Hao mapadri na masista waliofariki ni kwa sababu mbali mbali ikiwemo changamoto ya upumuaji (Na si kila changamoto ya upumuaji ni corona). Halafu ni Takwimu ya Tanzania nzima kwa miezi miwili!! Si kwa siku moja au wiki moja kwa jimbo moja!!
Kwa hiyo si ajabu sana maana vifo kwa kiwango hicho hata kabla ya Corona watu walikuwa wanafariki kwa sababu mbali mbali ikiwemo matatizo ya upumuaji. Matatizo ya upumuaji hayakuanzia kwenye corona!! Ukitaka kujua kuwa mkono wa Mungu bado unatuhifadhi, uliza nchi kama ya Marekani kuwa kwa miezi miwili ni mapadri na masista wangapi wamefariki katika kipindi Cha miezi miwili?
Ila tahadhari tuchukue, bila kutishana!! Serikali iliacha kuweka takwimu hadharani maana zilikuwa zinatumiwa na maadui wa Taifa kupandikiza hofu kwa watu!! Tayari hii takwimu ya vifo vya mapadri na masista tayari watu washaanza kuitumia kupandikiza hofu na kutoa taswira potofu kuhusu kiwango cha tatizo la corona!
Niwaombe watanzania wenzangu, tujizuie kutoa takwimu ambazo kwanza hauna uhakika nazo, (kwamba wamekufa ni sawa lakini nini sababu ya kufa kwao, hauna uhakika!).
We unatetea nini wakati Tz haitoi takwimu !!. America unaowasema kila siku wanatoa takwimu zisizo na uongo.

Corona ipo na inakula vichwa ipendavyo . Na kama hujaguswa kwa namna yoyote una bahati ya mtende
 
Je unataka kusema kuwa sisi hapa Tanzania hatujapambana? Au unataka mpaka tufanye copy and paste kama wanavyofanya mataifa mengine bila kuangalia hali halisi ya mazingira yetu?
Mbona wale unaowasifu ndio wameathirika zaidi? Tutawezaje kuiga mbinu ambazo waliozitumia hazikuwasaidia kivile?
Tanzania tumepambana kivyetu kwa kumtanguliza Mungu na kwa kuchukua tahadhari zilizo katika uwezo wetu na zinaendana na mazingira yetu na zimetusaidia Sana!! Mungu ametuponya na ataendelela kutuponya!!
Umejuaje kuwa Tanzania hatujaathirika Sana? Kwani tumeathirika kwa kiasi gani ambacho wewe unakiona si kuathirika Sana? Embu Tupe takwimu tulinganishe?
 
Huyu aliyetoa hii takwimu atawajibika kwa taharuki na hofu inayoonekana kuibuka pasipo sababu yoyote!

Hivi ni kweli kwa miezi miwili kwa Tanzania nzima kwa sababu mbalimbali (unazoweza kufikiria kama ajali, magonjwa nk) ikiwemo changamoto ya upumuaji (na si kila changamoto ya upumuaji ni corona), kufariki kiasi hicho kwa jamii hiyo ni ajabu?

Je kabla ya corona walikuwa hawafi au walikuwa wanakufa wangapi?
Hivi ukiuliza kwa nchi zingine kama Marekani watu wa jamii hiyo (mapadri na masista) kwa miezi miwili wamekufa wangapi?? Kama ukipata hiyo takwimu utamshukuru Sana Mungu kuwa kuihifadhi Tanzania dhidi ya Corona!!
 
Ni sawa kabisa haikatazwi mkuu. Sijawahi kushuhudia mtu akipelekwa polisi kwa kosa la kuvaa barakoa.

Tatizo ni mihemko ya watu kila tamko la corona wanataka kuligeuza kisiasa zaidi. Jilinde linda na uwapendao.
labda huko kwenu ila huku kwetu alivaa plus waumini tunavaa barakoa na ibada ni fupi fupi hakuna kuimba kwaya.
 
Kanisa limepoteza Imani hivyo wanavuna walichopanda.

Tunasahau hata wimbi la Kwanza hatukulishinda kwa nguvu zetu.

Petro alianza kuzama majini baada ya kupoteza imani.
Kujitoa ufahamu haikuwahi kuwa solution ya tatizo lolote
 
We unatetea nini wakati Tz haitoi takwimu !!. America unaowasema kila siku wanatoa takwimu zisizo na uongo.

Corona ipo na inakula vichwa ipendavyo . Na kama hujaguswa kwa namna yoyote una bahati ya mtende
Hauhitaji takwimu ili kujua kiwango cha vifo vya Corona maana vinatokea kwenye jamii tunayoishi pamoja!! Vikiwa vingi utajua tu! Tumshukuru Mungu hatujafika huko, na tuombe tusifike huko!! Takwimu hazikusaidii mtu binafsi!
 
Ni sawa kabisa haikatazwi mkuu. Sijawahi kushuhudia mtu akipelekwa polisi kwa kosa la kuvaa barakoa.

Tatizo ni mihemko ya watu kila tamko la corona wanataka kuligeuza kisiasa zaidi. Jilinde linda na uwapendao.
Hivi hawa maaskofu kama wako serious kwanini wasifunge kabisa makanisa? Kwani kuna mtu atawazuia?
 
Back
Top Bottom